Maadui wa CHADEMA hawa hapa

Maadui wa CHADEMA hawa hapa

Cherenganya

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2018
Posts
2,309
Reaction score
1,787
Salam wanagenzi

Siasa ni mchezo wa HOVYO unao chezwa na watu smart upstairs, SIASA inakupatia mambo matatu, marafiki, WANAFIKI na maadui unaowajua.

CHADEMA, wana maadui wengi sana na kutokana na kutokuwa na watu upstairs (NYUMBU) wanawapa nafasi kubwa maadui zao kuanzisha mashambulizi ya Mara kwa Mara kabla hawajajipanga wanashambuliwa toka pande nyingine.

NITAFAFANUA PARAGRAPH HIYO HAPO JUU.

1. CCM
2. DEMOKRASIA YA NDANI
3. UMBUMBUMBU JUU YA SHERIA

Walakini yote hayo nasikitika kusema yanakuja kutokana na udhaifu mkubwa ndani ya CHADEMA.

Udhaifu mamba moja ni chama kutokua na vision na mission na kujulikana ni cha mrengo gani?. Mabebari au Wajamaa, au mchanganyiko wa ujamaa na ubepari.

Pili, inayotukia kwa sababu ya para hiyo ya juu, chama kujikuta kikicheza ngoma isiyokua yake, hivyo kujikuta ikidumbukia kwenye kushadadia matukio ambayo yametengenezwa na CCM.

Hapa ikumbukwe kwamba CCM kama chama cha siasa hakina budi kujiimarisha, hivyo haina haja ya kuwalalamikia kwakua hata CHADEMA wangekua kwenye nafasi hiyo wangelitenda kama CCM

Tatu na mwisho chama kinawatu wasomi lakini wanaoendeshwa kwa mihemko badala ya hoja na facts. Kuna makosa madogo madogo sana ya kiufundi, wanayafanya ambayo huharibu kabisa taswira ya chama.

MFANO HIVI PUNDE
Hawakujiandaa kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hawakuwaandaa pia wagombea, CCM ilitawanya wanasheria 1250 nchi nzima kuwaandaa wagombea wao, wakawatega kwenye kimtego cha kisheria wakanasa.

Pia wameingia kwenye mtego ambao umewadondosha kwa asilimia kubwa. Kitendo cha Freeman Aikael Mbowe kuchukua form ya uenyekiti ndio CCM walichokua wakikisubiri, Jana Waziri Mkuu mstaafu Sumaye Tulway kajiondoa CHADEMA halikua tatizo sana bali alichokisema wakati anaondoka.

Maneno aliyoyasema yamekua yakijirudia rudia, kwa kila anayeondoka ndani ya chama na hata walioamua kubaki ndani ya chama rejea ya Komu na Said Kubenea.

CHADEMA aidha haina watu mahiri wenye kuijua siasa au watu mahiri wapo ila hawapewi nafasi kwa sababu hawako kwenye kambi kuu.

AHSANTE
 
Duh...!, Mkuu Cherenganya, you are wrong, hii hoja ya adui mkubwa wa Chadema ni CCM, this is the biggest mistake of Chadema, adui mkubwa wa Chadema sio CCM, adui mkubwa wa Chadema ni huyu niliyemtaja hapa
P
 
Mkuu waachie CHADEMA yao hayakuhusu zaidi ya wivu,maana utabiri wa kuizika hautimiliki zaidi ya wao kuvuka vikwazo.
 
Adui mkubwa wa Chadema ni mapandikizi na mamluki wanaotumwa na CCM

CHADEMA kinatakiwa safisha safisha ya brashi la chuma ili uchaguzi mkuu ujao twende tukiwa kamilgado mamiloni ya wananchi wanasubiri kutupa kura zao.
 
Kuna wakati nachanganyikiwa kama vile nimechanganya K-vant na Chang'aa!

Hivi inakuwaje maadui wa Chadema kila siku wakisemwa anatajwa Mbowe ndio namba one? Na wanaomtaja kwa uchambuzi na tahariri zilizo na Tashwishwi (in Kabudi voice) sio wengine bali ni "marafiki wakubwa" wa Chadema yaani CCM?

Ni kama vile uchunguzi wa adui wa Chadema na njia kupambana nae umefanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuletwa kwa wanachama wake wa upiganie kwa nguvu zote.

Hivi wenye Chama yaani Wanachadema hawaoni huyo adui mkubwa wa Chadema yaani Mbowe hadi waje wafundishwe na "marafiki zao wakubwa" CCM?

Naomba ambaye hajanywa chang'aa anisaidie kuelewa ni kwa nini hawa jamaa zetu Chadema hawataki kupokea ushauri musharabu toka kwa "rafiki zao" CCM?
 
Sisi tuliopo vijijini tunaona facts, kama unafikiri CCM wako vizuri unajidanganya.
Ushindi wa CCM serikali za mitaa ni magumashi hakuna wapinzani walipita bila kupingwa.
Walitumia ubabe sio ushindani, CCM imeisha kufa ni kubebwa na dola wakurugenzi na watendaji!!
Wapinzani wapo ni vichwa usipime, uchaguzi huru na wa haki CCM wanabwagwa asubuhi.
Hoja zako ni hewa hazina mashiko!!
 
Duh...!, Mkuu Cherenganya, you are wrong, hii hoja ya adui mkubwa wa Chadema ni CCM, this is the biggest mistake of Chadema, adui mkubwa wa Chadema sio CCM, adui mkubwa wa Chadema ni huyu niliyemtaja hapa
P
Nimeipenda hii

kulaumu tuu kuhusu CCM, bali sasa wajikite kueleza where CCM does wrong, lakini wao wakiingia, watafanya nini tofauti na CCM, na kitabadilisha nini, ili wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu, wapate sababu za msingi za kutoichagua CCM na kuwachagua wapinzani.
 
