Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,907
- 1,082
Kikukubwa hapa ni kwamba Lwakatare amesema kuwa alipokuwa n cheo ndani ya CUF alikuwa akilipwa sh 300,000 kwa mwezi hivyo amewaomba wananchi waone ni jinsi gani alivyokuwa anafanya kazi nyingi na kulipwa kiduchu.
inapatikana hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...are-wa-cuf-kuhamia-chadema-17.html#post495735Mijadala ya CUF ndani ya JF yasababisha Mkutano wa ghafla CUF-Taifa
Yah, Imetajwa kwenye kikao. Na baadhi ya wajumbe ambao wanaweza kumudu hii njia mpya ya mawasiliano wamepewa jukumu la kujiunga na kujibu mapigo.
Kuanzia sasa angalia ID za wachangiaji wa hoja za CUF/Lwakatare nyingi zitakuwa ngeni na mpya.
1. ......Majungu ambayo matokeo yake ni wazi kabisa kwamba watakuja gawana kura..Na wakija gawana kura kati ya CUF na Chadema basi bila shaka mnafahamu mshindi nani hapa!
Mchukia Fisadi said:Amekili kuwa yeye ni muumini wa ushirikiano ......... na siri anayo kwa nini haikuwezekana.
*Amesema si lazima tu yeye peke yake ndiye awe mgombea katika jimbo hili la Bukoba ....... Lakini anasema yuko tayari kushirikiana na mgombea yeyote na kumpigia kampeni kama atakuwa anakubalika hata kama atakuwa ametoka katika chama chake cha zamani Kafu.
Mkandala said:Navyojua mjini Bukoba, kwa hesabu kubwa unajengwa na Waislaam ambao kutokana na hizi hisia za Udini kuingia kati ya swala hili, sidhani kama Lwakatare atakuwa na mvuto mkubwa kwa waislaam isipokuwa Wakristu
Omutwale said:Wale wenye msimamo mkali wa kidini (mimi simo) wameanzisha uvumi kuwa Maaskofu ndiyo waliomshauri Lwakatare atoke CUF na kwenda CHADEMA kwa ahadi ya kumpigia debe 2010. (Hii nitaelezea siku zijazo kampeni ya namna hii zinaweza kula kwa nani na kwa sababu gani)
Nimefuatilia sana matukio yote haya na kama kawaida yangu najaribu sana kutazama upande wa pili kinyume cha Picha nzima inayotembea sasa hivi..
Pia kwa sababu nina marafiki na jamaa zangu wa karibu huko BK, mji ambao nimewahi kukaa ingawa sii muda mrefu miaka 80's baada ya vita nadhani pia mchango wangu unaweza kuwapa picha kamili ya huu upande ambao wewngi wetu tunashindwa au tunapuuza kuutazama..
Ni katika reality exploration zangu, nimekuwa mgumu kukubaliana na mawazo ya wengi kuhusiana na swala zima la Lwakatare kuhamia Chadema...Inanitisha zaidi ya kufurahia kutokana na sababu mbili muhimu ambazo zinatandika wingu zito kwa wakazi wa Bukoba mjini..
1. kwanza, kuhama kwake kunazua majungu makubwa kati ya vyama ambavyo vilikuwa chanzo cha muungano wa vyama vya Upinzani..Majungu ambayo matokeo yake ni wazi kabisa kwamba watakuja gawana kura..Na wakija gawana kura kati ya CUF na Chadema basi bila shaka mnafahamu mshindi nani hapa!
2. Sababu za kuhama ambazo zinazotembea mjini zinahusu zaidi UDINI.. Yaani sababu kubwa ya Lwakatare kuondoka/kuondolewa CUF na kupokelewa Chadema ni kwa sababu ya dini yake... Hii ni sumu kubwa ktk maendeleo ya vyama vyote hivi viwili..Tujihadhali sana na mtazamo huu kwa wananchi.
Navyojua mjini Bukoba, kwa hesabu kubwa unajengwa na Waislaam ambao kutokana na hizi hisia za Udini kuingia kati ya swala hili, sidhani kama Lwakatare atakuwa na mvuto mkubwa kwa waislaam isipokuwa Wakristu ambao kwa taarifa nilizozipata wapo wengi wamehamia mjini hivyo kuufanya mji wa Bukoba kuwa na mchanganyiko mkubwa.Hivyo basi, sidhani kama kuna matunda ktk jambo hilim pande zote mbili kukubali kuachia uvumi huu ukitembea ovyo!
