Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA


Mkandara,
Jamaa mwenyewe alishasema hii ni story japo akasema full story lakini inabaki ni story vilevile. Hapo kaongea kikurya angaongea kiswahili angesema "hadithi." Labda tumwulize kama Sara Dumba aalivyokuwa akiwauliza watoto wa kipindi cha mama na mwana RTD enzi zileeeeee. "Hadithi hiyo alikufundisha nani na inamaanisha nini?"
 
Lwakatare, endelea mbele. Tunaamini Jimbo la Bukoba mjini ni lako Mwaka 2010.
 

Mkuu
Ndiyo maana mimi siamini mabadiliko kuletwa na chama ,Na mimi nionavyo ktk hali halisi iliyopo saizi Tz kubadili chama si majibu sahihi na kukiacha chama madarakani pia si viable soln.Sasa chagua ama kunyowa.
 
Nawashauri wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF Wafanye haraka kuifanyia mabadiliko katiba yao ili wakutane tena Mwezi Ujao na wapitishe kwa Umoja kuwa sasa NAFASI YA NAIBU KATIBU MKUU itakuwa ni ya KUDUMU tena ni Kwa Mhe LWAKATARE Hadi mwisho wa Maisha yake hapo ubishi utakuwa umekwisha na MASANGARA atayatapika nakurudi kwa kasi katika nafasi yake na CUF haitakuwa tena na Makosa mbele yake kama ilivyo hivi sasa Kwa Kuchanganyikiwa kwake alivyojichanganya kutoka Kwenye TAASISI na Kukimbilia Kwenye UZAWA na UMAJIBO
 
Siasa ni kama soka ya kulipwa. Ukiona team uliyopo haikupatii kikombe una tafuta usajili sehemu nyingine.
 
Tatizo la viongozi hawa wa upinzani ni uchu wa madaraka
 

ahahahahahahah uuuuuuuuuuwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Hii imenichekesha sana.
Junius, Lwakatare kakuumizeni sana sio??????
Si mwacheni afuate hayo madaraka Chadema ili mradi kafu hamnayo? Sasa shida iko wapi?
Wala hajasema anafuata madaraka huko chadema. Nyie kafu hii mmeipata wapi?
Si mwacheni afuate hayo madaraka yaliko?
Nina imani yeye bado ni mali ya kafu. Usitie hofu😀
 
Tatizo la viongozi hawa wa upinzani ni uchu wa madaraka

Niambie wa sisi M asiyehitaji madaraka nyie watu!!!!!!!!!!!!!
Mbona walipigana juzi tu tena kwenye baa mpaka JMK aliwashangaa!!!!!!!!!
Ukitaka kuishi bila ya kuwa kiongozi hata nyumbani kwako, ujue umekwisha.
Naturaly mwanadamu kaumbwa kutawala. Asiyetaka kutawala ....................
 
Bukoba wanachama wa CUF nyoyo zao ziko kwa Cuf au Lwakatare?
 
MM wala sijaumia sijuwi CUF wenyewe vp?
Ninachoweza kusema kuwa ni Lwakatare mwenyewe amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa ameamua kujivua uongozi CUF kuwa amekuwa sidelined katika uongozi.
Na yeye mwenyewe ndiye aliyeitisha mkutano BK kuwauliza watu wake kama aende chadema au abakie CUF, kwa yeye Lwakatare huko anakowaomba wananchi wake wamruhusu aende (chadema) hatokuwa sidelined katika uongozi, ndo ninawauliza chadema vp watampa anachokitaka?
 
