M/kiti BAWACHA Agnesta Lambert, anashikiliwa kituo cha Polisi Oysterbay kwa kosa la kupiga picha mahabusu

Unamshikilia mtu mahabusu kikatili halafu unakataza kupiga picha? Jambo la kipumbavu kabisa! Lakini najua hata kuandamana litakuwa ni kosa tena maandamano yetu yatakuwa kushinikiza utawala huu uondoke madarakani hivyo tutakuwa tunafanya uhaini! Ila tutaandamana maana ndiyo njia sahihi ya kupambana na mshenzi.
Wewe andamana huku JF huko mtaani huwezi
 
Hivi hawa polisi wetu hawana sura za haya na aibu?! Mbona wanafanya vitu vya aibu sana na kuidhalilisha serikali?!
Lakini huyo mw/kiti kakosea kweli aisee unapigaje picha sehemu ile bila ruhusa au kibali....tena hiyo hali ya huko sijui ni kwann hakufikiria, sometimes tuache kuProvoke hao polisi,

Pamoja wanamakosa mengi lkn kwenda kwenye anga yao na kupiga picha aisee hata mm namshangaa huyo mw/kiti....ni zuzu.

Angetafuta hata hidden camera ss, empty set kabisa rubbish #*$&%@%&#&
 
Kama Kosa ambalo huyo Mwenyekiti wa BAVICHA amelifanya ndiyo hilo la kupiga Picha hapo Kituoni au mule ndani naungana na Polisi tena kwa 100%. Na kilichonisikitisha zaidi muda si mrefu nimetoka kupitia Kurasa ya Mbunge wangu na Mwanamke ambaye namheshimu kabisa na ni Mwanasheria mzuri tu Dada yangu Halima Mdee ambaye naamini kabisa kwamba hata Yeye anajua fika kuwa kupiga picha eneo la Polisi au mule ndani walipo wale Mahabusu ni Kosa lakini Yeye ( Halima Mdee ) amelaumu na kama vile Kudhihaki hatua iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi.

CHADEMA Watani zangu wa Kisiasa kama msipokuwa makini, kujitathmini na kuacha kuishi kwa mazoea na kutawaliwa na mihemko yenu kila siku mtakuwa mnalialia tu hovyo, kuilaumu Serikali / Mamlaka na Vyombo vyake vyote vya dola kuwa inawaonea wakati kumbe Kiuhalisia kuna muda nyie wenyewe ndiyo huwa mnakuwa sehemu ya matatizo ambayo yanawakumba.

CHADEMA badilikeni tafadhali.
Subili tu, iko siku isiyo na jina ikifika. Hata hiyo simu unayotumia kupost ujinga hutaiona!!
 
Kwa hiyo siku hizi kupiga picha nikosa
Hutakiwi kumpiga picha mfungwa wala mahabusu, labda uwe na kibali Cha kufanya hivyo.
Vile vile huruhusiwi kupiga picha gereza, kikosi cha jeshi wala kituo Cha Polisi, iwe ndani au nje.
Hayo yapo kwa sababu za kiusalama.
Huruhusiwi kupiga picha Askari wakiwa mafunzoni, iwe jkt,jwtz Magereza wala polisi.


Tusiwe watu wa kupinga kila kitu.
 
Hata kwa hili bado mna mtetea? Hivi kweli hata hilo hamtambui ni kosa?
Polisi wanauona uhalifu wa wapinzani tu kwenye siasa.....yule Mkurugenzi alewanyima barua za viapo vya kusimamia uchaguzi hadi kuvitoa baada ya watu kuandamana, yeye hakuvunja sheria!?

Watanzania tunapenda sana kukebehi misiba ya wenzetu lkn tunajua sana kutia huruma yakitupata
 
Pia polisi hajawahi sifiwa dunia nzima,na ukiona raia anasifu polisi jua kuna sehemu polisi atekelezi kazi zake vizr
Uongo wako huo, eti hakuna polisi aliowahi kusifiwa duniani, duh ujuha wako huo!! Umetembea tandahimba!!
 
CHADEMA Watani zangu wa Kisiasa kama msipokuwa makini, kujitathmini na kuacha kuishi kwa mazoea na kutawaliwa na mihemko yenu kila siku mtakuwa mnalialia tu hovyo, kuilaumu Serikali / Mamlaka na Vyombo vyake vyote vya dola kuwa inawaonea wakati kumbe Kiuhalisia kuna muda nyie wenyewe ndiyo huwa mnakuwa sehemu ya matatizo ambayo yanawakumba.

CHADEMA badilikeni tafadhali.


hakuna UTANI wa namana hiyo huku wengine wanaoza na bila kufikishwa mahakamani.
 
Wanaharakati limbukeni ambao kwa kiasi kikubwa wamejivika uanachama wa Chadema siku hizi hapa nchini na kwingineko walipo; mara zote wanapenda njia za mkato kufikia malengo yao. Malengo yao hayo asilimia kubwa ni ubinafsi. Wanaharakati hawa limbukeni hawataki kabisa kufuata taratibu katika ama kufikisha ujumbe wao ama kudai haki yao.

Sishangazwi na hatua ya jeshi la polisi kumkamata huyo 'mpiga picha'!
 
Sheria ipi ina nguvu kuliko nyingine n.a. kwa nini?
A.Raia kajeruhiwa n.a. kunyimwa matibabu/dhamana-hakuna ukiukwaji wa sheria na haki?
B.Afisha wa jeshi /taasisi kukiuka au kavunja sheria-tume inaundwa kuchunguza!

Raia akikosa tume haimhusu?

UNDUMILA KUWILI!
 
Polisi wanauona uhalifu wa wapinzani tu kwenye siasa.....yule Mkurugenzi alewanyima barua za viapo vya kusimamia uchaguzi hadi kuvitoa baada ya watu kuandamana, yeye hakuvunja sheria!?

Watanzania tunapenda sana kukebehi misiba ya wenzetu lkn tunajua sana kutia huruma yakitupata
mlipeleka taarifa polisi kuwa mmenyimwa viapo
 
Back
Top Bottom