Ma-Troubleshooters: Share nasi uzoefu wako kiufundi kwenye umeme baada ya kutatua tatizo fulani lililodumu kwa muda mrefu tujifunze

clion dismas

Senior Member
Aug 6, 2017
185
170
Heri ya mwaka mpya wanabodi

Moja kwa moja nikielekea kwenye mada, moja ya changamoto kubwa sana katika swala la kutatua shida za umeme wowote ule ni kuweza kujua chanzo kilichopelekea tatizo hilo kutokea.

Hii ni hatua inayotofautisha mafundi mafunzoni na mafundi walioiva katika tasnia hii ya umeme. "Experience is a best teacher ever".

Hapa ndipo huwa nasema kidogo matabibu wa binadamu wanapata wepesi wa kumponya mgonjwa baada ya kuchukua historia ya ugonjwa wake au maelezo yake juu ya shida aliyonayo tofauti na umeme ambao hauongei.

Nikianza na uzoefu wangu:-

Miaka 3 iliyopita nikiwa wilaya "C" mkoa "c" nchini Tanzania ilitokea shida moja iliyokua na changamoto kubwa sana kwa wataalam na wanachi wanaotegemea huduma ya wataalam.

Transfoma inayopoza umeme wa 33kV/11kV mpaka 0.4kV ilikua ikiungua, ilibadilishwa mara 3 ikisimamiwa na mhandisi mwandamizi mwenye uzoefu zaidi ya miaka 20 lakini isingepita miezi 3 bila ya transfoma hiyo kuungua tena.

Shida hii ilidumu zaidi ya miezi 5, ikabidi timu iingie mzigoni kuangalia shida ni nini, na kwanini ijirudie mara kwa mara even though kazi imefanywa na mtaalam mwenye uzoefu ndani ya mkoa?

Mrejesho wa eneo hilo ukachukuliwa ngazi ya wilaya na mkoa, moja ya sababu iliyotolewa na kuonekana ina mashiko mda huo ilikua ni kwasababu" eneo ambapo transfoma imefungwa kuna makaburi na hivyo inawezekana makeke wakawa wanafanya wao". Sababu nyingine zilitolewa nyingi tuu, ila mwisho wa siku timu ikafika site, eneo lenye taabu zake.

Kifupi transfoma ilikutwa ikiwa juu ya chanja lake lakini imeungua na eneo zima umeme hakuna.

Kabla ya hiyo kubadilishwa, iliyokuwepo iliwaka moto kabisa na kuungua baada ya mvua ya radi kunyesha.

Earthing ya transfoma ilifumuliwa (lightning arrestor, neutral na body la transfoma).

Kwakweli earthrod zilitumia nyingi tu, zaidi ya 7 ili kupata ukinzani mdogo kwenye njia ya udongo (soil resistance).

Megger ilipima resistance ya awali kabl ya kufumua earth, arrestor ilikua zaidi ya 30 ohms na neutral ilikua zaidi ya 20 ohms na body la transfoma ilikua zaidi ya 10 ohms.

Jambo jingine iliangaliwa "angle" kati ya arrestor na neutral ilikua chini ya nyuzi180. Pia insulation resistance za phase na body zilipimwa na zilikua zaidi ya megaohms.

Kimsingi, ilikuwa sehemu ya troubleshooting, lakini katika hizi stages mbili ilikua rahisi kuweza kubaini shida ni nini.

Kufupisha swala hili, kazi ilifanyika upya, earthrods zilitumika idadi ndogo katika parallel connection na mwisho wa siku resistances zote zilikua chini ya ohms 10, ikumbukwe, hakuna chemical treatment iliyofanyika kushusha resistance ya udongo kama vile chumvi na mkaa.

Jambo la kitaalam lililokua likiunguza transfoma za awali ilikua ni "nyuzi ambayo ilikua chini ya 180 kati ya arrestor na neutral na huku ndiko kulikokua kukiunguza transfoma.

"Kitaalam"

Nyuzi inapokuwa chini ya 180 kati ya arrestor na neutral, radi inapopiga, mawimbi ya umeme wa radi usambaa eneo lote la ethi kwa njia ya mawimbi duara (radial).

Sasa, kwasababu nyuzi ni chini ya 180, mawimbi hupanda kwenye transfoma kupitia eneo la output windings, na umeme huu zaidi ya million volts ukifika kwenye windings, kilichopo ni kuziunguza.

"Mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa ufungaji wa transfoma"

1. Nyuzi lazima iwe 180 kati ya arrestor na neutral na body la transfoma.

2. Waya za ethi ziingiazo ardhini za neutral na arrestor ziwe zimevalishwa (insulated) na kila moja iwe na njia yake, zisiungwe shimo moja.

3. Hakikisha windings kwa kutumi mega kabla ya installation ya transfoma.

4. Usitumie chemical soil treatment bali jitahidi kutumia njia za kiufundi kupata resistance ya soil chini ya 1 ohms. Hii ni kwasababu, chemical treatment huharibu materials (rods na bars) na itahitaji ufanye hivyo mara kadhaa kwasababu ya kuyeyuka kwake na running cost yake ni kubwa.

Muwe na wiki njema na karibuni kujadili.

"MUNGU KWANZA"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom