Maabara ya Taifa ya Afya(NPHL) boresheni haya

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
4,262
6,908
Maabara ya Taifa inajihusisha na kufanya tafiti pamoja na upimaji wa magonjwa ya mlipuko Kama Corona n.k.
Kipindi hi Cha Corona ndiyo wanaohusika na kupima wagonjwa na wasio wagonjwa.

Msafiri yeyote anayetaka kutoka nje ya nchi hairuhusiwi kupanda ndege mpaka awe na Cheti kutoka kwa Hawa jamaa.
So kwa Upande mwingine Ni Kama ofisi ya uhamiaji pale airport maana hakuna mgeni Wala mwenyeji anaweza kutoka nje ya nchi bila KUPITIA pale (NPHL).

Wakati nataka kusafiria kwenda nje ya nchi HV karibuni ilinilazimu KUPITIA pale ili kufanya vipimo vya Covid..kwa Upande mwingine wafanyakazi wa pale wanajitahidi Sana kuhudumia kwa Moyo na nguvu zote na wanahitaji pongezi kubwa Sana ila nafikiri wakifanyia kazi baadhi ya changamoto wataweza kwenda vzuri zaidi na hata kuitangaza nchi vizuri.

CHANGAMOTO NILIZOZIPATA PALE
1. Hakuna clear instructions ( hakuna maelekezo yanayoeleweka)- unaweza jikuta unakaa pale siku nzima kutokana na maelekezo yasiyoeleweka, unaweza muuliza mtu wa SUMA JKT anakuambia vile, ukamuuliza wahudumu wakakuambia hivi, mgongano wa maelekezo unaweza kufanya ujikute unazunguka huku na huko na hata kukata tamaa.

2. Mazingira siyo rafiki..viti na shades ( vivuli) vipo lakini havilingani na idadi ya watu. So unaweza kuta rundo la watu wamesimama juani wakisubiri control numbers au majibu ya vipimo.

3. Wahudumu wasiokuwa na weledi- Ni Jambo la kushangaza kuona wahudumu wa Usafi wanahudumia wageni pale..wahudumu hao hawana elimu yeyote ya customer care na hawajui impact ya majibu yao ya hovyo kwa wageni au hata wenyeji..nilishangaa Sana kuona muhudumu wa Usafi aliyekuwa anagawa karatasi za control number akimfokea foreigner ambaye alikua anamuulizia utaratibu wa kupata control numbers.

4. Upungufu wa wahudumu- uchache wa wahudumu unasababisha watu kutokupata huduma kwa wakati...Ni Jambo la kushangaza kuona mtu anasubiri control number kwa zaidi ya nusu saa...

NINI CHA KUFANYA
1. Kuwe na watu maalumu wa mapokezi wenye uweledi watakao husika katika kupokea wageni wote na kuwapa maelekezo yanayoeleweka na si hii ya watu kuranda randa huku na huko.

2. Kuweke shades na viti vya kutosha..sioni haja ya kuwashindisha watu juani wakati Ni watu wanaokuja kupata huduma kwenu...na Ni wateja ambao Ni predictable.

3. Kuwekwe wahudumu wanaoelewa utu wa watu na waoweza wahudumia watu wa Kariba yote..coz pale wanaokuja wabongo, wazungu, wacomoro n.k. Wasifikiri jinsi sisi wabongo tumezoea huduma za hovyo na wengine wamezoea hivyo hivyo...huduma mbovu au nzuri ndiyo itakayotoa taswira ya utu wa watanzania.

4. Wahudumu wawe wa kutosha..ikumbukwe kwamba wateja wanaokuja hapo Ni watu wenye safari zao..wengine wanaemmergence wengine wanaenda kwenye biashara zao, upimaji wa corona isiwe ndiyo sababu ya kuwachelewesha kwenye Mambo yao

NIMEMALIZA
 
Duh! Mumeanza kupoteana, wewe si ndiye uko humu kila siku kubeza mambo ya Kenya, leo unachanganyikiwa na kuweka bandiko linalokosoa mambo yenu na kuliweka kwenye habari za Kenya.
 
Duh! Mumeanza kupoteana, wewe si ndiye uko humu kila siku kubeza mambo ya Kenya, leo unachanganyikiwa na kuweka bandiko linalokosoa mambo yenu na kuliweka kwenye habari za Kenya.
Tulia wewe...
 
Back
Top Bottom