Kutokana na sababu hizi mbili naogopa sana kinachokuja huko mbele ya safari pamoja na kwamba Wahaya umoja na muungano wa jamii zao haufuati sana dini..lakini kama kutatokea kichochezi kama hiki cha fitna na tenguzi, nachelea kusema makosa makubwa yamefanyika toka Uongozi wa pande hizi mbili.
Unaweza kutokubaliana nami lakini haya ni mawazo yangu ambayo yametokana na hisia zilizoambatana na tetesi nilizozipata. Ushauri wangu nadhani ungekuwa kwamba kabla ya Lwakatare hajahamia CVhadema viongozi wa pande hizi mbili wangekutana na kuzungumiza swala hili kiundani zaidi wakizingatia umuhimu wa muafaka walioujenga..Kuzuka kwa fitna na uhasama kati ya vyama hivi na hasa UDINI ukitumiwa kuwa kiamsho cha fikra za Lwakatare kunanipa wasiwasi mkubwa sana hata kama yeye anafahamu fika kuwa vitu hivi havihusiani..
Nitawaomba viongozi wa Chadema na CUF kukaa kitako kueleishana kilichotokea na kujaribu kuondoa wingu hili kubwa linalozidi kutanda mjini Bukoba na hasa Uswahilini..Sintapenda kuona kura za wanachi zikitazama kwanza dini ya mhusika au ushindani utokane na dini zao kwani wananchi watakuwa hawatumii tena akili zao kufikiri uwezo wa mhusika Kisiasa. Kura zitagawanywa kulingana na dini za waumini jambo ambalo ni hatari sana kwa vyama vyote hivi viwili..
Mkuu,Mchukia Ufisadi,
Mkuu hivi tetesi za Bongo unazifahamu ama unazungumza tu ili mradi kulainisha watu..
Ushahidi gani unaoutaka wewe ikiwa Lwakatare ni mkristu amehama chama ambacho kinadaiwa kuwa ni cha Waislaam..Lwakatare mwenyewe ndio wanamchukulia kuwa sababu mkuu wangu..Ebu kwanza fikiria uzito wa tetesi hizi ktk akili za mlalahoi. Unafikiri watu watasubiri ushahidi unaotaka wewe?..
Nimesema hizi ni tetesi na sumu ya maendeleo ya vyama vyote hivi viwili kwani wananchi wataanza kuamini na wakisha amini huwezi kuwambia CUF sii chama cha Waislaam au Chdema sii chama cha wakristu..
Inachukua muda mfupi sana kwa Wadanganyika kuamini haya..Na nakuhakikishia asilimia 90 ya Wakristu wanaamini CUF ni chama cha Waislaam/Wapemba kutokana na kampeni ya CCM kukidondosha chama hicho baada ya uchaguzi wa mwaka 2000..Kufikia uchaguzi wa mwaka 2005, CUF Kushnehi! na umeona watu humu kibao wakitoa hoja zao wakiamini kabisa kwamba CUF ni chama cha waislaam...CCM hawakutoa ushahidi wowote wala hawakuwa na haja ya kufanya hivyo.. kwani Ndivyo Tulivyo!
Ushahidi hakuna zaidi ya sisi wenyewe kuona dini za watu (wakazi wa Pwani) wanaokipa support chama hicho..
It's just a wake up call mkuu wangu.
*Amekili kuipenda sana kafu hadi kumiliki kadi namba 149 ya mwaka 1991lakini anasema anaipenda nchi yake sana kuliko vyama vya siasa.
*Amesema ameamua kuwa muandishi na kuna kitabu anachoandika ingawa kakili anahitaji msaada ili akichapishe, ambapo alipata ahadi ya sh laki 3 toka kwa Dr Slaa, laki 2 toka kwa Baregu, 250,000 toka Balozi Ngaiza nk nk nk.
*Amesema mipango yake anayofikiria kuianzisha sasa ni kujenga chuo cha Technologia hapa Bukoba, ili kuhakikisha vijana wengi wanapata mafunzo ya namna ya kujiajili mara wamalizapo shule.
*Katangaza kuwakutakuwa na party ya kumpongeza itakayokuwa katika hotel ya Spice Bukoba.
