Maajabu: Tunafundisha kwa lugha tusiyoijua

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,101
114,685
Moja kati ya ajabu ambalo huwa naliona katika mfumo wetu wa elimu ni kufundishwa kwa lugha tusiyoijua!Kingereza ni lugha ya kufundishia kuanzia kidato cha kwanza na kuendelea.

Hii lugha ni mtihani mkubwa kwa wasomi wetu ikiwemo mimi mwenyewe, natumia nguvu sana kuiongea, kidogo kuandika!Hivi hili suala limekosa muafaka jamani?Kwani China wamefanyaje?
 
Mpaka tutakapoithmini lugha yetu ndipo tutaona tija kwenye elimu yetu.....ikiwamo suala la ubunifu
 
Huwezi jifananisha na china ambao hata wakijifungia maisha yataendelea. Sisi lazima tujifunze tena tumechelewa.
 
Labda wananchi waelimishwe, kwa sasa kiongozi kama hachanganyi na kingereza katika speech yake haeleweki na anaonekana "Sio msomi" Mnalijua hilo.
 
Mi naona suluhisho ni kufanya lugha ya kiingereza kuwa ya kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu alafu kiswahili kiwe somo tu. Hata hivyo haitaleta athari yoyote maana kiswahili kimeshaenea vya kutosha alafu lugha kujifunza kwa maana ni rahisi sana
 
Dunia inaendeshwa kwa mfumo wa kibepari, huwezi kudhibiti mfumo huu kirahisi hata kidogo, hatuna namna mkuu, tunalazimishwa na ni lazima tukubali tu there is no way tutaepuka na tatizo hili
 
Back
Top Bottom