Alisema hatashangazwa kama atasikia Lwakatare kaihama CUF kwa kuwa ni kawaida ya viongozi wa Tanzania Bara waliomo ndani ya vyama vya upinzani kuhama chama mara yanapotokea mabadiliko ya uongozi.
Lipumba alisema tabia hiyo ya kuhama inaonekana kuanza kuwa sugu, lakini ni vema wanaohama wakajenga utamaduni wa kutambua na kukubali mabadiliko yanayofanyika ndani ya vyama vyao.
Prof wa Pumba akiwa kazini!
Mkuu sina uhakika kama sheria ya vyama vingi inaruhusu chama kuwa upande mmoja wa muungano. Labda kama unazungumzia kuungana kiutendaji tu wakati kikiwa bado kina presence Bara. Nadhani hilo linawezekana.Marwa post yako ina ukweli mkubwa sana na si biased kama nyingi hapa zilivyo.
Ila tu napenda niweke wazi kuwa kafu itaendelea kuwapo Zanzibar tena zaidi Pemba lakini bara itaungana na vile vyama vingine si unajua? nncr,tlp,udp,dp na ww ongeza orodha hapo. Vipo kama havipo vile.
naona hii issue imekuwa BIG DEAL kwa wana chadema eee?
Kuna utofauti kati ya Mwanafunzi aliyeko Lab na yule aliyeko class. Aliye class ataweza kujifunza na kusoma nadharia ilihali aliyeko Lab anaweza kuona matokeo ya nadharia kwa vitendo.
Unalolisema Bw. Masatu ni sawa na aliyeko sebuleni kubishana na mpishi juu ya chakula kuiva. Mpishi anasema chakula bado, aliye sebuleni anasema kimeiva, pakua.
Tuliokuwepo wakati mageuzi na vyama vinaingia hapa BK tunatambua kuwa CUF ni Lwakatare but vice versa is true not! Selestine Mutakyawa ni NCCR-Mageuzi lakini NCCR-Mageuzi siyo Selestine Mutakyawa.
Ni jambo la kawaida kabisa kwa Watwale mtu kuwa icon ya industry. Katika medani za kisiasa BK, Lwakatare ni selling Brand yeye kama Lwakatare na si kama Chama.
Thibitisha haya niliyoyaandika kwa kuangalia njugu za kadi za CUF zitakazorejeshwa kesho.
Masatu, Kuna ka-PM nakutumia
He!!! Yanafika huku tena!...lakini sikulaumu sana maana YOU ARE ALCOHOLIC....bila shaka mvinyo wa chuki umekulevya....
Ohhh, Simpendi kaka yangu Lipumba kama mwana siasa maana naona anatutia aibu Wanyamwezi kupapatikia Waarabu. Ila jambo moja ni kweli kwamba JAMAA NI PROF. WA UCHUMI MZURI sana. Kundi lao wakisoma Tabora Boys, walikubaliana kuwa wote waje wawe Madaktari. Kweli wote walienda kuwa madaktari kasoro LIPUMBA ambaye aliwasaliti wenzake na kwenda kusomea Uchumi. Shule yake aliisoma vizuri tu na kufaulu saafi kabisa hadi kuja kuwa Prof. Kama mwana siasa, hicho ni kitu kingine kabisaa. Sawa na Dr. Bilal. Kama mwalimu wa Atomic physics, jamaa ni mkali saana na anatambulika hadi nje ya Tanzania kwa umahili wake ila kama mwana siasa kwa kweli ni mzinga wa soo. Tujuwe kuchambua mchele na puma alionao kila binadamu. Vinginenvyo tutaonekana tunadandia treni la umeme kwa mbele!!!
Masatu, wee mbona inakuuma sana hii topic ya Lwakatare, uliibiwa na jamaa nini? Na Wahaya wakishapita na ile style yao ya Kate...... wee mtu wa upande wa pili wa ziwa unabaki tu kuja kwenye JF kumalizia hasira zako teteteteee ......
