Maabara ya Taifa: COVID-19 yapimwa kwa Tsh. 40,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Baadhi ya nchi zinahitaji mtu anayeingia nchi husika kuwa na cheti cha kuthibitisha amepima CoronaVirus ili aweze kuingia nchi husika.

Maabara ya Taifa ya Tanzania imetangaza kupima na kutoa vyeti kwa waliopima kwa gharama tofauti tofauti, ikitegemea kama mtu ni mtanzania au ni mgeni.

Mtanzania atapimwa kwa Tsh. 40,000. Raia wa Kigeni mwenye kibali cha kuishi nchini atapimwa kwa Tsh. 60,000 na Raia wa kigeni asiye na kibali atapimwa kwa dola 50.

Majibu na vyeti vinatolewa saa 24 baada ya vipimo. Aidha hela ya upimaji inalipwa kwa mfumo wa GePG baada ya kupewa ‘Control Number’

1596450276653.png
 
Walipewa msamaha wa madeni ili zoezi hili liwe kwa wote, sasa ya kulipisha kweli mtu aliye na kipato cha chini ataweza kupimwa!!! Kuna wanaougua dalili za corona, hawa wanapimwa au ndio kujitibu ubaki hai au ufe tu?
 
Raia wa kigeni asiyekuwa na kibali kwa nini wametaja dola wakati raia wa kwanza na wa pili wametaja kwa Tshs
 
Inawezekana vipi raia wa kigeni kukosa kibali cha kuishi nchini wakati yumo nchini? VISA? Kama ni 'resident permit', Kiswahili chake hakiwezi kuwa hicho.
 
Walipewa msamaha wa madeni ili zoezi hili liwe kwa wote, sasa ya kulipisha kweli mtu aliye na kipato cha chini ataweza kupimwa!!! Kuna wanaougua dalili za corona, hawa wanapimwa au ndio kujitibu ubaki hai au ufe tu?

Mkuu. Kwa mnaoita wameendelea euro 190 Around 501,600. 00. dalili kama hujazidiwa wote hukaa nyumbani na kujiasolate. Hakuna Tiba. Kula limao na Tangawizi. Anayetaka kuja ulaya kweli akose 40 Elfu. Acha kuwa msemaji kwa kuwa una bundle na mpingapinga mambo.
 
Shame on you that you can read but.......!!!
 
kuna nchi zimesema ili uende nchi zao unatakiwa upimwe na serikali yako na uwe na cheti.
Sasa ndo ukitaka kusafiri ili upimwe unatakiwa ulipie elfu 40..
Hyo ni shida yako wewe na huko unapokwenda serikali ya Tanzania HAIWAHUSU.
Walipewa msamaha wa madeni ili zoezi hili liwe kwa wote, sasa ya kulipisha kweli mtu aliye na kipato cha chini ataweza kupimwa!!! Kuna wanaougua dalili za corona, hawa wanapimwa au ndio kujitibu ubaki hai au ufe tu?

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Na je kama mimi nipo zangu tu nyumbani najihisi mgonjwa je naweza kwenda kupima?
 
Watanzania wengi wagumu sana kuelewa mbona mtoa mada anaeleweka, yaan kuna nchi zimetoa maelekezo kwamba nchi fulan zikitaka kuingia kwao lazima msafiri apimwe kwanza atokako awe negative, hata kwenye ndege kwa sasa hutapata Boarding Pass kama huna hii cheti yaan ni kama yellow fever, mfano dubai katika nchi walizokubal kuingia kwao East Africa ni Tanzania pekee tumekubalika japo hatukuwa na lock down maajab haya watu kama Kenya, Uganda hawapo ila sasa moja wapo ya sharti ndio hio kuwa na cheti hiko
 
Back
Top Bottom