Maajabu ya kutisha ya Mto Rutale (Chemchem ya Rutale) - Kigoma Ujiji

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
May 25, 2021
229
593
Miondoko hii ya maandishi haijafanyiwa utafiti wowote bali ni nadharia za kusikika kutoka kwa mashuhuda mbalimbali kunako mtikisiko wa maajabu ya chemchem hii kongwe ya Kanyabeza inayopatikana eneo la Rutale, pia unaweza kuita chemchemya Rutale hivyo unaruhusiwa kupinga au kukubali, kupunguza au kuongeza pale kwenye mapungufu.

1663790577097.png


Rutale ni jina la chechem inayopatikana mkoani Kigoma, manispaa ya Kigoma Ujiji, kata ya Kipampa, eneo linaloitwa Rutale ambalo lipo karibu kabisa na ziwa Tanganyika mwambao wa Ujiji.
Jina Rutale inasemekana lilitokana na mkazi mmoja aliekuwa akiishi mahala hapo miaka mingi iliyopita, watu walikuwa wakija kuchota maji kwenye chemchem hii walikuwa wakisema tunakwenda kuchota maji kwa Rutale.

1663790658093.png


Maji yake ni mazuri kwa kunywa, yenye baridi ya asili na yenye utulivu kwenye koo ambayo hukuacha na ladha itayokufanya uyakumbuke na kuyahitaji tena baadae. Sifa ya kipekee ya mto huu hata mvua inyeshe namna gani maji yake hayachafuki abadan, chemchem hii haijawahi kukauka tangu kuumbwa kwake, inatiririsha maji yake kuelekea ziwa Tanganyika ambapo pembezoni mwa mfereji kumelimwa nyanya na mazao mbalimbali, kilimo cha nyanya eneo hili kinakubali mno ikiwa tu nyanya zitamwagiliziwa kwa maji ya rutale. Barabara ya Rutale inatokea kwenye barabara kuu ya Kigoma Ujiji sehemu inayoitwa 'Bimala'

1663790797040.png


Inasemekana mnamo miaka ya 1950 eneo hili lilikuwa linaaminika kuwepo kwa joka kubwa lenye pete ya dhahabu mkiani, nyoka huyu alikuwa akifanya safari zake baina ya Rutale na pori la uwanja wa Lake Tanganyika enzi hizo, inamaanisha huyu nyoka alikuwa akisafiri kutoka eneo hilo la rutale na kuvuka barabara ya Kigoma ujiji sehemu inayoitwa Mnarani, kwenye kona ambayo ukichomoza na gari unaanza kuiyona ujiji'

1663791293093.png



Hii ndio sehemu nyoka huyu alikuwa akivuka na hii ndio sehemu iliyokuwa ikiongoza kwa matukio ya ajali za barabarani mara kwa mara kama gari kupinduka au magari kugongana au mtu kugongwa, inasemekana ajali hizi zilikuwa zikisababishwa na nyoka huyu wakati akivuka eneo hilo ambapo akikukuta ni lazima upate ajali.

1663791151861.png


Nyoka huyu kutoka chemchem ya Rutale inasemekana pindi atokapo kunakuwa na upepo mwingi unavuma mfano wa kimbunga cha vumbi.

Nyoka huyu Rutale inasemekana alikuwa na uhusiano na nyoka wa Burega aliekuwa akienda kunywa maji kwenye mto Katubuka, nyoka wa Burega alikuwa akivuka barabara ya Kigoma Ujiji eneo la Mwanga selemala ambayo pia ni sehemu iliyokuwa ikiongoza kwa ajali za mara kwa mara. Vijana waliokuwa wakipotea kimazingara kwenye mto katubuka inakisiwa walikuwa wakichukuliwa na nyoka huyu wa Burega.

1663791467841.png


Maji ya rutale inasemekana hayafahamiki haswa yanatoka wapi, yani chemchem ilipo haifahamiki ipo wapi lakini ni eneo kwa ujumla limelozungukwa na nyasi, maji ya rutale yalikuwa yakiuzwa kwenye madebe ya bati ambapo muuzaji hubeba madebe mawili yaliyoshikiliwa na mti mgumu kwenye bega la kulia na kushoto, pia muuzaji huvaa kengere za asili miguuni pindi anapoanza kuyatembeza maji haya kwenye mitaa, kengere zinamlio wakipekee ambao huamsha masikio ya msikilizaji na kufahamu kwamba maji ya ratule yanapita,

1663791636439.png


Mzegamzega alikuwa ni yule muuza maji ya rutale ambae anabeba madebe manne, mawili bega la kulia na mawili bega la kushoto, msimulizi anatueleza kwamba mlio wa kengere hizi ulikuwa unasikika maeneo ya mto Rutale kama mlio wa ndge au wadudu ambapo wachota maji wengi wanaokwenda rutale walikuwa wakiusikia, ndipo wauza maji wakabuni kengere mfano wa mlio huo wa 'ngere, ngere, 'ngere, ngere, kwa hiyo wanunua maji mitaani wakisikia mlio huo akili hugota kwamba maji ya rutale yanapita.

