Kabla sijameza mate wala sijabuni sala
Naambiwa walikuja wazabuni kwa biashara
Na kwakua nilichelewa kufungua ofisi
Mchongo ukafa, nimeingizia kampuni hasara
Baada ya masaa kibao ya kufikiri
Ofisi ikaweka kikao kunijadili
Waliniona driver nimeangusha basi
Wakafikia mwafaka wakunifukuza kazi
Nikatahamaki, sikujua lakufanya
Pale kwenye kamati hakuna wa kumtazama
Nikahisi ni mipango ya kikuda imefanywa
Sio gari tu, maana hata nyumba nilinyang'anywa
Nikajiuliza huruma imekwenda wapi?
Kila mtu alijua kua nilipenda kazi
Niliheshimu kama navyoheshimu ndoa ama mzazi
Ama muumba, leo nimepata doa kwenye shati
Acha familia, vipi deni la ofisi
Wamenipa mwezi, nikifeli watanifilisi
Mtoto shule, pia bunju nina shamba la kukopa
Sijalipa na kijiji nina ndugu wa kutosha