*Amekili kuwa yeye ni muumini wa ushirikiano katika vyama vya upinzani, na amewahi kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa vyama vinne vya upinzani ulioundwa ili kutafuata namna vyama vinavyoweza kushirikiana katika masuala ya uchaguzi na siri anayo kwa nini haikuwezekana.
*Amesema si lazima tu yeye peke yake ndiye awe mgombe katika jimbo hili la Bukoba mjini maana hajui kama chake kitamteua wakati ukifika. Lakini anasema yuko tayari kushirikiana na mgombea yeyote na kumpigia kampeni kama atakuwa anakubalika hata kama atakuwa ametoka katika chama chake cha zamani Kafu.
*Na kwa sababu hiyo ameamua kujikita hapa Bukoba na kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa upinzani unashinda na kuchukua council na hatimaye ubunge kwa mbunge yeyote wa upinzani anayekubali. Ameapa kufanya kila jitihada kuona anatimiza aima yake hiyo.
*Amesema sasa anahitaji wanachama walio hai katika chama na si kundi la ushabiki tu. Hao wawe na kadi kadi zakupigia kura wafahamike waliko, waorodheshwe katika daftari la chama, wajulikame simu zao au hata email zao.
sio kweli mimi nipo jf toka 2007 acha uongo na mjadala huu wa lwekatare ni mimi niliyeuleta hapa.wana jf,
rejea thread yangu yenye title:
Inapatikana hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...are-wa-cuf-kuhamia-chadema-17.html#post495735
nilitoa taarifa ifuatayo:
Nikamalizia hivi:
Sasa angalia id ya bw. Ukoko alafu tafakari. Haja ya kutoa taarifa kwenye suala hili haihitajiki kwa mtu atakayepata mantiki toka hapo juu. Assume unaangalia tangazo la haki elimu, si kila kitu wanakutafunia. Simply, ...... At work!
Eni wei, najua wengine itawauma, ila ukweli kadi zimerejeshwa na kununuliwa kama vocha za tigo.
Bandugu naomba mie nijipe likizo kidogo maana nimechoka ile mbaya. Toka mida ile nahudumia mramba na rubisi.
nimefuatilia sana matukio yote haya na kama kawaida yangu najaribu sana kutazama upande wa pili kinyume cha picha nzima inayotembea sasa hivi..
Pia kwa sababu nina marafiki na jamaa zangu wa karibu huko bk, mji ambao nimewahi kukaa ingawa sii muda mrefu miaka 80's baada ya vita nadhani pia mchango wangu unaweza kuwapa picha kamili ya huu upande ambao wewngi wetu tunashindwa au tunapuuza kuutazama..
Ni katika reality exploration zangu, nimekuwa mgumu kukubaliana na mawazo ya wengi kuhusiana na swala zima la lwakatare kuhamia chadema...inanitisha zaidi ya kufurahia kutokana na sababu mbili muhimu ambazo zinatandika wingu zito kwa wakazi wa bukoba mjini..
1. Kwanza, kuhama kwake kunazua majungu makubwa kati ya vyama ambavyo vilikuwa chanzo cha muungano wa vyama vya upinzani..majungu ambayo matokeo yake ni wazi kabisa kwamba watakuja gawana kura..na wakija gawana kura kati ya cuf na chadema basi bila shaka mnafahamu mshindi nani hapa!
2. Sababu za kuhama ambazo zinazotembea mjini zinahusu zaidi udini.. Yaani sababu kubwa ya lwakatare kuondoka/kuondolewa cuf na kupokelewa chadema ni kwa sababu ya dini yake... Hii ni sumu kubwa ktk maendeleo ya vyama vyote hivi viwili..tujihadhali sana na mtazamo huu kwa wananchi.
Navyojua mjini bukoba, kwa hesabu kubwa unajengwa na waislaam ambao kutokana na hizi hisia za udini kuingia kati ya swala hili, sidhani kama lwakatare atakuwa na mvuto mkubwa kwa waislaam isipokuwa wakristu ambao kwa taarifa nilizozipata wapo wengi wamehamia mjini hivyo kuufanya mji wa bukoba kuwa na mchanganyiko mkubwa.hivyo basi, sidhani kama kuna matunda ktk jambo hilim pande zote mbili kukubali kuachia uvumi huu ukitembea ovyo!
