Maafisa uhamiaji wa Julius Nyerere Airport hawana professionalism

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,144
15,145
Aisee leo nimetoka zangu ng'ambo tukafika kwenye Passport check nimekaa kwenye foleni ya Tanzania Citizens kama dak 20 jamaa wa uhamiaji alikua anamhudumia mdada alokua mbele yangu halafu hamalizi.

Kumbe muda wote jamaa linang'ang'aniza dem alipe namba linamchelewesha makusudi.

Mwishowe yule dada kama akakasirika akampa namba kama kwa kushout kidogo. Basi akamruhusu huyo dada kupita.

Sasa vile vibanda vyao ukishagongewa stamp unapita kwa nyuma kuelekea luggage claim.

Cha ajabu yule jamaa wa uhamiaji akainuka kwenye kiti halafu akageuka akawa anamkadiria yule dada kwa nyuma aone mzigo 😂😂😂. Na hapo kumbuka kuna bonge la foleni tunasubiri tuhudumiwe.

Tulivofika luggage claim yule mdada akawa amemind anamhadithia mwenzake, ajabu na mwenzake akasema nae aliombwa namba na jamaa alomhudumia ila akampotezea.

Kile kitendo kilinikimbusha kisa kimoja ambacho nilikipuuziaga ila hapa ntakielezea maana nadhani hawa maofisa wanashindana kutongoza pale.

Mwaka jana kazini tulikua na regional retreat ilifanyika Tanzania kwa hiyo watu toka mataifa tofauti walikuja.

Basi jioni tupo dinner kuna wadada toka nchi mbalimbali wakawa wanahadithia kila mmoja alivopata kashkash ya jamaa wa uhamiaji pale airport.

Ajabu kila mmoja akawa anaelezea jinsi wahudumu walivyokua wanawatongoza na kuomba namba tena kwa kuwafrustrate.

Na kweli jioni ile kuna jamaa wa uhamiaji walikuja mida tofauti kwenye hotel tuliyokuwepo wakawa wapo parking area wanawatafuta wale foreigners eti wawape kampani.

Kuna mdada mmoja ambae alitoa namba akawa anatuonesha texts za jamaa kuwa yupo parking area na jinsi anavopigiwa WhatsApp calls.

Basi wale wadada wakaishia kutuponda pale ikaisha.
Anyway inaonekana ni kitu kidogo ila nahisi hii hali isipodhibitwa inatia doa taifa maana ni kama wanashindana kutongoza na kufanya watu wasihudumiwe kwa wakati.

Ningewawekea hata namba ya afande wa uhamiaji alotuweka kisa anatongoza, bahati yake nzuri alikua kavaa sweta so namba haionekani
 
Hapa umetupiga kamba na sidhani kama umewahi hata kusafiri nje ya nchi

Naomba nikuelimishe kidogo, ukipita airport lazima utoe taarifa zako binafsi ikiwemo mawasiliano ya ulipotoka na unapokwenda. Lazima uwape maafisa wa mpakani mawasiliano yako kwa maana ya address na kwa bongo lazima utaje namba ya simu waitie kwenye mfumo.

Hasa hao jamaa watalazimishaje kupewa namba za simu na mademu wakati hizo namba wanazo kwenye hayo mamifumo wanayotumia?

Kwa hii story yako hapa najua kabisa umetupiga kamba au ulitaka kutueleza jambo jingine ukachomeka mapenzi ndani............
 
ulichoandika hakihusiani na maelezo yako, kipi cha ajabu kutongoza, au kuomba namba? mbona jambo la kawaida au ulitaka utongozwe wewe?
 
Aisee leo nimetoka zangu ng'ambo tukafika kwenye Passport check nimekaa kwenye foleni ya Tanzania Citizens kama dak 20 jamaa wa uhamiaji alikua anamhudumia mdada alokua mbele yangu halafu hamalizi.

Kumbe muda wote jamaa linang'ang'aniza dem alipe namba linamchelewesha makusudi.

Mwishowe yule dada kama akakasirika akampa namba kama kwa kushout kidogo. Basi akamruhusu huyo dada kupita.

Sasa vile vibanda vyao ukishagongewa stamp unapita kwa nyuma kuelekea luggage claim.

Cha ajabu yule jamaa wa uhamiaji akainuka kwenye kiti halafu akageuka akawa anamkadiria yule dada kwa nyuma aone mzigo . Na hapo kumbuka kuna bonge la foleni tunasubiri tuhudumiwe.

Tulivofika luggage claim yule mdada akawa amemind anamhadithia mwenzake, ajabu na mwenzake akasema nae aliombwa namba na jamaa alomhudumia ila akampotezea.

Kile kitendo kilinikimbusha kisa kimoja ambacho nilikipuuziaga ila hapa ntakielezea maana nadhani hawa maofisa wanashindana kutongoza pale.

Mwaka jana kazini tulikua na regional retreat ilifanyika Tanzania kwa hiyo watu toka mataifa tofauti walikuja.

Basi jioni tupo dinner kuna wadada toka nchi mbalimbali wakawa wanahadithia kila mmoja alivopata kashkash ya jamaa wa uhamiaji pale airport.

Ajabu kila mmoja akawa anaelezea jinsi wahudumu walivyokua wanawatongoza na kuomba namba tena kwa kuwafrustrate.

Na kweli jioni ile kuna jamaa wa uhamiaji walikuja mida tofauti kwenye hotel tuliyokuwepo wakawa wapo parking area wanawatafuta wale foreigners eti wawape kampani.

Kuna mdada mmoja ambae alitoa namba akawa anatuonesha texts za jamaa kuwa yupo parking area na jinsi anavopigiwa WhatsApp calls.

Basi wale wadada wakaishia kutuponda pale ikaisha.
Anyway inaonekana ni kitu kidogo ila nahisi hii hali isipodhibitwa inatia doa taifa maana ni kama wanashindana kutongoza na kufanya watu wasihudumiwe kwa wakati.

Ningewawekea hata namba ya afande wa uhamiaji alotuweka kisa anatongoza, bahati yake nzuri alikua kavaa sweta so namba haionekani
tatizo linalowatesa wanaume wa kitz ni upwiru.
 
Huu ni upumbavu ambao utaharibu taswira ya Nchi vibaya kuliko harufu mbaya ya samaki ozo
 
Hapa umetupiga kamba na sidhani kama umewahi hata kusafiri nje ya nchi

Naomba nikuelimishe kidogo, ukipita airport lazima utoe taarifa zako binafsi ikiwemo mawasiliano ya ulipotoka na unapokwenda. Lazima uwape maafisa wa mpakani mawasiliano yako kwa maana ya address na kwa bongo lazima utaje namba ya simu waitie kwenye mfumo.

Hasa hao jamaa watalazimishaje kupewa namba za simu na mademu wakati hizo namba wanazo kwenye hayo mamifumo wanayotumia?

Kwa hii story yako hapa najua kabisa umetupiga kamba au ulitaka kutueleza jambo jingine ukachomeka mapenzi ndani............
Soma vizuri Kwa ufahamu
 
Ndo tabia za Hamas hizo.

Hovyo kabisa haya magaidi.

mwandende
Papa amekufikia mkuu unakaribishwa
IMG_20231109_231209.jpg
 
Back
Top Bottom