M-wekeza kutoka Vodacom Riba 13%

M-wekeza kutoka Vodacom Riba 13%

Kampuni ya vodacom imeanzisha mfuko wa uwekezaji ambapo mwekezaji atapata faida 13% kwa mwaka .

M-wekeza ni huduma inayomuwezesha mteja wa M-Pesa kuwekeza kima cha chini kabisa kuanzia TZS 1000 na zaidi kutoka M-Pesa na kupata faida nzuri bila gharama ya ziada.

Wateja wote wa M-Pesa wanaweza kujiunga na kusajili Akaunti za M-wekeza na kuanza kuwekeza Unachotakiwa kufanya ni kupiga *150*00#>Huduma za Kifedha>M-wekeza.

M-wekeza ni huduma ya kidigitali inayorahisha uwekezaji kiganjani mwako bila gharama za ziada.

Pia kupitia M-Wekeza mteja anaweza kuwekeza Kiwango chochote na kupata faida mpaka 13% endapo atawekeza fedha zake kwa mwaka mzima na unaweza pata taarifa ya kifedha ya uwekezaji wako muda wowote kiganjani mwako.^EK
Kwanini sio kila mwezi uwe mwaka?
 
Hawa jamaa kuna vipengele vichache wakiviingiza kwenye mfumo wao, watakolect milioni and millions!, aidha wakishindwa monthly waweze kutoa gawio kila baada ya miezi mitatu kwa anayehitaji kupata fedha za kujikimu,
Waige toka safaricom kenya, watu waweze kutoa hela zao muda wowote wanaotaka
 
Hii sekta passive income inakuja kwa kasi. Voda 13%, nimeona bank ya Azania na wao wameleta 12.5%, nasubiria atakayeleta 25% hata 100%🤣
Hamna atakayezidi ile 15%+ ya BOT kwa sababu wote hao ni madalali wa BOT.

Mnawapa hela wao wanapeleka BOT wakipewa ile 15%+ yao wao wanawapa 13% wanabakiwa na 2% faida yao.
 
Back
Top Bottom