waeleze waelewe maana ya ushirikiano wa afrika mashariki ni nini? Hauwezi kuitangaza tanzania pekee ukapata wageni,kwanza kiwanja kikubwa cha ndege hatuna hizo terminal 2 za mwl nyerere int. Airport hazitoshi kurupushani ya ndege kenyata int. Airport zipo terminal kama 100 wageni wanaingia na kutoka kwa wingi,mashirika mengine makubwa ya ndege hayatui dar kutokana na ufinyu wa uwanja,hiyo hata hao wanaoitangaza tz wageni wakija wanatua kenya ndiyo wapande precision air kuja tz,haidhuru wakiitangaza serengeti au kilimanjaro wageni hawaishii kenya ni lazima wavuke mpaka kuja tz tabu iko wapi?,kenya wana shirika lao kenya airways sisi letu liko wapi?unategemea walete wageni mpaka dar kwa faida ya nani?hiyo kilimanjaro airport ndiyo usiseme hata sehemu ya kurukia ndege mashimo matupu bado wanyama kama ndege wadogo wanalala katika sehemu ya kurukia mara nyingi ndege za kimataifa zimepata hititafu kwa ndege kuingia katika turbo power engine za ndege wakati wa kuruka hasa usiku,pia umbali wa kuruka kutoka nairobi kuja kilimanjaro kwa ndege kubwa distance ni ndogo sanaaaaa,tunatakiwa kuwekeza katika miundombinu ya kuwezesha wageni kufika nchini siyo mahoteli makubwa na hifadhi nzuri tu,kenya hawana hifadhi nzuri au mahoteli mazuri kama sisi ndiyo sababu wanatangaza vivutio vyetu nao wapate maslahi kidogo na hayo ndiyo maisha,mpaka hapo nasi tutakaposhituka,tukijaribu tutaweza,kenya wana ndege inaitwa tanzanite tena boeing 787 new,sasa we jiulize hiyo tanzanite ipo kenya?au ni sisi tumewapelekea?,vikwazo tunajiwekea wenyewe kisha tunalalamika.tena wanaotangaza utalii wa tz huko kenya ni wa tz kutokana na miundombinu yetu mibovu sisi tumekalia siasa tu utendaji 0%.