Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,553
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano.

Naomba kuanza na angalizo,
Kuna watu wana allergy na pongezi zozote kwa rais Magufuli na awamu yake ya 5, hivyo akifanya jema lolote au akipongezwa kwa zuri lolote, wao wanakasirika. Kwa vile bado tuko kwenye festival season, kama wewe ni mtu wa kundi hili, nakuomba uishie hapa ili tusiharibiane festivals seasons zetu.

Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.

Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.

Ripoti hiyo ni hii
Year in Review_ 2019-Tanzania Yaongoza.jpg


Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.

Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.

Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.

Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.

Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakapo takiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.

Maendeleo haya mazuri ya vita dhidi ya umasikini pia yamezungumzwa kwenye ripoti hii ya UNDP


Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali
Up Date.
Nimegundua Watanzania wengi sio wasomaji wa links, hivyo japo niliweka links lakini ni wachache sana waliifungua.
Kufuatia ubishi mkubwa ulioibuka katika bandiko hili swali kuu likiwa kwa nini survey ilifanywa 2011 lakini ripoti inatoka mwaka huu wa 2019, hivyo nimeamua kuwawekea ripoti yote ya umasikini, pia kuna waliofanya hizo survey pia nimekuwekea na kama una swali lolote, waulize wenyewe na sio mimi.
Which countries reduced poverty rates the most?
|NOVEMBER 12, 2019
This page in:
One of the goals of the World Bank Group is to reduce extreme poverty—defined as living on less than $1.90 per day in 2011 PPP—to less than 3% by 2030. We know that the world has seen tremendous progress in reducing extreme poverty since 1990. So, where in the world has poverty reduction been most successful?
The graph below shows 15 countries that experienced the largest annual average percentage point declines in extreme poverty rate between about 2000 and 2015, out of the 114 countries for which we can measure poverty in a comparable way over this period.

In each of these countries, an average of at least 1.6% of the population moved out of extreme poverty every year. This meant 802.1 million fewer people were living in extreme poverty in these 15 countries between 2000 and 2015. For example, between 2000 and 2011, the extreme poverty rate fell by 36.9 percentage points in Tanzania, from 86.0% to 49.1%, for an annual average rate of reduction of 3.2 percentage points, which led to a reduction of 5.3 million in the number of Tanzanians living in extreme poverty. Tajikistan, Chad, and the Republic of Congo had average reductions in poverty of around 3 percentage points per year.
While extreme poverty remains endemic in low-income and conflict-affected countries, many of which are in Sub-Saharan Africa, there is cause for optimism even in these countries. Seven of the top 15 countries are in Africa, and two are on the World Bank Group’s Harmonized List of Fragile Situations for FY19.
Some of the 15 countries (China, Kyrgyz Republic, Moldova, Vietnam) effectively eliminated extreme poverty by 2015. In others (e.g. India), low rates of extreme poverty in 2015 still translated to millions of people living in deprivation. In some of the countries in Sub-Saharan Africa (e.g. Democratic Republic of Congo, Tanzania, Burkina Faso), extreme poverty rates, even after rapid reduction, remain above 40%.
These 15 high performers make up a diverse group of countries—by geographic location, average income levels, poverty rates, and size of the population and the economy:
  • Two of these countries were lower middle-income countries in 2000 and rose to upper middle-income status by 2015; eight were low-income countries in 2000 and rose to lower middle-income status by 2015; and five remained low-income countries over the entire period.
  • The countries had vastly different poverty rates at the turn of the century—the extreme poverty rate ranged from 94.1% in DRC (2004) to 28.6% in Pakistan (2001).
  • Their populations ranged from 2 million for Namibia (2003) to 1.3 billion for China (1999).
  • The size of their economy ranged from $861 million for Tajikistan to $1.2 trillion for China in 2000, in current U.S. dollars.

Notes on Data Selection:
Data are extracted from the PovcalNet database. Two data selection criteria were applied; (1) Countries should have at least two surveys—one between 1995 and 2005 and another between 2010 and 2019. (2) The same welfare measures, either income or consumption, should be used for those surveys. Applying these restrictions, 114 countries were selected, including high-income countries.
Countries marked with * indicates that the poverty rate from the two surveys are not fully comparable. Nepal, Niger, Gambia, Guinea, Solomon Islands, and Ecuador were removed due to low confidence in their data comparability.
Kyrgyz Republic data in 2000 uses HBS survey for 2000.
Growth rate calculation uses survey year, which could be different from reference year.
Median income information is based on PovcalNet and Global Database of Shared Prosperity.
Reference: Historical country classification by income




POVERTY
=topic:303&f[1]=language:en']=topic:303&f[1]=language:en']=regions:655&f[1]=language:en']AFRICA
=topic:303&f[1]=language:en']=topic:303&f[1]=language:en']=regions:275&f[1]=language:en']EAST ASIA AND PACIFIC
=topic:303&f[1]=language:en']=topic:303&f[1]=language:en']=regions:276&f[1]=language:en']EUROPE AND CENTRAL ASIA
=topic:303&f[1]=language:en']=topic:303&f[1]=language:en']=regions:279&f[1]=language:en']SOUTH ASIA
=topic:303&f[1]=language:en']=topic:303&f[1]=language:en']=regions:280&f[1]=language:en']THE WORLD REGION
=topic:303&f[1]=language:en']=topic:303&f[1]=language:en']=series:781&f[1]=language:en']#DATAVIZ

Authors
Miyoko Asai's picture https://www.linkedin.com/in/miyoko-asai-a400a049/
Miyoko Asai
Consultant – Data Analyst
MORE BLOGS BY MIYOKO
دانيال ماهلر
Daniel Mahler
Young Professional
MORE BLOGS BY DANIEL
سيلفيا مالجيو https://www.linkedin.com/in/silvia-malgioglio-9590a127/ twitter.com/intent/follow?screen_name=@Smaljoelho
Silvia Malgioglio
Social Scientist
MORE BLOGS BY SILVIA
آمبر نارايان
Ambar Narayan
Lead Economist, Poverty Global Practice, World Bank
MORE BLOGS BY AMBAR
Minh Cong Nguyen
Minh Cong Nguyen
Senior Data Scientist, Poverty and Equity Global Practice, World Bank
MORE BLOGS BY MINH

Join the Conversation


The content of this field is kept private and will not be shown publicly

Paskali
Update 17/02/20
Shuhudieni live jinsi Awamu ya Tano inavyoondoa umasikini



P
 
Hata kama iwe 2000-2015 abadilishe tu, aseme tunaipongeza CCM kwa juhudi za kupunguza umaskini uliotopea.

Tuisubiri na ripot ya 2015-2025.... ndiyo tuitaje hii awamu pendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sababu zilizo pelekea kupunguza Umasikini ulio topea mbona hazija ainishwa !?.Ni kwa nini wame angukia tu kwenye Matokeo ambayo hata kiuhalisia hayaonekani ?

Sikubaliani kabisa na hizo Sifa zisizo stahili.
 
Back
Top Bottom