Maajabu ya dunia-live ktk tv za asia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maajabu ya dunia-live ktk tv za asia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jul 22, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Kuanzia leo tarehe 22/07/2012 wanyama kutoka MASAI MARA wataanza kusafiri na kuelekea SERENGETI,wamekaa masai mara kwa miezi 3 na sasa wataenda serengeti na watakaa huko kwa miezi 8

  Tv zote za kimataifa macho yao yapo huko ili kuweza kuonyesha moja kwa moja wananchi wao jinsi wanyama hao wanavyosafiri
  na jana tu baadhi ya hizo TV ziliomba jambo hili liingizwe ktk moja ya maajabu ya dunia

  je wewe kama mtanzania,mbuga ipo tanzania unayaelewa haya? tv zetu zinaelewa haya? viongozi wetu wanaelewa haya?

  chakushangaza ni tv za asia na kenya ndizo zinaonyesha maajabu haya,wapi watanzania? baadae tusianze kulalama wenzetu wakiwa wanapeleka watalii kuangalia safari za wanyama hao kutoka serengeti kwenda masai mara na kutoka masai mara kwenda serengeti

  tanzania oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

  KWA WENYE MTANDAO ANGALIA CCTV 13 ONA HAPA LIVE

  http://cctv.cntv.cn/live/cctvxinwen/index.shtml#online

  KWA WALE MSIOELEWA KICHINA MNAWEZA ONA HII

  http://english.cntv.cn/live/
   
 2. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,316
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 180
  Good news, ngoja nifuatilie na mimi. Napenda sana habari za wanyama.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Kagasheki yupo na bi mdogo mh.mbunge ccm vijana viti maalum anakula bata na swaum hii atajulia wapi?
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Mkuu Eng. Mtolera, haya ni mambo ya awareness campaign na kuwa conscious!. Viongozi wetu na ma promoteters wetu wa utalii kila siku wanashinda ulaya wakihudhuria kwenye mafunzo, mikutano, semina, warsha, makongamano na vikao vya kukuza utalii, lakini wanachorudi nacho ni yale ma jumbo suitcases na hawa implement chochote!, kumbe wakifika kule, mawazo yao ni shopping tuu kwa zile per diem zao ndefu walizovuta!.

  Wenzetu Kenya wamelipromote tukio hili kimataifa, sasa hivi kuna malaki ya watalii nchini Kenya waliobook several months in advance ili wasikose nafasi kushuhudia maajabu haya ya dunia, cha ajabu zaidi ni communication na mobilization ya mamilioni ya wanyama hawa kwanza kujikusanya mahali pamoja na kusubiria kipenga, na huanza kutimka kwa mbia za ajabu na kutumia ruti moja!.

  Huwezi amini Utalii Tanzania, unatangazwa zaidi na Wakenya kuliko sisi Watanzania!. Idadi ya Wazungu wanaokuja kupanda mlima Kilimanjaro, wengi zaidi wanapitia Kenya na kuiacha pesa yote huko, na kutuletea sisi peanut ya viingilio na vitafunwa!. Wakenya wanautangaza Mlima uko kwao na sasa wanajenga Internation Airport chini ya mlima kule upande wao, ndio watumalize kabisa!. Hata utalii wa Zanzibar, unatangazwa zaidi na Wataliano kuliko Wanzanzibari wenyewe!.

  Mungu ametujalia Watanzania kila aina ya maliasili, ila pia ametujalia na upendo mkubwa kabisa wa mshumaa, tukimulikia wenzetu huku kwetu kunateketea!, kitafikia kipindi ile barafu kule kileleni itayeyuka na kuisha kabisa!, yale madini yatamalizika na kubakia mashimo!, mito itakauka, na bahari itakupwa!, by that time ikifika, mshumaa ndio utakuwa umefikia chini kabisa!.

  Mungu Ibariki Tanzania!.
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  lakini ilitakiwa tuangalie kupitia tv za kibongo,maana ni swala letu,iweje tunatumia tv za asia kuangalia jambo ambalo lipo kwetu tanzania?
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  PASCO
  nakubaliana na wewe kwa 100%
  tukisema tunaelezwa tunalalamika sana,lakini tangia wiki iliyopita nafuatilia swala hili,nawaona wakenya wakishirikiana na cctv 13 na cctv news ktk habari ya saa mbili usiku wamejitahidi kuliweka hili kila kona na sasa wapo live asia nzima inalishuhudia swala hili la uhamaji wa wanyama hawa,je ni viongozi wangapi wa tanzania wanalielewa hili?

  upo uwezekano hata hao wahusika wa wizara hawaelewi nini kinaendelea
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  WENZETU WANAPIGA PESA KITU LIVE SASA HIVI

  CCTV13?_???????
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Hizo ndizo priorities zetu!. Nilihudhuria Maonyesho fulani ya kukuza Utalii nchini US yaliyoandaliwa na AGOA, banda la Tanzania ilikuwa ni aibu ukilinganisha na Kenya!. Hebu fuatilia timu yetu ya Olympic jijini London ulinganishe na timu ya Kenya!.

  Ila tusilaumu, sisi concetration yetu ni kale ka mchezo cha kwenye 6x6!.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  jamani wanyama ndio wameanza kuondoka hivyo,nawaona hapa na pundamilia nao wameunga tela
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hahahaha
  pasco mbavu zangu bwana,sisi tunaleta utani sana ktk mambo ya msingi,ndio tatizo letu,hatupo makini sana na mambo ya kuitangaza nchi,kama ulivyosema tunapenda sana padiem na ile sehemu maalum
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii nchi yetu mtu unaweza ukabaki unamwaga tu machozi, ni kama yatima asiye na wazazi.
   
 12. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ni king'amuzi gani unatumia, nimeona kwenye CCTV news wame feature kwenye habari
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kikawaida ukitaka habari za ndani usiangalie cctv news,hawa huwa wapo juu sana

  tv ninayoyangalia mimi ni local tv ya kichina ndani ya mtandao inaitwa CCTV 13 ,NIMEWEKA LINK HAPO JUU,tumia link ya kwanza hapo juu
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  tusilaumu sana serikali yetu....leo naweza kuitetea kidogo sana.....mwaka huu wamejitahidi kuutangaza utalii.....tuna wageni wengi sana nchini kwa sasa....ki ufupi kumefurika....na mkumbuke Kenya kuna al shabab....kufa kufaana.....
  source: msiniulize....nyie jueni habari ndo hiyo.....
   
 15. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nishakupata asante sana.........................amazing is all i can say........natamani Watanzania tungeishi to our full potential
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  na wameshatangaza kuwa watashambulia ktk kipindi hiki cha mfungo
  inamaana hatuwawezi wa kenya bila tishio la alshababu tusingepata kitu.
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kwa hili tuwapongeze Al-Shabab?
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa huwa ndio tishio letu katika utalii......serikali yetu inatambua hilo lakini sijui kwa nini hailishughulikii.......na cha kushangaza hawana vivutio kama tulivyo navyo sisi.....huwa mara nyingi tunawabana pale wanapopatwa na matatizo......ndio inakuwa neema kwetu.....
   
 19. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hi hi hi....hatuwezi kusema hivyo Katavi (labda kimoyomoyo).......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ni siri
  ila kimoyo moyo mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh
  angarau vihotel vimejaa,na bila alshabab hata wale watalii walionusurika ktk ile meli tusingewaona
   
Loading...