Kamende
JF-Expert Member
- Mar 1, 2008
- 416
- 45
Wakuu ninaleta jukwaani habari ambayo kama hujaisikia kutoka eneo la tukio ni lazima uwe na mashaka na uwezekano wa tukio husika.
Leo kulikuwepo mkutano wa hadhara huko jimboni Busanda ambako Mhe. Bukwimba mbunge wa jimbo hilo aliandaliwa kuhutubia wananchi wa kata ya Katoro jimboni mwake.
Mkutano ulianza saa 10.20 jioni kwa Mhe. Diwani wa Viti Maalum Maimuna Minasi kutoa hotuba ya utangulizi na hatimaye kumkaribisha Mhe. Lolesia Bukwimba yapata saa 11.00 kamili.
Wakati Bukwimba akihutubia lilionekana wingu dogo likitanda angani na hatimaye likakusanyika na kuwa kubwa. Mvua ilianza kidogo kidogo na hatimaye radi kubwa ilianguka juu ya mti kulikokuwa kumetundikwa bendera ya CHADEMA. Radi ile iliangusha bendera ya CHADEMA na ilipofika chini iliwaka moto ikateketea.
Wananchi kuona hivyo walianza kuzomea kwa sauti kubwa na kusababisha mkutano kuvunjika.
Haijaeleweka rasmi nini hasa kimesababisha radi hiyo?
Bado hatujajua kwa nini radi ipige bendera peke yake?
Na ni kwa nini iwake moto?