m-tanzania creative | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

m-tanzania creative

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by kimtu, Dec 5, 2008.

 1. k

  kimtu New Member

  #1
  Dec 5, 2008
  Joined: Sep 19, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna chizi flani alipanda juu mnara mrefu sana,uliojengwa kwa zege,na nondo..sikumbuki ni wa kumbukumbu au laah?!!na kupanda kwake ni shughuli pevu,urefu ni kama zile twin tower za epa.....basi shughuli ikawa kumshusha huyo chizi kwa usalama wake...walianza na mgambo wa jiji,wakifuatiwa na vitengo vingine vya usalama wa taifa ilikuwa kama ifuatavyo...

  mgambo wa jiji:-kwa kutumia kipaza sauti-tunasema shuka haraka,la sivyo tutakuchakaza kama tunavyowafanyia mama lishe,na wamachinga....

  chizi:-hahahahahahahaaaaaaa-kicheko cha dharau!!!

  askari (ffu):-tunakuomba ushuke haraka sana la sivyo tunakupa muda wa nusu saa usionekane hapo..kama unabisha waulize wanafunzi udsm...
  chizi:--hahahahaahahahahaa-kicheko cha dharau!!!!!

  jeshi la wananchi(jwtz):--tunakuomba ushuke haraka sana,la sivyo tunakufanya kama idi amini mwaka 79....

  chizi:-hahahahaaahahahaaahaaa kicheko cha dharau.

  Baada ya kutumia kila mbinu ilishindikana kumshusha chizi...
  Basi kijana flan simpo sana,aliyekuwapo kwenye tukio,aliondoka kwa kasi eneo la tukio..baada ya muda mfupi...alikuja kaongozana na chizi flan......wakati huo makundi yote yaliyoshindwa kumshusha chizi yakishuhudia..maongezi yakawa ifuatavyo kati ya chizi aliye chini na chizi aliye juu ya mnara...

  chizi wa chini:-nakuomba ushuke haraka iwezekanavyo..
  chizi wa juu ya mnara:-hahahahahaaaaaaa kwa dharau!!!

  chizi wa chini:-nakupa dakika 5 uwe chini..la sivyo naukata huu mnara..kwa kiwembe...huku akimuonyesha chizi wa juu,kiwembe...

  chizi wa juu:-kwa kuogopa mnara utakatwa na kiwembe chizi alishuka juu ya mnara kwa dakika mbili........
   
Loading...