Maafisa kazi na maafisa uhamiaji ndio tatizo katika ajira

Kizoku

Senior Member
Apr 30, 2014
186
66
Huwa nakosa majibu ninaposikia viongozi wanapolalamika na kusema hatua za kisheria zitachukulia kwa makampuni yote yenye kuajiri wageni kwenye kazi zinazoweza kufanywa na wazawa na kuwashughulikia waajiri wenye kuwatumia wageni wasiokuwa na vibali vya kazi.

Nadhani ingekuwa busara zaidi kama serikali ingetangaza kuwafuta kazi maafisa kazi na maafisa uhamiaji wote ambao maeneo yao ya ukaguzi yatabainika kiwepo kwa wageni wasiokuwa na vibali vya kazi au kufanyakazi ambazo kisheria au kitaratibu zinatakiwa kufanywa na wazawa.

Kwani hawa watu kila mwezi hufika maeneo hayo lakini kwao hayo maeneo ni sehemu ya mradi.

Watakaponza kushughulikiwa hawatoendelea kuwatumia waajiri wa aina hii kama sehemu ya kuongezea mafao yao.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom