Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Wanasahau kuwa CUF ni kama daladala, akishuka abiria mmoja wengine kumi wana'nga'ngania mlango.Libeneke kama kawa.
 

Kitila kazungumza hoja nzito na post yake ilikuwa inaonyesha kiwango chake kikubwa cha elimu.
Angalia sasa post za wale waliolewa maji ya kijani uone, utaona tofauti hata ya vyama hivi viwili, na utajua kwa nini nchi yetu iko hivi ilivyo......
 
Ndugu yangu Fundi Mchundo, kumbuka mtu anapokuwa kiongozi anatakiwa kwanza awe mvumilivu, lakini pia anatkiwa awe makini na kauli zake anazozitoa maana kiongozi mwenye hadhi ya kuitwa Mhe Mbunge ana nadhamana kubwa kwa wananchi anaowawakilisha na watanzania wote kwa ujumla wake.

Sasa anaposimama na kusema Waziri majibu yake ni ya hovyo hovyo inatutia shaka,alipotamka mara ya kwanza ilichukuliwa kuwa ameteleza.

Lakini hata pale alipotakiwa afute kauli hiyo bado alisisitiza kauli yake hiyo ina maana kuwa alikuwa amekusudia.

Mwisho naomba nikushauri kuwa nduguyo anapokosea msaidie faini na siyo kesi.
 
Hapa mtasema mengi amabayo hayakuwahi kutoka midomoni mwenu, lakini Lwaks huyooooooooooooooo chadema. Mnayodhani kuwa yatakuwa maafa kumbe itakuwa baraka.
Ndege(Lwaks) katua CCM No.2 sasa, on his way to CCM No.1 tusiandikie mate.
 

Aisee Nziku hiyo bottoline yako imenichekesha saaaaaana...
 

Marwa post yako ina ukweli mkubwa sana na si biased kama nyingi hapa zilivyo.
Ila tu napenda niweke wazi kuwa kafu itaendelea kuwapo Zanzibar tena zaidi Pemba lakini bara itaungana na vile vyama vingine si unajua? nncr,tlp,udp,dp na ww ongeza orodha hapo. Vipo kama havipo vile.
 
Ukimnyooshea mwenzio kidole kimoja, vinne vinakugeukia wewe, Si afadhai hata huyo Zitto kathubutu? wewe je? nyuma ya keyboard?

Bravo Zitto, songa mbele wala usirudi nyuma!

kathubutu kufanya nin?kutetea ununuzi wa mitambo ya dowans KWA NGUVU ZAKE ZOTE,KWA UWEZO WAKE WOTE,NA KWA AKILI YAKE YOTE?
..........nah!hainiingii akilini kabisa!lazima alitangaza njaa hapa

mwanasiasa wa kiwango chake akishaprove failures to that level,AACHIE NGAZI!uongozi,au siasa watu hawazaliwi navyo bwana

.........huyu chuo-mate wangu nae ALIONYESHA UDHAIFU MKUU,aliamua kuondoka ccm baada ya jina lake kutopita katika kuwania ubunge kule tarime,UROHO WA MADARAKA?AU NJAA?HUYU SI MWANASIASA!na bahati mbaya i knw him IN-OUT
 
 
Kuhama toka CUF kwenda CHADEMA ni sawa na kubadilisha kiti kwenye basi la kusafiria.
 
Last edited:
Wakuu kwa habari kamili niliyo nayo Lwakatare bado anamiliki uanachama wa kafu hadi ijumaa ya wiki hii.
Stay tuned kujua nini kitatokea ijumaa huko Bukoba.
Nasubiri kupata info zaidi na nitawahabarisha.
Junius nawe utakuwepo huko Bukoba na Lipumba? Nasikia kuna bonge la party ya wana kafu Bukoba siku hiyo ya ijumaa😀 Sijui ameamua kuvunja kimya?
 
Ijumaa kuna jambo litatokea huko Bukoba kuhusu sakata hili.
Stay tuned.............
 
Kama Chadema wakitoa mwaliko hapana shaka.
 

