Ziara ya Rais Hanang ilitakiwa kuwa very brief, kuangalia madhara yaliyotokea, atoe pole, basi. Nina Imani Rais alishapewa ripoti nzima ya hali ilivyo Hanang na hivyo alikuwa walau na picha ya yaliyojiri, leo ilikuwa kwenda kuwaona waathirika na aongeze nguvu kwa waathirika angalau kuwa sehemu nzuri wakati wanasubiri utaratibu mwingine.
Kama ni kutoa ripoti/salamu nyingine baada ya kuwatembelea wahanga angeweza kufanya hivyo ofisini, wengine tukaangalia mubashara bila kuongeza gharama nyingine ambazo hazina msingi.
Sasa watu wanaandaa mkutano mzima utafikiri anaenda kwenye mikutano yake ya kawaida ya hadhara, nguo za CCM zimetaradadi, mnaenda mpaka na wasanii? Mnazidi kutumia rasilimali kwenye mambo ambayo hayana maana.
Wasanii wenyewe wanaimba upuuzi, eti Rais umeacha vinono Dubai umekuja kutuona hanang! Kwani ni hisani hiyo? Si ni majukumu yake kama Rais kuwa mstari wa mbele kuwajali wananchi anaowatumikia?
Haya mmeamua kufanya yote hayo basi nendeni kwenye point bado mnaanza uchawa! Hao waathirika hawahitaji yote hayo, wanahitaji misaada ya hali mali, wanahitaji kuwa salama, wahitaji faraja, sio uchawa na mambo ambayo hayana maana.
Kwenu nyuki wa mama.