Kutokana na sababu hizi mbili naogopa sana kinachokuja huko mbele ya safari pamoja na kwamba wahaya umoja na muungano wa jamii zao haufuati sana dini..lakini kama kutatokea kichochezi kama hiki cha fitna na tenguzi, nachelea kusema makosa makubwa yamefanyika toka uongozi wa pande hizi mbili.
Unaweza kutokubaliana nami lakini haya ni mawazo yangu ambayo yametokana na hisia zilizoambatana na tetesi nilizozipata. Ushauri wangu nadhani ungekuwa kwamba kabla ya lwakatare hajahamia cvhadema viongozi wa pande hizi mbili wangekutana na kuzungumiza swala hili kiundani zaidi wakizingatia umuhimu wa muafaka walioujenga..kuzuka kwa fitna na uhasama kati ya vyama hivi na hasa udini ukitumiwa kuwa kiamsho cha fikra za lwakatare kunanipa wasiwasi mkubwa sana hata kama yeye anafahamu fika kuwa vitu hivi havihusiani..
Nitawaomba viongozi wa chadema na cuf kukaa kitako kueleishana kilichotokea na kujaribu kuondoa wingu hili kubwa linalozidi kutanda mjini bukoba na hasa uswahilini..sintapenda kuona kura za wanachi zikitazama kwanza dini ya mhusika au ushindani utokane na dini zao kwani wananchi watakuwa hawatumii tena akili zao kufikiri uwezo wa mhusika kisiasa. Kura zitagawanywa kulingana na dini za waumini jambo ambalo ni hatari sana kwa vyama vyote hivi viwili..
sio kweli mimi nipo jf toka 2007 acha uongo na mjadala huu wa lwekatare ni mimi niliyeuleta hapa.
Bw.Ukoko said:Lwakatare ahamia rasmi chadema na kudai CUF walikuwa wakimlipa sh 300,000 tu kwa mwez
Wakuu.
Leo katika pita pita zangu katika Mkoa wa Kager kikazi nimejikuta navutika kuudhuri mkutano wa CHADEMA uliolenga kumpatia Lwakatare kadi mpya ya chma hicho.
Kikukubwa hapa ni kwamba Lwakatare amesema kuwa alipokuwa n cheo ndani ya CUF alikuwa akilipwa sh 300,000 kwa mwezi hivyo amewaomba wananchi waone ni jinsi gani alivyokuwa anafanya kazi nyingi na kulipwa kiduchu.
Sasa angali hapa:
Bw.Ukoko
Bw.Ukoko has no status.
Junior Member
Join Date: Fri Jun 2009
Posts: 2
Thanks: 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Rep Power: 0
Credits: 5,585
Safi sana.
Swali langu ni, hivi Bw. Ukoko ndiye kanda2?
Bw. Ukoko ndiye aliandika yaliyorejewa hapo juu. Nami nilikuwa namzungumzia huyo huyo. Yawezekana Bw.Ukoko = kanda2 lakini si mwangalifu. Kisha soma profile ya Bw.Ukoko hapo kwenye attachment na mwisho amua mwenyewe.
Sisi wote tunashangaa sana sana katika hili maana huwa. Kila mtu ana haki ya kujiunga na vyama, but wale walikwenda upinzania kwa ajili ya ulaji warudi haraka CCM
ni kweli amejiunga na chama kabla ya kusoma katiba na sera za chama na soon baada ya kujiunga kapitisha bakuli la njaa. Inatia aibu sana.njaa za viongozi wetu wala hatutashangaa sana
Kwa hiyo wewe ndio Mchukia ufisadi = Lwekatare.
sababu anayejadiliwa Lwekatare wewe unajibu tena unaongea hadi kihaya.
kwani maoni yako huko juu ulisema kuwa wana CUF wameambiwa waje kwa wengi kujiunga JF na ukatoa mfano wa ukoko. kwa vile ulisema kwa ujumla ndio nikakujibu.ila ujue kuwa mimi member hapa toka 2007 kabla ya wewe kuja kujiunga 2008 mwishoni.
nina michango mingi zaidi ya 400.wewe una posts 99 tu tena asilimia 70 za Lwekatare.hivyo nazidi kuamini wewe=Mchukia Ufisadi ambaye ndiye Lwekatare.