Watanzania wa ajabu, mafanikio kidogo, kelele utadhani wametenda maajabu ya dunia

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,077
Watanzania walio wengi wanaugua ugonjwa wa unafiki. Na hawa wanafiki ambao siku hizi wanaitwa machawa, wakati wote hutafuta vitu vidogo vidogo ili waisifu Serikali, wamsifu Rais au waisifu CCM. Hata vitu vya kawaida vikifanyika, watatoa sifa unaweza kudhani labda tumefanya ugunduzi ambao Dunia nzima ilikuwa haijawahi kufanya.

Jana tumeambiwa kuwa mlango mmoja wa bwawa la Nyerere, wa kufua umeme umefunguliwa na kuanza kuzalisha umeme. Tunashukuru kwa hilo kuwezekana maana inaweza kupunguza madhira makubwa ambayo Watanzania wamekuwa wakiyapitia kwa kuwekwa kwenye mgao mkali wa umeme kwa zaidi ya mwaka mzima. Lakini hakuna kikubwa cha kusherehekea. Bwawa hili likizalisha sawasawa, maximum generation capacity yame itakuwa 2,115MW. Ukimjulisha na generation capacity tuliyokuwa nayo ya 1,938MW, tutakuwa na total generation capacity ya 4,053MW. Huo utakuwa ndio uwezo wa mwisho wa uzalishaji kama kila chamzo na kila mtambo vikafanya kwa ufanisi wa 100%. Lakini kwa poor efficiency ya TANESCO kama zilivyo taasisi zote za Serikali, hawatazidi 70% ya capacity, ambayo ina maana haitazidi 2,837MW.

Wakati sisi tunapiga kelele na kushangilia kama vile tumefanya maajabu, nchi nyingi, tena za Afrika hii hii wanazalisha umeme kama huo na nyingine kutuzidi kwa mbali sana:

Nigeria yenye watu milioni 213 , ina installed capacity 22,000 MW.

South Africa yenye watu milioni 59 inaninsatlled capacity 58,095MW

Ghana yenye watu milioni 32 ina insatlled capacity 5,134MW

Mozambique yenye watu milioni 32 ina installed capacity 2,780MW

Kenya yenye watu milioni 53 ina installed Capacity 3,300 MW.

Zambia yenye watu milion 19 ina installed capacity 3,356MW

Ninachotaka kusema kuwa hata kama Bwawa la Nyerere litazalisha MW zote 2,115, siyo maajabu na wala haimaanishi tumetatua tatizo forever. Ikumbukwe kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa matano yanayoongoza kwa kuzaliana katika Africa. Hivyo muda si mrefu, kwa vile sisi ni watu ambao huwa hatuna mipango, kwa kuzingatia ongezeko la watu, ongezeko la shughuli za kiuchumi, ufanisi mbaya wa TANESCO, ukame, na udhaifu wa Serikali katika kuisimamia TANESCO, haitapita muda mrefu, tutarudi kwenye matatizo haya haya ya kukosa umeme.

Kuwashwa kwa umeme wa Bwawa la Nyerere isiwe sababu ya kupeana sifa za kupitiliza, isiwe sababu ya Serikali na TANESCO kubweteka bali muda huu utumike kufikiria na kutekeleza miradi mipya ya umeme ili angalao tufikie 10,000MW. Tulisherehekea hivyo hivyo tulivyoanza kuzalisha umeme bwawa la Mtera, Kihansi na baadaye wa gas, lakini ikawa ni sherehe ya muda mfupi.

Yatupasa kufikiria miaka 50 mbele.
 
Watanzania wengi ni watu wenye viwango vya chini sana vya matarajio [low expectations].

Hivyo, sioni ajabu wao kusherehekea vitu vidogo vidogo.

Licha hivyo, mimi siamini hayo maneno ya kwamba mgawo/ shida ya umeme sasa basi.

Maneno kama hayo nimeanza kuyasikia siku nyingi sana….zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Nitaamini pale nitapoona kweli sasa shida ya umeme imekuwa historia.

Nje ya hapo, sidanganyiki na maneno hewa ya viongozi wa CCM.
 
wana-CCM wengi wana reasoning capacity ndogo sana sana, na wako comfortable kushangilia ujinga kila uchao. Kwa mfano, Treni iliyojaribiwa leo, tumeambiwa tena kwa uwazi kabisa kuwa Umeme ulikatika mara kadhaa treni ikiwa safarini na kwamba hata AC za treni kuna muda hazikufanya kazi, ila haya mapungufu hatuyaoni, tuna kazi ya kushangilia ujinga tu. Designing na Project document inasoma Treni itakua ya 160km/hr hii imetembea roughly kwa 80km/hr na bado tunakenua, HATUHOJI as if ni jambo la kawaida/.

ukiuliza kulikoni wanakuja akina Pascal and Comapny wanasema Mjifunze "kushukuru hata kwa Kidogo" as if hizi fedha hazituhusu. Pumbafu kabisa, kuzaliwa Tanzania kisha kutawaliwa na CCM ni kama bahati mbaya hivi.
 
Watanzania wengi ni watu wenye viwango vya chini sana!
wanatoa elimu duni ili tusiweze kuwaza kwa uwanda tofauti ndugu yangu, siku hizi mitihani ni ya multiple choice, yaani mitihani ni kama betting tu
 
Watanzania wengi ni watu wenye viwango vya chini sana!

Hivyo, sioni ajabu wao kusherehekea vitu vidogo vidogo.

Licha hivyo, mimi siamini hayo maneno ya kwamba mgao/ shida ya umeme sasa basi.

Maneno kama hayo nimeanza kuyasikia siku nyingi sana….zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Nitaamini pale nitapoona kweli sasa shida ya umeme imekuwa historia.

Nje ya hapo, sidanganyiki na maneno hewa ya viongozi wa CCM.

Upo sahihi sana. Muda si mrefu tutatengenezewa hadithi nyingine. Na ikifika mwezi wa September, tutaambuwa maji yamepungua, alimradi tu wapate sababu, hata kama siyo halisia.
 
Nadhani ni wanaccm wenyewe ndiyo wenye matatizo. Kwasabb hata wanaosifia ni wanaccm (machawa).
 
wanatoa elimu duni ili tusiweze kuwaza kwa uwanda tofauti ndugu yangu, siku hizi mitihani ni ya multiple choice, yaani mitihani ni kama betting tu
Mitihani ya multiple choice si tatizo. Marekani hadi kwenye vyuo vikuu mitihani ya multiple choice ipo!

Tatizo letu ni zaidi ya elimu ya darasani.
 
Blah blah nyingiii kutoka kwa viongozi

Na siku hiyo rais akienda huko mtegeme na tamasha juu wasani wakitumbuiza

Ova
 
Siasa zetu zimepelekea wenzetu watake sifa/kusifia zaidi ya wanavyoyahitaji maendeleo yenyewe
 
Upo sahihi sana. Muda si mrefu tutatengenezewa hadithi nyingine. Na ikifika mwezi wa September, tutaambuwa maji yamepungua, alimradi tu wapate sababu, hata kama siyo halisia.
Sinema itaendelea

Ova
 
Back
Top Bottom