Maadui wa CHADEMA hawa hapa

Maadui wa CHADEMA hawa hapa

Kuna wakati nachanganyikiwa kama vile nimechanganya K-vant na Chang'aa!

Hivi inakuwaje maadui wa Chadema kila siku wakisemwa anatajwa Mbowe ndio namba one? Na wanaomtaja kwa uchambuzi na tahariri zilizo na Tashwishwi (in Kabudi voice) sio wengine bali ni "marafiki wakubwa" wa Chadema yaani CCM?

Ni kama vile uchunguzi wa adui wa Chadema na njia kupambana nae umefanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuletwa kwa wanachama wake wa upiganie kwa nguvu zote.

Hivi wenye Chama yaani Wanachadema hawaoni huyo adui mkubwa wa Chadema yaani Mbowe hadi waje wafundishwe na "marafiki zao wakubwa" CCM?

Naomba ambaye hajanywa chang'aa anisaidie kuelewa ni kwa nini hawa jamaa zetu Chadema hawataki kupokea ushauri musharabu toka kwa "rafiki zao" CCM?
Kaka Kuna watu wanashauri na hawana mapenzi na chama chochote, hawa husimama Kama wanataaluma au wazoefu. Kamwe CCM hawezi kutoa ushauri kwa CHADEMA kwakua wote wanalengo moja wote wanahitaji aidha kuendelea kukaa kwenye dola au kuingia na kushika dola.
 
Mbowe siyo tatizo tatizo ccm hawataki demokrasi ya ushindani, labda ushauri itumike njia nyingine nje ya demokrasia

Mbowe bado ana nafasi nzuri ya kukijennga chama,

Aliyekuwa ameandaliwa kumrithi yuko uhamishoni,

Waliotaka kugombea uenyekiti wamesema walikuwa hawana nia ya kuitoa ccm
na kushika dola/ madaraka, ila tu kutest kama demokrasis iko chamani.

Muwe mnajihoji halmashauri kuu ya vichwani kwenu kabla ya kuandika upuuzi
Haki haiombwi kaka inadaiwa.
 
nimeshajua kabila lako
Kaka hawa kina Mangi wanasahau kwamba Taifa hili lina makabila zaidi ya 120 hawajui kwamba japo wanazo chembechembe za Kiingereza kupitia (CHIEF MALIARRE) haiwapi tiketi ya kuona wengine Ni maboya tu.
 
Ukishajiuluza na kujijibu kwanini sio Cheyo,Mrema,Lipumba au Mbatia basi utapata jibu chuki hii ni kwaajili ya kitu gani?Kwanini hawaongelei yule kiongozi mkuu katika chama ambae hachaguliwi kabisa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]utagundua kuwa watu wana interest kubwa sana na chokochoko katika chama hiki na sababu kubwa ni kwamba wanawaogopa kwakweli
Hapo sio kwamba wanaogopeka Mkuu, CHADEMA inajadiliwa l, laumiwa, kosolewa kwa sababu moja tu KWAKUA NDIO CHAMA KIKUU CHA UPINZANI,l. Labda ulikua na umri mdogo, wakati Mzee wa Kiraracha akiwa katika form tulikua tukimjadili yeye kuliko Marehemu Mtikila, Shabani Mloo na baadae Prof Lipumba. Prof. Lipumba na CUF yake walipokua kwenye form alikua hajadiliwi tena Mrema.
 
Unailaumu vipi cdm haikujiandaa kisiasa wakati ww mwenyewe unajua cdm wamezuiwa kufanya siasa mwaka wa nne sasa
Kaka kama chama cha siasa KILITAKIWA KUJIONGEZA, ULISHAWAZA IWAPO WANGETUMIA MIKUTANO YA NDANI KUWAELIMISHA NA KUWAANDAA WAGOMBEA?

Wazee wetu walioleta Uhuru kama wangekua na attitude kama za viongozi wa bado tungekua kwenye upe utumwa wa kufungwa minyororo.
 
Mkuu Chakaza siku ukiwa umepumzika ndani kwako nyakati za usiku na ukasikia huko nje vibaka wanapita na horn speaker wakisema jamani tunawatangazia leo hakikisheni mmeingiza kila kitu ndani maana tutapita kuiba wewe relax uje hata kidekio hakijaachwa nje.

