Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
Leo ni Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya katika viwanja vya Ruanda Nzomve.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Hassan Suluhu.
Miongoni mwa wageni walio fika katika viwanja hivyo ni waziri mkuu Mh. Majaliwa kassim Majaliwa, Naibu spika Dkt Tulia Ackson, mawaziri na manaibu mawaziri, Balozi wa Marekani nchini na wageni wengine.
Updates
Naibu spika Dkt Tulia Ackson ameingia katika uwanja wa Maadhimisho.
Waziri wa Afya Dorothy Gwajima ameingia pia uwanjani hapo.
Mkuu wa mkoa wa mbeya anaongoza msafara kwa ajira ya kumpokea mgeni Rasmi.
Waziri mkuu Majaliwa ameingia uwanjani akepikelewa na jenister muhagama wakiambatana na Naibu spika Dkt Tulia Ackson.
Burudani:
Kikundu cha Ngoma za Asili kikiambatana na wana sarakasi kinaingia kutumbuiza.
Pia Msanii wa nyimbo za Asili almaarufu kana Awilo anatumbuisha.
Msanii wa Bongo fleva nchini ambae pia ni mwenyeji wa Mbeya Rayvanny ameingia kutumbuiza katika viwanja vya eneo la tukio akisindikizwa na mchungaji Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji).