GE2025 Maajabu ya Dunia! Mbona sizioni pongezi za machawa, makampuni, kulikoni?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Chibike

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
4,896
Reaction score
7,522
Tumsifu Yesu Kristu

KWANZA kabisa nawapongeza sana Kanisa katoliki angalau kwa kuweka siku maalumu ya kuombea wafu WALIOUWAWA oktoba 29. Tena kwenye barua zenu hamjakwepesha maneno.

Tukiachana na Hilo tendo la kishujaa la kanisa katoliki, nmekua napitia media outlets mbalimbali tumezoa kuona pongezi nyingi za kumwaga ambazo hua zinatolewa kwa rais alieshinda na kuapishwa...ila Sasa ni za kuhesabu au hamna kabisa, si machawa, kampuni mbalimbali watu kimyaaa...

Kulikoni..
 
Unaambiwa maandamano yaliondoka na uchawa wote,hivyo vitu vilishakufa,pongezi ajipongeze yeye na Abdul
 
Subutu yani saivi ukijidai kiherehere imekula kwako.Tunaishi kiuhalisia sasa
 
Wanahofia kuhatarisha ustawi na usalama wa wafanyakazi na mali za kampuni.
 
Taifa lipo katika kipindi cha mashaka makubwa,simanzi,hasira na sintofahamu isiyomithilika,viziwi nawasikie,vipofu nawaone kwani huenda ndiyo watakaoliponya taifa hili.Kwani wenye masikio wamekataa kusikia na wenye macho wamekataa kuona ilhali wenye akili wamezilazimisha kulala tena ajabu katika kipindi hiki cha mitihani ya utimamu wa taifa letu pendwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…