CCM imekamatwa vilivyo na Mbowe mayowe unayosikia ujue vibaka wameshidwa kupenya. MwanaCCM yeyote hawezi kuionea hurumaCDM katika maamuzi yake ya Kijinga !!!
Gwallo, Kama ambavyo mwana CHADEMA hawezi kumtakia mema mwana CCM. Usipepese macho palipo na ukweli.
 
Chadema mnaitakia nini nyie, Chadema, Chadema hebu endeleeni na li chama lenu la kijani.
 
Mbona sababu wanazo tayari na hawaichagui CCM? Ndio maana wanatumia mbinu mbovu
Mkuu,chama kiko madarakani miaka 50++kinabaka demokrasia ya vyama vya 1992!!eti walitawanya wanasheria nchi nzima kisirisiri uwoga wote wa nini??kwa vyama ambavyo kwa ujumla wao havina majority bungeni,uwoga na kutojiamini kwa ccm ndio kiini cha kuharibu chaguzi.
 
Mkuu,chama kiko madarakani miaka 50++kinabaka demokrasia ya vyama vya 1992!!eti walitawanya wanasheria nchi nzima kisirisiri uwoga wote wa nini??kwa vyama ambavyo kwa ujumla wao havina majority bungeni,uwoga na kutojiamini kwa ccm ndio kiini cha kuharibu chaguzi.
Nadhani tuendelee kuibaka democrasia,naona hata cdm wameibaka inaelekea raga sana
 
Salam wanagenzi

Siasa ni mchezo wa HOVYO unao chezwa na watu smart upstairs, SIASA inakupatia mambo matatu, marafiki, WANAFIKI na maadui unaowajua.

CHADEMA, wana maadui wengi sana na kutokana na kutokuwa na watu upstairs (NYUMBU) wanawapa nafasi kubwa maadui zao kuanzisha mashambulizi ya Mara kwa Mara kabla hawajajipanga wanashambuliwa toka pande nyingine.

NITAFAFANUA PARAGRAPH HIYO HAPO JUU.

1. CCM
2. DEMOKRASIA YA NDANI
3. UMBUMBUMBU JUU YA SHERIA

Walakini yote hayo nasikitika kusema yanakuja kutokana na udhaifu mkubwa ndani ya CHADEMA.

Udhaifu mamba moja ni chama kutokua na vision na mission na kujulikana ni cha mrengo gani?. Mabebari au Wajamaa, au mchanganyiko wa ujamaa na ubepari.

Pili, inayotukia kwa sababu ya para hiyo ya juu, chama kujikuta kikicheza ngoma isiyokua yake, hivyo kujikuta ikidumbukia kwenye kushadadia matukio ambayo yametengenezwa na CCM.

Hapa ikumbukwe kwamba CCM kama chama cha siasa hakina budi kujiimarisha, hivyo haina haja ya kuwalalamikia kwakua hata CHADEMA wangekua kwenye nafasi hiyo wangelitenda kama CCM

Tatu na mwisho chama kinawatu wasomi lakini wanaoendeshwa kwa mihemko badala ya hoja na facts. Kuna makosa madogo madogo sana ya kiufundi, wanayafanya ambayo huharibu kabisa taswira ya chama.

MFANO HIVI PUNDE
Hawakujiandaa kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hawakuwaandaa pia wagombea, CCM ilitawanya wanasheria 1250 nchi nzima kuwaandaa wagombea wao, wakawatega kwenye kimtego cha kisheria wakanasa.

Pia wameingia kwenye mtego ambao umewadondosha kwa asilimia kubwa. Kitendo cha Freeman Aikael Mbowe kuchukua form ya uenyekiti ndio CCM walichokua wakikisubiri, Jana Waziri Mkuu mstaafu Sumaye Tulway kajiondoa CHADEMA halikua tatizo sana bali alichokisema wakati anaondoka.

Maneno aliyoyasema yamekua yakijirudia rudia, kwa kila anayeondoka ndani ya chama na hata walioamua kubaki ndani ya chama rejea ya Komu na Said Kubenea.

CHADEMA aidha haina watu mahiri wenye kuijua siasa au watu mahiri wapo ila hawapewi nafasi kwa sababu hawako kwenye kambi kuu.

AHSANTE
Mnapiga Kelele mnapoteza muda na radilimali bure tu propaganda dhaifu. Hakuna atakaye wasikiliza,
 
Back
Top Bottom