Pamoja na kwamba sioni sababu ya ku-question nia yake ambayo ameitimiza kwa kuhamia chama kingine, naona haikuwa vyema kwake kusema alikuwa akilipwa kiasi gani na CUF. Masuala ya mshahara ni makubaliano yake na chama alichokuwepo. Na ni masualaya kibinafsi sana. Kinachotakiwa ni sababu za kuhama, na kuhamia CHADEMA, nia ya kuendeleza upinzani wa kidemokrasia na mikakati aliyonayo ya kisiasa baada ya kuondoka CUF.
Kuweza kupata wanachama wa CUF wenye nia ya kuhama nae ni hatua muhimu sana pia. Kwani anaingiza mtaji mpya kwenye chama chake kipya. Ila anatakiwa kuahidi kushirikiana na chama chake kipya na kujifunza imani zao, malengo yao na kupania kukiimarisha zaidi kwa kushirikiana na wenzake aliowakuta huko.
Siasa za upinzani Tanzania ni ngumu sana. Inabidi tumuelewe tu ndugu yetu huyo kwamba amebidi kuhama na zaidi ametumia haki yake kufanya hivyo. Tuheshimu maamuzi hayo, kwani kufanya hivyo ni kumtendea haki. Hakuna haja ya mtu kubaki sehemu moja ambayo una uhakika kuwa hutaweza kutoa mchango wowote kwa haki, na uhuru. Hasa baada ya kutokea yaliyotokea.
Kila binadamu hupenda challenges. Bila challenges maisha yanakuwa boring. Hivyo kuhama kwa Lwakatare inaweza kuwa ni challenge kwake, ni kwa manufaa yake kabla hayajawa manufaa kwa mwingine yeyote.
Wasiliana na viongozi wa Chadema kama na wewe unahitaji kujiunga kuwa mwanachama. Watakupa maelekezo😀Ebo! Fujo zote hizi kumb mtu hata fomu za maombi ya uanachama hajajaza! Mimi nilifikiria kuwa wakuu walikuwa wanaenda kumkabidhi kadi baada ya kukubaliwa maombi yake ya uanachama! Iko kazi.
P.S. Hivi hizo fomu MAALUM za maombi zikoje? Zina tofauti gani za zile za kawaida?
Amandla.......
Wasiliana na viongozi wa Chadema kama na wewe unahitaji kujiunga kuwa mwanachama. Watakupa maelekezo😀
Watu wengine wa ajabu sana. Is this spinning?I love CHADEMA..... wanakwenda kisasa zaidi. Kuweza kuajiri watu 24/7 kushinda mtandaoni na kufanya spinning.. is not a joke!
Omutwale hongera amakweli unakula kwa jasho lako, maana kwa propaganda! utadhani ulipitia pale Kivukoni?
*Anasema alipata kadi ya kafu mwaka 91 katika tawi la Kibeta wakati huo akiwa mtumishi wa serikali, na hata famila yake ililidhia. Na aliona vigumu kuwakubalia watu hadi awasiliane na famila yake.
*Anasema alipata maswali mengi na kikwazo kikubwa kilikuwa kwa baba yake mzazi ambaye alihofia hatima ya usalama wa mwanae kisiasa na hata katika maisha ya kisiasa.
Baada ya kupata ushauri toka kwa wazee fulani alikubaliana na utashi wa wananchi wa Bukoba mjini kwamba anaweza kuhama.
*Alisisitiza aliamua kuchukua hatua zote hizo maana yeye si mwanasiasa sawa na wale wanasiasa ambao uamua tu kwenda Maelezo na kuita waandishi wa habari kutangaza kuamia chama kingine bila kutafakari. Wala yeye hakushauriwa na viongozi wa Chadema kuhamia huko, na si kweli kwamba amepewa rushwa kama wengine wanavyovumisha, maana yeye si mla rushwa. Bali alitaka kuheshimu matakwa ya wapiga kura wake.
Alisisitiza kuwa yeye hakuumbwa kunyamazia kitu kibaya kinapotokea na huwa tayari kujitoa kukieleza wazi maana hiyo ndivyo alivyo katika maisha yake.
*Anasema alikuwa anapata mshahara wa sh. laki 3 alipokuwa kafu kama kaimu katibu mkuu, na anasema uamuzi wa kumuondoa katika wadhifa kwa ghafla ulimfanya afikiri kuanza ujasiliamali na alianza kuuza Matikiti maji na Chips kuku. Na amebainisha kwamba kwa mwezi kwa kuuza matikiti maji alipata faida ya sh. laki 2 na chips laki 3.
*Alisema kwa sasa tunahitaji kujenga misingi ya vyama na si ushabiki wa vyama na kuwaasa wanachi wa Bukoba kulielewa hilo.
*Aliomba iwekwe detector ya kubaini wale watu wanaokwenda katika vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, dini au ukabila. Maana hayo uua vyama badala ya kuvijenga.
Wait a minute plz Kandambili, usianze kulialia 😀KWENYE barua zake alizoweka hapa JF alionekana anatafuta mtu wa kumpa pesa za wakili na kumsaidia gari nk.Chadema lazima watakuwa wamekubali kuchukua gharama zake.alikuwa kama anajitembeza yaani kibaya chajitembeza na kizuri cha jiuza.kwani barua zile za chama chake kuziweka kwenye mtandao ni kinyume na maadili ya uongozi.wenzake CUF hawajatoa siri zake
😀 umenichekesha sanaDuh..huyo jamaa aliyepiga sun glasses ndo 'security detail' ya Chadema?