Maafisa Ugavi wa Wizara ya Elimu wafikishwa Mahakamani kwa Rushwa ya Tsh. Milioni 40

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 22/2023-Jamhuri dhidi ya 1.YAHYA AMOUR OMAR, 2. AUDIFASY ANGELUS MYONGA ambao ni Maafisa Ugavi katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na 3. SHANA WILLIAM MUNISI -Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kampuni ya S. Scientific Centre Limited, limefunguliwa leo tarehe 18/10/2023 mbele ya Mhe. ANNETH NYENYEMA (RM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.

Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa matano yakiwemo; Ubadhirifu na Ufujaji, Matumizi mabaya ya Mamlaka, Kughushi nyaraka, Kuwasilisha nyaraka za uongo na Kuisababishia Serikali hasara kiasi cha sh. 40,362,250/=

Washtakiwa wote wamekana makosa ambapo mshtakiwa Yahya Amour na Audifasy Myonga wamepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi tarehe 1/11/2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.

TAKUKURU
 
Takukuru hizi ndio kesi zenu zile za CAG mnazichungulia tuu...
Mi Takukuru niliwadharau na kuwashusha thamani siku mkuu wao akiwa na makombati ya jeshi alipotamka vongozi wa ccm waliokamatwa na rushwa watashughulikiwa na chama Chao wao Takukuru hawana cha kufanya wala kuingilia
 
Mi tangu Takukuru niliwadharau na kuwashusha thamani siku mkuu wao akiwa na makombati ya jeshi alipotamka vongozi wa ccm waliokamatwa na rushwa watashughulikiwa na chama Chao wao Takukuru hawana cha kufanya wala kuingilia
Daah hao mimi nawaona kama wakina Baba levo tuu hawana meno zaidi ya kujipendekeza ndio wafanye kazi...
 
Back
Top Bottom