Kuna wengine wanasema kabisa kuwa ile methali ya wajuu mngoje chini, kwao haifanyi kazi. Ukimtaka basi mfuate juu kulekule. Lwakatare ni mtu wa hivyo, au umfuate hukohuko na kumpa habari yake kama utaweza au kaa kimya kabisaa. Kupiga kelele hapa JF kwa kumpakazia ohh hivi au vile haimpunguzii jamaa Unyota wake kwa Wahaya. Upende usipende, jamaa atakuwa CHADEMA na atakuwa Mbunge, then what?? Hii imekaakama Makelele ya Chura akifikiri Tembo ataogopa kuja kunywa maji.
Wananifurahisha zaidi wanaokuja hadi huku kumfuata Kitila Mkumbo, eti akajibu kesi ya HOUSE GIRL, tena wanadai kwa nguvu utafikiri Mkumbo kazi anayoifanya kaipata kwa kuomba wananchi. Jamaa kakata umande na kufikia hapo alipo. Hadi siku atakuja kuomba kura, hapo ndipo tuanze kumdai atupe maelezo ya hiyo kesi. Ila kwa sasa, Mkumbo weee achana na hili swali. Umesota kwa nguvu yako mwenyewe kufikia hapo na si kodi za wananchi. Mwenye wivu juu yako mwambie ajinyonge.
Profesa Lipumba ktk hotuba yake amekiri kwamba wana-Kafu wana tabia ya kuhama. Hasa wale wa bara. Hiza, Akwilombe na wengine amewataja kama ni mifano.
Kuna wanaJF wengine, kama Masatu, ambao ni optimistic kwamba bado Kafu inadunda, na kwamba Lipumba ana role ya ku-serve Tanzania tupate demokrasia na maendeleo ya kweli. Huenda Lipumba ana uwezo lakini ni lazima awe na chama madhubuti.
I happen to know the Professor well, and respect him as a serious politician and a genuinely committed patriot. But I seriously suggest that he will figure in Tanzania's history, as a great democrat and liberator, if he now follows Wilfred Lwakatare to join hands with Chadema and its leaders to uproot grand corruption and rampant misuse of public funds and other resources of this country.
I am confident that Chadema leadership will find a fitting position for Lipumba in its hierarchy, just as I know Wilfred Lwakatare may already have a suitable place in Chadema in which to continue serving the people of Bukoba constituency and Tanzania as a whole. Lipumba will prove that he is not "king'ang'anizi" cha madaraka ktk kafu, kama baadhi ya wana-JF wanavyosema, endapo ataamua sasa ni wakati wa kuimarisha chama ambacho kina dalili za kutoa changamoto stahili kwa ccm na mafisadi wa Tz.
Hao wana-JF wanaorudia accusations za udini ktk Kafu na Uchagga ktk Chadema, wanaonekana wameishiwa na hoja zinazolenga uimarishaji wa demokrasia, uhuru na uwezo wa dhati wa wananchi kumiliki maliasili zetu na kuendesha nchi yetu.
Ninachotaka kusisitiza ni kwamba, kama vyama vya siasa vya upinzani vimeshindwa kuungana rasmi ili kutoa changamoto stahili kwa ccm, basi viongozi wazalendo wa kweli wajiunge na chama kilichodhihirisha kina mwelekeo wa kufaulu kutekeleza jukumu hilo. Kwa sasa chama hicho ni Chadema.
Thanks,Lipumba ni Profesa wa Pumba kweli si uongo. kama kashindwa kukipeleka chama kisomi, sasa tumsemeje?
Arudi darasani kufundisha pumba zake.
La Haaaaaashaaa!!!!Junius, pamoja na yoote yaliyosemwa, naomba tujenge tabia ya kuwa waangalifu, hivi unawezaje kuchanganya jina la Wilfred na Alfred? Huyo mwandishi naye anaandika Winfred...jamani, seriousness ikikosekana kwenye mambo kama haya, ndiyo kusema inakuwa tabia hata kwenye mambo makubwa.
Nimesikia kuwa tayari kaingia Chadema jana jee kuna ukweli?
Inaonekana wewe ndio uliomuandikia hizo barua zake zina makosa mengi ya kiswahili.Tukuulize wewe uliopo Kanyigo....