M-Pesa Gawio.

Eheeeeee! teaaaaanaaaa nyie VODA nilikuwa na hasira na nyie sana! Tabia gani kunistua moyo wangu, eti meseji ya empesa halafu nikifungua oooops imethibitishwa nimepokea 250/= sijui kutoka faida..
Sitaki upuuzi wenu huo, mkome kabisa.
Tell her my friend .. .
 
Wengine tukiona tu imethibitishwa ,moyo unakunjuka ,sasa unasoma SMS unakuta eti umepokea 250,,
 
Message ndefu mpaka inakubidi ukaoge, ule then ujipumzishe kwenye kochi ile unafungua message yao unakuta imethibitibshwa umepokea kiasi cha tsh 175 ya gawio kutoka Vodacom, Salio laki jipya ni 700,175/=. Hapo naona mnatia nuksi tu Salio langu lililokuwepo.
 
Vodacom to me is best hasa kwenye swala la network na vifurushi bila kusahau huduma zao huwezi linganisha na mitandao mingine.
 
Japokuwa tu nilishindwa kurenew line yangu ya voda kisa tu nilipoteza kitambulisho ila voda wako vizuri.
 
Back
Top Bottom