1663791755872.png


Kutokana na uhaba wa maji mjini Kigoma miaka hiyo ya 1990 hupelekea watu kuwa wengi kuchota maji ya rutale kwa ajili ya matumizi, inasemekana watu wakiwa wengi jambo ambalo hupelekea kelele na fujo kuwa kubwa basi maji hugeuka na kuwa mekundu mfano wa damu, msimulizi anaeleza kwamba nyakati za jioni majira ya saa kumi na mbili kulikuwa na kiumbe kikiuonekana eneo hilo na ghafla hupotea na watu hutawanyika kwa kukimbia.

1663791880139.png


Inasemekana pia kulikuwa na mpango kabambe wa kuyadhibiti maji ya rutale, ambapo wadhamini walijenga mabomba na kuweka mifereji ili maji yatoke kwa utaratibu maalum na waweze kufanya biashara ya kuwauzia watu maji hayo, hali hii ilipelekea maji hayo kutoka yakiwa yameambatana na nyoka wengi wadogo wadogo, na baada ya nyakati maji yaligeuka rangi na kuwa mekundu, kwa hiyo zoezi la kuyadhibiti maji kwa ajili ya biashara lilisimama na watu wakaendelea kuchota maji bure kama kawaida.

1663791975056.png


Huu ndio mto rutale wenye maajabu yakusisimua, sehemu ya kutolea maji nyakati zingine maji yalikuwa yakiambatana na samaki wadowadogo wazuri sana wenye rangi za kumeremeta na wanaovutia kwa macho mfano wa samaki wa mapambo, ilikuwa hairuhusiwa kuwagusa au kuwakamata samaki hao kutokana na imani za wazee kipindi hicho, samaki hawa wazuri wenye mvuto wa kila aina ya rangi walikuwa wakiporomoka kuelekea ziwa Tanganyika na baadae hupotea.

1663792215279.png


Maji haya kwasasa yamepimwa na wataalam na pia yamethibitika kuwa yanafaa kwa afya ya binaadamu, ispokuwa sharti la kuchota maji hapa hutakiwi kugombania maji au kuleta fujo kwenye eneo hili, kwani kufanya hivyo huaminisha kutokea kwa matukio ya mauzauza. Eneo hili kwasasa linamabomba makubwa yasiyo na koki na maji humwagika masaa 24 kwa kasi ile ile, maji huchotwa kwenye mabomba, na yale maji yanayomwagika yanakwenda moja kwa moja ziwani Tanganyika.

1663792315861.png


Inasemekana idara ya maji ilileta wadhamini kuja kufunga mitambo kama mradi wa maji, kitendo cha kufanya hivyo maji ndio yalianza kubadilika nakuwa mekundu kama damu ikabidi wataalam watoe mitambo yao na kukabaki mabomba makubwa ndio hayo yapo yanamwaga maji saa 24 miaka nenda rudi. Huu ndio mto rutale, hairuhusiwi kuingia na viatu, na pia maji yake hutakatisha nguo yoyote ile chafu na kuing'arisha upya.

Kwasasa Rutale haina budi kupewa hadhi ya kuwa kama sehemu ya kivutio kwa watalii wanaofika Kigoma.
 
Nimekuwa nikisikia mara nyingi vyanzo vya maji (vijijini) vikihusishwa na nyoka sijui kwanini.

Tukuyu(Mbeya) nako kuna sehemu wanaita Kibwe ,kuna"salala" inayotokana na chemchem bibi alikuwa akitusimulia kwamba hapo kale wakazi wa kijiji kile walibaini uwepo wa joka kubwa lililokuwa lina control hicho chanzo cha maji. Nilikuwa nikisikia hizo stori hata hamu ya maji inakata.
 
Nimekuwa nikisikia mara nyingi vyanzo vya maji (vijijini) vikihusishwa na nyoka sijui kwanini.

Tukuyu(Mbeya) nako kuna sehemu wanaita Kibwe ,kuna"salala" inayotokana na chemchem bibi alikuwa akitusimulia kwamba hapo kale wakazi wa kijiji kile walibaini uwepo wa joka kubwa lililokuwa lina control hicho chanzo cha maji. Nilikuwa nikisikia hizo stori hata hamu ya maji inakata.
Ahsante na karibu sana Kigoma
 
Baada ya kusikia kasulu wanawashinda maendeleo naona kigoma mmeamka, fact ni kwamba wenzenu wa kasulu sio wavivu ni wachapa kazi,
Ahsante, kurasa huu ni kwa mkoa wa Kigoma nasio sehemu moja ya mji. Maendeleo ya Kasulu bado ni yetu sote ndugu.
 
Back
Top Bottom