Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania bara

Kwenye tembo unaongelea uchama?!hapo uchama unatoka wapi?

Hivi unafahamu kuna wanajeshi kutoka moro walikamatwa na meno ya tembo kilo 250 au kwasababu hawatangazi kwenye vyombo vya habari kukwepa aibu!najua ninachokiongea

Sasa kama tukiongea ubaya unaofanywa na mtu ama taasisi ni nani atakaesimama bila hatia? Kupitia Jeshi ilo ilo Hayati Mwl Nyerere alifanya baadhi mauaji na kwa Jeshi ilo ilo akamtoa madarakani, naomba tusiongelee haya. Ila JWTZ wapo Imara.
 
jamani hawa watoto wa halaiki wanafurahisha kweli.....lakini utashangaa watu wamepiga mabilioni kupitia mgongo wao, hususa jezi zao, nauli na posho kama wanapewa
 
hakutakuwa na ngoma leo sababu ya kuomboleza msiba wa mandela.......tupunguze kujipendekeza kwa a.kusini jamani haitusaidii chochote
 
hakutakuwa na ngoma leo sababu ya kuomboleza msiba wa mandela.......tupunguze kujipendekeza kwa a.kusini jamani haitusaidii chochote

Kuomboleza nini wakati mwenyewe alisema akifa watu wasilie, bali wacheze.
 
Rais kikwete anatoa neno km maombolezo ya kifo cha mpigania haki na mpinga ubaguzi wa rangi na rais wa kwanza mzalendo wa afrika kusini nelson madiba mandela
 
Rais anaelezea historia ya mandela, maisha yake, harakati alizofanya na umuhimu wake ktk historia ya bara la afrika
 
Anasema mandela aliapa kuwa tayari kufa lakini afrika kusini iwe huru kutoka kwenye minyororo ya wakoloni
 
Nafuatilia hotuba ya jk, jambo moja halitaji kabisa nalo ni uhusiano wetu na south africa uliasisiwa na nani kama si Nyerere? Hamtaji kabisa...kwangu hicho ni kisasi...
 
Kama taifa tuna kila sababu ya kujivunia Amani, Mshikamano, na Utulivu vitu ambavyo ni tunu pekee tuliyorithi kwa waasisi wa taifa letu.

Kwa sasa kila Mtanzania lazima awajibike na kutimiza wajibu wake ili Taifa lizidi kusonga mbele na kuwashinda maadui zetu Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Kwa pamoja lazima tumuunge mkono Mh Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika jitihada zake mbali mbali za kuliletea taifa letu maendeleo makubwa na ustawi wa kijamii.

Na pia lazima tukiri kwa dhati toka moyoni kwamba Mh Rais ameitangaza vyema Tanzania katika medani ya kimataifa na kwa sasa tumepata heshima kubwa kama taifa na kuaminika katika uso wa kimataifa (Hongera sana Mh Rais)

Pia kama taifa lazima tuendelee kujivunia rasilimali watu tuliyonayo na tuitumie vyema katika kuleta manufaa kwa taifa na hasa nguvu kazi ya VIJANA WA TAIFA LETU.

NAWATAKIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA UHURU WA TAIFA LETU.
 
hii ni hotuba au ni nini ? Nani anatoa ujumbe huu ?
kama taifa tuna kila sababu ya kujivunia amani, mshikamano, na utulivu vitu ambavyo ni tunu pekee tuliyorithi kwa waasisi wa taifa letu.

Kwa sasa kila mtanzania lazima awajibike na kutimiza wajibu wake ili taifa lizidi kusonga mbele na kuwashinda maadui zetu ujinga, maradhi na umasikini.

Kwa pamoja lazima tumuunge mkono mh rais dk jakaya mrisho kikwete katika jitihada zake mbali mbali za kuliletea taifa letu maendeleo makubwa na ustawi wa kijamii.

Na pia lazima tukiri kwa dhati toka moyoni kwamba mh rais ameitangaza vyema tanzania katika medani ya kimataifa na kwa sasa tumepata heshima kubwa kama taifa na kuaminika katika uso wa kimataifa (hongera sana mh rais)

pia kama taifa lazima tuendelee kujivunia rasilimali watu tuliyonayo na tuitumie vyema katika kuleta manufaa kwa taifa na hasa nguvu kazi ya vijana wa taifa letu.

Nawatakia wote sikukuu njema ya uhuru wa taifa letu.
 
Ww ndo Rais wa awam ya 5 EL?mungu akusimamie tuu tupo tayar kukupigia kampein
 
Katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika,kikwete amesema watu tuwe na moyo wa kusameheana.Alisema, na nukuu"wengine hapa wanatamani wakichaguliwa watanikoma".Je,kikwete anamaanisha serikali ya ccm ni ya kikoloni,kibaguzi au ya kikaburu? Anamaanisha kuwa kwa mateso kwa raia,mauaji ya raia,ufisadi uliopo unaofanywa na ccm kwa kuwa ccm ni serikali ya kikoloni? Je,yeye ni rais wa kikoloni?
Kwa kauli ya kikwete,ccm wamepoteza uhalali wa kutawala nchi,kumbe tunatwaliwa na makaburu(yaani CCM).Je,anafanya maovu makusudi ili aje kusamehewa kama makaburu wa S.A?
 
Back
Top Bottom