Salam wanagenzi

Siasa ni mchezo wa HOVYO unao chezwa na watu smart upstairs, SIASA inakupatia mambo matatu, marafiki, WANAFIKI na maadui unaowajua.

CHADEMA, wana maadui wengi sana na kutokana na kutokuwa na watu upstairs (NYUMBU) wanawapa nafasi kubwa maadui zao kuanzisha mashambulizi ya Mara kwa Mara kabla hawajajipanga wanashambuliwa toka pande nyingine.

NITAFAFANUA PARAGRAPH HIYO HAPO JUU.

1. CCM
2. DEMOKRASIA YA NDANI
3. UMBUMBUMBU JUU YA SHERIA

Walakini yote hayo nasikitika kusema yanakuja kutokana na udhaifu mkubwa ndani ya CHADEMA.

Udhaifu mamba moja ni chama kutokua na vision na mission na kujulikana ni cha mrengo gani?. Mabebari au Wajamaa, au mchanganyiko wa ujamaa na ubepari.

Pili, inayotukia kwa sababu ya para hiyo ya juu, chama kujikuta kikicheza ngoma isiyokua yake, hivyo kujikuta ikidumbukia kwenye kushadadia matukio ambayo yametengenezwa na CCM.

Hapa ikumbukwe kwamba CCM kama chama cha siasa hakina budi kujiimarisha, hivyo haina haja ya kuwalalamikia kwakua hata CHADEMA wangekua kwenye nafasi hiyo wangelitenda kama CCM

Tatu na mwisho chama kinawatu wasomi lakini wanaoendeshwa kwa mihemko badala ya hoja na facts. Kuna makosa madogo madogo sana ya kiufundi, wanayafanya ambayo huharibu kabisa taswira ya chama.

MFANO HIVI PUNDE
Hawakujiandaa kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hawakuwaandaa pia wagombea, CCM ilitawanya wanasheria 1250 nchi nzima kuwaandaa wagombea wao, wakawatega kwenye kimtego cha kisheria wakanasa.

Pia wameingia kwenye mtego ambao umewadondosha kwa asilimia kubwa. Kitendo cha Freeman Aikael Mbowe kuchukua form ya uenyekiti ndio CCM walichokua wakikisubiri, Jana Waziri Mkuu mstaafu Sumaye Tulway kajiondoa CHADEMA halikua tatizo sana bali alichokisema wakati anaondoka.

Maneno aliyoyasema yamekua yakijirudia rudia, kwa kila anayeondoka ndani ya chama na hata walioamua kubaki ndani ya chama rejea ya Komu na Said Kubenea.

CHADEMA aidha haina watu mahiri wenye kuijua siasa au watu mahiri wapo ila hawapewi nafasi kwa sababu hawako kwenye kambi kuu.

AHSANTE
Mbowe siyo tatizo tatizo ccm hawataki demokrasi ya ushindani, labda ushauri itumike njia nyingine nje ya demokrasia

Mbowe bado ana nafasi nzuri ya kukijennga chama,

Aliyekuwa ameandaliwa kumrithi yuko uhamishoni,

Waliotaka kugombea uenyekiti wamesema walikuwa hawana nia ya kuitoa ccm
na kushika dola/ madaraka, ila tu kutest kama demokrasis iko chamani.

Muwe mnajihoji halmashauri kuu ya vichwani kwenu kabla ya kuandika upuuzi
 
Adui mkubwa wa Chadema ni mapandikizi na mamluki wanaotumwa na CCM

CHADEMA kinatakiwa safisha safisha ya brashi la chuma ili uchaguzi mkuu ujao twende tukiwa kamilgado mamiloni ya wananchi wanasubiri kutupa kura
Uzuri wenu ni kumbukumbu zenu za muda mfupi.
Ona saa hizi unasubiri kwa hamu kubwa uchaguzi. Ukipita tu unakumbuka tena kilio cha tume huru.
 
Nimeipenda hii

kulaumu tuu kuhusu CCM, bali sasa wajikite kueleza where CCM does wrong, lakini wao wakiingia, watafanya nini tofauti na CCM, na kitabadilisha nini, ili wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu, wapate sababu za msingi za kutoichagua CCM na kuwachagua wapinzani.

Mbona sababu wanazo tayari na hawaichagui CCM? Ndio maana wanatumia mbinu mbovu
 
Uzuri wenu ni kumbukumbu zenu za muda mfupi.
Ona saa hizi unasubiri kwa hamu kubwa uchaguzi. Ukipita tu unakumbuka tena kilio cha tume huru.
CCM waliyoyafanya ktk uchaguzi wa serikali za mitaa ni jambo zuri kwani wamejisababishia jumuia za kimataifa kuuangalia uchaguzi mkuu kwa ukaribu zaidi waangalizi wa kimataifa watakuwa wengi sana na wakisema ccm wameiba kura vikwazo vinafuata.
 
1575526038194.jpeg
 
Nimejaribu kuunganisha kichwa cha habari na yaliyomo ndani...nimeshindwa kuona ulinganifu...nimeona lawama, kejeli na kujifanya unajua maadui wa CDM kumbe wala huna hata Idea.
nimeshajua kabila lako
 
Nimeipenda hii

kulaumu tuu kuhusu CCM, bali sasa wajikite kueleza where CCM does wrong, lakini wao wakiingia, watafanya nini tofauti na CCM, na kitabadilisha nini, ili wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu, wapate sababu za msingi za kutoichagua CCM na kuwachagua wapinzani.
Are you sure bongo kuna uchaguzi kama inavyojinasibu??
 
Back
Top Bottom