M4C: watinga Simanjiro..

Wana Simanjiro ni watu wa amani mambo ya kwenda kwenye mikutano na sime sio mazuri angalizo kwa wana Chadema na wana CCM hatutaki damu imwagike.

Vipi hamjafanya kama mlivyofanya Iramba?Mbona kusini damu haikumwagika au walikuwa ccm?
 
Kazi imeanza kwa ole sendeka kulibakiza jimbo uchaguzi ujao dhidi ya milya kazi anayo
 
m4c yatua kwa olesendeka kwa chopa, wakazi wa mjini arusha leo asubuhi walijitokeza kwenye uwanja wa nmc kuwaaga makamanda watatu lema, ole milya na mawazo walipokuwa wanajianda kupanda chopa kuelekea simanjiro watakoenda kufanya mikutano kwenye kata 14 yaani leo kata 7 na kesho kata 7 kisha wataelekea kwa jimboni kwa lusinde kabla ya kutua jimboni kwa wasira...


Kwasasa ndiyo tumetua viwanja vya Mererani nashangaa kwanini ipoCCM madarakani mpaka sasa...by Godbless Lema
 
Wana Simanjiro ni watu wa amani mambo ya kwenda kwenye mikutano na sime sio mazuri angalizo kwa wana Chadema na wana CCM hatutaki damu imwagike.
Wahuni wa aina ya Mwigulu Lameck Mchemba kule Simanjiro hawako, kwa hiyo tegemea mikutano ya amani tele.
 
Jamani Mwacheni JK, aliahidi katika moja ya kampeni zake mwaka 2005, akarudia 2010 kuwa suala la ajira atahakikisha "kila mwaka atatutengenezea ajira milioni moja" NA SI AJIRA MILIONI MOJA KWA KIPINDI CHOTE CHA YEYE KUWA RAIS KWA MIAKA 10..nilimnukuu vizuri jamani.....Amejaribu na kweli ameweza. Tatizo la ajira alizozingeneza ni AJIRA M'BADALA .

Naziita m'badala kwani ni kama vile UZURURAJI, UJAMBAZI, WIZI, ETC ETC. Huku akijua hao watanzania aliowaahidi wana elimu na hawajui pa kwenda.

Nachoka kabisa.
Zilifanyika reshuffle tele tu wengi wakatupwa nje....wamekosa pa kwenda hivyo wameishia kujifunza kazi m'badala ndio hizo nilizozitaja.
 
si kweli kuwa watanzania wote waliohudhuria hapo hawana ajira.Hao ni wapiganaji hata kama wana ajira za.Wanaacha kwa muda na kwenda kuwatia moyo wana mageuzi.
 
Sikujua kama idadi kubwa ya Watanzania hawana ajira rasmi mpaka nilipoona picha ya waliokwenda kuangalia Helcopta ikiruka

Kwa sababu ya desperation and anguish ya ukali wa maisha wanaona CCM imewasaliti. Hakuna maisha bora maana uchumi umeharibika. Ukiona hivyo ujue CCM bye.
 
Kwa Yeyote Anayehusika:

Aliyesema chadema ni chama cha watu wa kaskazini ni mnafiki, mchochezi, msaliti, m'baguzi na muuaji.

Kwani CCM ni chama cha watu wa wapi? Sasa huu ubaguzi wa nini? Lini tutapevuka na akili zetu kuwa na akili? Akitokea mtu wa mbeya akaanzisha chama kitakuwa ni mali ya watu wa mbeya? Yule babu aliyeasisi Chadema alikuwa na fikra pana.

Lazima tumuheshimu mtu aliyetumia nauli yake kumfuata rais wa Kenya (aliyekuwa mwenyekiti wa eac) mzee Kamau Ngengi wa Muigai kwenye uwanja wa golf na mara nyingine pale Kasarani. Alitumia fedha yake na kurudi nyumbani. Lengo ni kudumisha uhusiano pamoja na kujadili maendeleo ya nchi yetu bila kujali ni wapi atamkuta mwenyekiti.

Kwa ujumla yeye ni baba mlezi aliyewalea watoto wake vizuri.....na hao ndio chadema

Enzi hizo rais huyo wa Kenya alikuwa ananyimwa usingizi na makamu wake, Jaramogi Oginga Odinga.
Ni vizuri tukipevuka. Kuna mfano mzuri sana, na huwa najifunza kutokana na siasa za kibaguzi za za south africa. Democratic Party ni chama kilichoasisiwa na mwanamama wa kizungu, Helen Zile, kutoka kusini (Capetown) lakini chama chake kimesheheni watu weusi toka sehemu zote ingawa yeye ni mzungu, chama cha waafrika anc kipo na changamoto zake na hakina wazungu ingawa wapo baadhi.

Kimeasisiwa na watu weusi, tena wa kaskazini, lakini ni mali ya wote....sasa kama mtu akiona chama fulani hakimfai aende kwenye kile anachokipenda. Pia ni mchezo mchafu kuanza kuwabagua watu.......sera safi za CHADEMA zinapendwa kwa kuwa hazimshambulii mtu bali sera za chama husika...hakuna mtu anaitwa ccm, au CHADEMA ila ni sera.

Hivyo kwa mtazamo wangu: Tanzania bila CHADEMA haikaliki, umasikini bila CHADEMA hautakwisha, maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezekani bila mabadiliko ya kweli.
VIVA CHADEMA ..VIVA




 
kwa mjibu wa Godbless Lema anasema katika mikutano yaleo wanachama zaidi ya 1200 wanejiunga na chadema na anasema watu walikuwanajitokeza kwa wingi sana...mwenyekiti wa kata ya mererani amesema kabla ya mkutano huo mkubwa kufanyika jion ya leo walifungua matawi matano makubwa..bye bye Ole Sendeka, kwa kheri ccm.
 
Ikitoka huko ije kwimba hatuna wabunge; majimbo yote mawili wawakilishi wetu wanazidi kulala
 
Wana Simanjiro ni watu wa amani mambo ya kwenda kwenye mikutano na sime sio mazuri angalizo kwa wana Chadema na wana CCM hatutaki damu imwagike.

Simanjiro sio Iramba bana!......huko hawaongwi kwa pombe za kienyeji......usitegemee ya iramba kutokea huko!
 
Simanjiro sio Iramba bana!......huko hawaongwi kwa pombe za kienyeji......usitegemee ya iramba kutokea huko!

jibu zuri sana, ila hata huko iramba walioleta fujo wengi wao walikuwa vijana wa ccm kutoka dar sasa huo uhuni wasithubutu kuupeleka huko...
 
Back
Top Bottom