Maajabu Tanzania

Maajabu Tanzania

Hahaha sasa Barbara zikiwa safi sana jamaa si atadhani sisi mambo yetu safi sana atasitisha misaada kwa nini serikali isingeacha barabara chafu tu na ombaomba kibao pembeni ili mzee achangamshe mkono wa misaada mkiweka barabara fresh hata mkiomba msaada wa kujengea barabara atawauliza mbona njia ziko poa tu sijaona njia mbaya?
 
Hiv Kikwete akiendaga Marekani na yy huwa wanamtungia na nyimbo?
 
Nasikia ubungo pameng'aa mpaka basi, afu naskia posta ombaomba wote wamechukuliwa na kuwekwa mahali huko wanakamua vyuku na vyoda kwa kwenda foward...

huko lazima pawe segerea..
 
Akika Yesu au Mohammad sijui itakiwaje, nadhani wataoaka rangi hewa kabisa!
 
Nasikia kuwa atakwenda Morogoro pia kupitia Morogoro road ndio maana leo nikielekea Chalinze asubuhi nimekuta kuna disposable pipe linatandikwa kutoka mto Ruvu nilipouliza nikaambiwa kuwa kuna kazi ya kudeki morogoro road kutoka Kimara hadi morogoro! Kweli nothing impossible under ujio wa Obama
 
wewe ndo umeongea point mkuu, wengine wanapiga kelele tu, wagonjwa wana lala chini mahospitalini eti leo kaja mpumbafu mmoja nchi mpaka raisi mwenyewe ananyenyekea kama MUNGU kashuka kuja kutukomboa, niko natazama BBC NEWS, wao ndo wameongea sababu ya Obama kuja Tanzania ni competitions ya G8 kuweza ku exploit resources zilizopatikana especially Gesi ya mtwara, Naumia sana aiseeh ...

Baba wa Taifa kabla hajafa alisema,"Wajanja wameliondoa Azimio la Arusha na wachache wenye akili tukagundua sasa ndiyo basi tena mambo yameisha haribika!" Maono ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere sasa hivi ndiyo yanatimia! Maskini Watanzania sijui tulilishwa nini manake hatusikii,hatuoni wala kujua tunapelekwa wapi na viongozi wetu wasiyo na uzalendo! Bado tupo tupo tu!
 
Kila mara huwa nagombana na viongozi wangu kwa tabia yao ya kuwapa mashuka mapya wagonjwa waliolazwa wodini pale tunapotarajia ugeni, wakati mwingine mambo haya hufanyika hata pale ambapo dawa na vifaa tiba hamna. Yaani huwa najiona mpumbafu pale mgonjwa anaponiuliza eti 'hata panado hamna?'

Leo nimejifunza kitu, kumbe upumbafu huu unaanzia huko juu! Nadhani Ikulu!

hilineno 'pumbafu' mpaka limg'oe mtu meno na kumtindua kucha ndo litakoma !
 
Nilileta thread hapa jamvin ya kaz ya kudeki barabara watu wakaniponda na iliondolewa kwa haraka sn leo mmeyaona!
 
Naomba kujuzwa hivi wanatumia gari maalumu kudeki au wanatumia mafagio na maji? Duh that is our country!


Hilo la kupiga deki namimi nimeliona, inasikitisha sana.
 
Nıpo ubungo mataa: Morogoro road na Samnujoma road zınapıgwa dekı: Kwelı Obama Nomaaaaa.....! Tutashuhudıa mengı

Thank you the SWEEPER for sweeping our roads!!
 
Last edited by a moderator:
Mwongo huyu. Mi nipo ubungo hapa. mbona amna mtu anapiga deki barabara. labda wafagizi ndo nilikuta wapo bize kile kinjia cha Ubungo maziwa wanafagia. Deki? aaaah....jamani punguzeni uongo. Barabara yenyewe ya kupiga deki iko wapi...Strabarg wametindua kila mahali.

992905_436826973082739_1634559402_n.jpg


Nini kinafanyika hapo?
 
992905_436826973082739_1634559402_n.jpg


Nini kinafanyika hapo?

mwenzangu!? nilikuwa sijaona! ....lakini hii picha pia sina hakika kama ni ubungo. deki za ubungo kumbe zilipigwa asubuhi na mapema. kuna mtu alikuwa anashuhudia pale kwenye baa usiku; yeye aliwahi kupanda treni pale ubungo maziwa ndo akawa anasimulia pale kwenye baa nini aliona. ni sie wachelewaji kuamka ndo hatukuona hizo deki. Barabara zinapigwa deki? sijapata kuona mie. Bush na Klintoni hawakumpigia deki barabara.... huyu Obama kapendelewa mno jamani! kha.... au ndo yaleyale mtoto wa kwanza karudi kutoka safari ya mbali baba na mama wanahangaika kumfurahisha? mmh. Nakosa hata la kusema mie....

Nimpongeze Kikwete japo kwa hili. Safari hii kafanya jambo kubwa la kihistoria. Hii picha itatumika miaka mingi sana nina hakika. Kotekote Tanzania na Marekani. Pengine hata Kenya.
 
Tatizo dar es salaam mmeshazoea uchafu barabarani hali mnayoisababisha wenyewe mbona mwanza zinadekiwa daily bila ugeni wowote
 
Back
Top Bottom