Maadhimisho ya miaka 55 kufanyika katika uwanja wa Uhuru

RUCCI

RUCCI

JF-Expert Member
1,701
2,000
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatafanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Tarehe 9 Desemba, 2016.

Mgeni Rasmi katika sherehe hizi atakuwa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Kauli Mbiu: "Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu"


 
Mshana Jr

Mshana Jr

Platinum Member
138,079
2,000
Kubana matumizi kumeisha! Maana hata michezo ya wanajeshi imeruhusiwa
Bana matumizi Zilikuwa nguvu za Soda. Mwendo mdundo.
Chama Cha Matumizi (CCM)
Kuokoa Pesa hakupo tena?
Lizaboni hebu njoo utuambie kama kubana matumizi kumeshamalizika ama bado!!
mji umekuwa msafi? unafanyaje sherehe kwenye uchafu?
Reply zenye kuwakilisha maelfu ambao hawapo JF!
 
Tua Ngoma

Tua Ngoma

JF-Expert Member
2,382
2,000
Kanchi ka maigizo,yaani Tanzania ni burudani tupu,Japo ina ongeza stress pia.
 
jme

jme

JF-Expert Member
4,346
2,000
Ile kauli mbiu ya kufanya kuifanya siku hiyo kuwa ya usafi imeishia wap
 
juvenile davis

juvenile davis

JF-Expert Member
4,589
2,000
Bora,maana hali mtaani ilikuwa ni mbaya sana kifedha,matumizi hayabanwi tena,serikali imeamua kuacha ubahiri
 
miss chagga

miss chagga

JF-Expert Member
57,814
2,000
si walisema tunadisplay bidhaa za viwanda vidogo vidogo saba saba ?
 
B

Babati

JF-Expert Member
31,999
2,000
Hongera zao wataoenda kwenye maazimisho.
 
K

kabombe

JF-Expert Member
23,663
2,000
Kupanga ni kuchagua.Wakati Magufuli anaingia madarakani serikali ilikua imetoka kwenye uchaguzi,cash flow haikua nzuri na hali za miundo mbinu zilikua mbaya ndio maana alichukua hatua ya kufuta baadhi ya sherehe,lakini hakusema kwamba hatua ile itakua ni ya kudumu.
Sasa serikali ina uwezo wa kukusanya zaidi ya trilioni kwa mwezi,basi si vibaya tukasheherekea uhuru wetu,karibuni sana wapendwa!
 

Forum statistics


Threads
1,424,784

Messages
35,072,388

Members
538,098
Top Bottom