M/kiti BAWACHA Agnesta Lambert, anashikiliwa kituo cha Polisi Oysterbay kwa kosa la kupiga picha mahabusu

Hivi Polisi wanaogopa Dunia kuona wanavyohifadhi watu vibaya
Sasa tutaanza kuzitoa picha mpaka za ndani ya mabanda yao ya bati wanakoishi
 
Sheria za nchi hii zinafanya kazi upande mmoja tu shilingi.
 
Yaani kwa ujinga huu hata waliokuwa wanampenda japo kidogo huyo mzee wa frastrations watamchukia tu nakwambia
 
Agnesta Lambert. Ha ha ha, mzungu wa wapi huyu?
 
Hata marekani huwezi kuingia kituo cha polisi ukapiga picha bila kibali.

Kama unataka kujua sheria ipo au haipo chukua kamera yako nenda pale central polisi nje ya jengo uanze kulipiga picha halafu ndio utajua sheria vzr.


Huyo mwenyekiti kakosea acheni sheria ichukue hatua
 
ndugu zangu chadema hili ni kosa kisheria na linafahamika kwa sheria za jeshi la polisi/uhamiaji/magereza na hata jeshi la wananchi
ni kosa kupiga picha ukiwa ndani/nje ya kampaundi zao
 
Wakati Chadema wanalalamika kuonewa na nyinyi mnaona ni sawa...Nchi inaendelea kupoteza uhalisia wake.
Mbegu mbaya inaendelea kumea..na hii ni hasara kwa Taifa na vizazi vijavyo.
 

Nyie si mna bunduki na mabomu tuueni tu mubakie wenyewe.
 
Hata mbwa atakuwa na heshima kuliko baadhi ya wachangiaji! Jana Mambosasa kasema hakuna majeruhi mahabusu na kwamba tunapewa uthibitisho wa picha (hata kama ni kosa) mbwa wengine wanachukia!! Mbwa ni mbwa tu hata kama ni binadamu!
 
Usipige picha hapa... Unapiga..

Huyo dada hana tofauti na wale wanaoambiwa usifanye biashara hapa, halafu yeye ndio kwanza anapaki beseni lake la mihogo na machungwa..

Tii sheria bila shurti!
Mbona Pale ilala boma ofisi ya mkuu Wa mkoa kuna zuio la biashara lkn Bdo Kna watu wanafanya biashara

Ova
 
Pamoja na kushikiliwa kikatili lakini sheria haitoi opportunity ya kupigwa picha katika mazingira hayo. Alichopaswa kukifanya ni kuipiga kwa kificho na kiisambaza kwa kificho, lakini si kama alivyofanya huyo bint.
 
Swali la msingi ni kwann ampige picha huyo Aida? na kwann leo?....Aida ni mhanga anayehitaji msaada kwa namna yoyote ile, ili kufanikisha hilo lazima kila mbinu itumike kuonesha ukweli iwe mbinu halali au isiyo halali! kuongeza msukumo kwa Jeshi la polisi kumtendea haki Aida. Ni rahisi kumlaumu mwenyekiti wa Bavicha lakini inahitaji uwendawazimu nakujitolea kufanya aliyoyafanya...Saidieni serikali ifanye reformation jeshi la polisi ili haki za raia zisikiukwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…