Inaonekana pasipo shaka kabisa kwamba unachuki binafsi na Bw. Mwikwabe.Kama sivyo wewe utakuwa mshirika/mwanachama wa chama cha mafisadi, manake mlikereka sana kwa bw.Mwikwabe kuwatosa na kujiunga Chadema. Hapa tunazungumza habari ya Lwakatare kuihama CUF na kujiunga Chadema lakini wewe uko busy kumshambulia bw.Mwikwabe.
Kwani wangapi wamesoma na bw.Mwikwabe na walikuwa karibu zaidi nayew kuliko wewe lakini mbona hawasemi.Watu kama wewe sitashangaa kukuta kuwa hata UDSM hamkupenda awe rais na mlikuwa upande wa mpinzani wake kwahiyo mna wivu wa kijinga, tena hadi leo hii takribani miaka minne baada ya kutoka UDSM una mawazo ya kijima namna hiyo.
Kama una hoja juu ya Mwikwabe anzisha thread tukupe mambo sio kuanza kulia lia hapa eti unamjua in and out, upuuzi mtupu!!!Chuki zenu zimezidi baada ya kushindwa kulirudisha jimbo la tarime kwa chama cha mafisadi. Fungua akili yako kwa upana zaidi ndg yangu usiifungie akili yako ndani ya
box mwisho wake ni kuanza kushambulia watu kwa vioja badala ya kuleta hoja.
 
Fundi,
Huo mvuto wa Lwakatare hakuja nao CUF bali aliupata CUF.

Kuna utofauti kati ya Mwanafunzi aliyeko Lab na yule aliyeko class. Aliye class ataweza kujifunza na kusoma nadharia ilihali aliyeko Lab anaweza kuona matokeo ya nadharia kwa vitendo.

Unalolisema Bw. Masatu ni sawa na aliyeko sebuleni kubishana na mpishi juu ya chakula kuiva. Mpishi anasema chakula bado, aliye sebuleni anasema kimeiva, pakua.

Tuliokuwepo wakati mageuzi na vyama vinaingia hapa BK tunatambua kuwa CUF ni Lwakatare but vice versa is true not! Selestine Mutakyawa ni NCCR-Mageuzi lakini NCCR-Mageuzi siyo Selestine Mutakyawa.

Ni jambo la kawaida kabisa kwa Watwale mtu kuwa icon ya industry. Katika medani za kisiasa BK, Lwakatare ni selling Brand yeye kama Lwakatare na si kama Chama.

Thibitisha haya niliyoyaandika kwa kuangalia njugu za kadi za CUF zitakazorejeshwa kesho.

Masatu, Kuna ka-PM nakutumia
 
Prof wa Pumba akiwa kazini!


Acha ulimbukeni, upumbavu na ushenzi wako. Kama Lipumba anaweza kuwa prof wa Pumba wewe utakuwa profesa wa kinyesi! Unadhani u profesa unapatikana kwa kuandika JF.
 

Lipumba ni Profesa wa Pumba kweli si uongo. kama kashindwa kukipeleka chama kisomi, sasa tumsemeje?
Arudi darasani kufundisha pumba zake.
 

Nafikiri sumu waliyoipandikiza chama cha kijani kwamba CUF ni chama cha kidini, hivyo inakuwa ngumu kidogo watu hao kujiunga na CUF waona may be hawato shine hasa hasa huku bara.Na kwa kundoka huyo jamaa(Lwakatare) ambae kidogo alikuwa anaondoa dhana hiyo kama alivyosema member mmoja ndio utakuwa msumari wa mwisho wa CCM na sumu yao kwa CUF.CUF watanyooshewa kidole mpaka.Yangu macho ngoja nivue na miwani yangu.
 
Acha ulimbukeni, upumbavu na ushenzi wako. Kama Lipumba anaweza kuwa prof wa Pumba wewe utakuwa profesa wa kinyesi! Unadhani u profesa unapatikana kwa kuandika JF.

Heeeh....yashakuwa hayo tena?
 
Aliingia chama ambacho hakikuwa size yake.....aende chadema akapige jembe la maendeleo ya demokrasia....aachane na unafiki na fitna hataziweza......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…