Siwezi wajibia Chadema. Ili mradi viongozi wengi wako hapa wakiona sababu watakujibu kama wanaweza kumpa au hapana.
Hivi ngoja kwanza niulize kwani kafu walimpa nini kiasi kwamba asitoke kafu?
Nyerere alisema chama sio mama yake. Anaweza kuki bull shit
 
MkamaP,
Mkuu nakusikia sana na ndio maana siasa za Bongo nimesema mimi siziwezi hata kidogo. Matatizo ya ndani CCM, CUF Chadema sijui TLP yote hayatokani na maauzi yoyote yanayohusiana na maamuzi kwa ajili ya wananchi..Wote hawa ugonvi wao mkubwa ni viti vya Uongozi..
wapinzani wameshindwa kuungana sio sababu za mrengo, sera wala rangi ya bendera isipokuwa nani atakuwa nani ktk muunganmo huo. Mvutano wa nguvu ya watu hawa ndio imevuruga muungano na haitawezekana hata siku moja..
Unajua kuna rafiki yangu Myahudi, yeye alinambia kitu kizuri sana jinsi alivyowasoma watu weusi na hasa Waafrika.. Tunajali sana Title yaani jina la cheo kuliko kila kitu... Mtu mwenye degree yake akipewamkazi ya kufagia klakini akiitwa MD basi ataikubali hiyo kazi bila hata kuuliza mshahara, wala majukumu ya kazi hiyo maadam apate hilo jina la Managing Director..

Sasa huko ktk vyama utasikia nafasi kama hizi zipo wazi ni lazima watu watatoana roho..TITLE mkuu wangu Wabongo tunapenda sana jina kubwa bila kujali responsibility zake.. Sasa tazama majivuno ya Lwakatare! kila anachojivunia ilikuwa part ya kazi alizobidhiwa alitakiwa/tegemewa kufanya nini chini ya hapo!..
Hivi kweli angekuwa hana madaraka hayo angeyafanya yote yale kwa roho nyeupe?...na hivi kama asingekuwa CUF angeweza kulitengeneza jina lake nje ya Bukoba!.... sidhan, sidhani sidhani.. mafanikio yake yametokana na kuwepo CUF na sii kinyume. CUF haikumtegemea Lwakatare!

Hata hivyo pamoja na yote haya sikuona mahala Lwakatare akizungumzia chama au kuwalumu wana CUF isipokuwa uongozi wa juu wa CUF.. Na mapendekezo yake hata kama akiondoka CUF ni muhimu wayafanyie kazi..Waswahili wanasema - Hata mchawi husema ukweli...
 
Waungwana,

Kama viongozi wa CUF - Mwenyekiti Lipumba na Katibu wake Hamadi wanatuhumiwa kung'ang'ania viti vyao, basi nafikiri na huyu ndugu yetu ni mng'ang'anizi wa cheo chake. Yale yale ya Tambwe Hiza. Viongozi wote wa Tanzania ndivyo walivyo. Pakiwa na mtetereko wowote katika nyadhifa zao basi zinatafutwa sababu za kuhamia kwingine kwa matumaini ya kuendelea kuwa madarakani.

Wangapi tunafiri au kudhani Nyerere angebaki TANU au CCM kama angenyang'anywa uongozi? Nkrumah alilikikimbia chama cha wazee wake akaanzisha cha kwake ili mradi tu awe kiongozi. Na Zuberi Mtemvu hivyo hivyo. Na mimi pia. Cheo kizuri bwana, hata kama ni cheo tu! Tuna kaaazi kweli kweli.
 
Ukitaka kuishi bila ya kuwa kiongozi hata nyumbani kwako, ujue umekwisha.
Naturaly mwanadamu kaumbwa kutawala. Asiyetaka kutawala ....................
Ama kweli kama mambo ndio haya kaaazi kweli kweli..
Miafrika - NDIVYO TULIVYO..
 
Hivi punde CUF-Taifa wamemaliza mkutano wa siri. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kumdhibiti Lwakatare kwa kurejea aliyoyazungumza kwenye mikutano yake (wa ndani na wa hadhara) tarehe 19/06/2009 mjini Bukoba.

JF ndiyo imekuwa chanzo cha Uongozi kujua nini kinaendelea Bukoba na kupata mwanga wa kinachoendelea ndani ya chama.

Paparazzi wetu ambaye ni Shehe aliyeweza kupata nafasi katika altare ndani ya kanisa ambamo ulifanyika mkutano huo anatuandalia taarifa kamili.
 
DVD ya Mkutano wa Lwakatare alioufanya Bukoba tarehe 19/06/2009 inapatikana Sasa.
Kwa wale walioko Dar es Salaam tuwasiliane kupitia 0717041781
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…