LWAKATARE: Kuna unafiki CHADEMA

LWAKATARE: Kuna unafiki CHADEMA

Alikumbana na unafiki CCM AKAHAMA, akaenda CUF akakumbana tena na unafiki AKAHAMA, akaenda CHADEMA, amekumbana na UNAFIKI, HATAKI KUHAMA!!.

Kama ni unafiki uliokuwa unamfanya ahame, kwa nini asihame tena CHADEMA?.

Maelezo yake yanaonyesha yeye ndiye CHANZO cha unafiki au ndiye mchochea unafiki kwa sababu haiwezekani yeye tu anayeona unafiki kila kule kwenye chama anakohamia.

Kikubwa zaidi, hizi anazozisema ni kauli tu za kisiasa lakini kinachomwongoza zaidi ni fikra kwanza za tumbo lake. Kama siyo fikra za tumbo lake, kwa nini hajahamia kwenye chama ambacho hakina mtaji wa kisiasa Tanzania?. I'm sorry, kwa nini asihamie kwenye vyama vya siasa vyenye debe tupu la kisiasa kama NLD, DP,TADEA,UPDP, n.k.

Kwani hafahamu kama Kufa kufaana!. Wenzake kwa sasa wanapiga mahesabu na kumuomba shetani kesi inayomkabili imkabe hasa ili wakipate cheo chake na pia nafasi ya ugombea ubunge Kagera 2015. This is politics.
 
magazeti yote hayakuinyaka hiyo story ila FAHAMU, wajinga ndio waliwao
 
Fahamu ni gazeti la CUF na Mhariri ni Mtatiro sasa unategemea liandike vipi?

CUF = CCM (FAHAMU=UHURU)
kwa hiyo walichonadika ni sawa
 
Kwanini hilo gazeti liandike hiyo habari wiki moja baadaye? Balile kazini. Angalizo: mikutano hurekodiwa, si busara kutengeneza rekodi ya kwako!
 
hii habari wewe na ilo gazeti mmeitafasiri kikudakudaa serukamba u atuondoi tension yetu kwenye mabomu arusha
 
gazeti matatizo matupu...magamba mmeshikwa pabaya lazima mtang'oka tu.
 
Kama lwakatare kaligundua hilo awataje hao wanafiki tuwajue,funguka lwakatare .
 
Safari hii naona kama ndiyo kwanza inaanza kileo naye akitoka au akifungwa tutaendelea kusikia mingi.
 
CHADEMA inapambana na maadui wengi, hata unafiki nao ni adui mkubwa. Ila ataonyeshwa hadarani punde
 
Anayoyaongea Lwakatare nakubaliana nayo kabisa. Ndani ya Uongozi wa juu wa CHADEMA kuna matatizo pia.

Sisi kama Watanzania tuliochoshwa na Utawala wa Chama Tawala cha CCM na tunaoipigania CHADEMA kwa kila hali tungependa kuona Uongozi makini. Wenye kujali demokrasia na unaothamini siasa za kuvumiliana ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima na hatimaye kufukuzana. CHADEMA kama Taasisi inaundwa na Wanachama, Viongozi, Makada na Wapenzi wenye mitizamo na maono tofauti ya kisiasa.

Tujenge utamaduni wa kuelewana hata pale tunapotofautiana kimawazo,Haijalishi kama misimamo yetu pia inapingana na ya Uongozi wa Chama. Ila tuchukuliwe kama ni watu ambao lengo letu na wale wanaounga mkono baadhi ya Viongozi wa Chama kwa jambo lolote lile kuwa siku zote ni moja tu; Nalo kuijenga CHADEMA kuwa Chama imara na tishio zaidi kwa Chama Tawala. Haya mambo kukataa kutofautiana tuwaachie CCM.

Si tunawaona na namna wanavyowapiga vita Wanachama na Makada wanaopingana na mienendo ya Viongozi wa Chama na Serikali yao? Tusiwe kama Mafisadi wa CCM
 
Mi sioni kosa kama kilichoandikwa ndicho alichosema Lwakatare. wana CDM si Mungu ni binadamu kama wengine. muhimu unafiki hautakiwi CDM bali Ukweli
Hawa wanasiaasa
wanatuchanganya sana.

Sasa kama alishazungumza na Mbowe kuhusu unafiki ndani ya chama, kwanini
aende kulizungumzia hilo tena kwenye mkutano wa hadhara? Au viongozi wa
juu wa chama hawaelewani?

Kweli, kufikia ukombozi wa kweli ni mission.

CHADEMA imekuwa kama serikali ya CCM, viongozi wa juu wote chamani
wanalalamika; Zitto analalamika, Lwakatare analalamika! Sasa nani
atachukua hatua?
 
Authenticity ya gazeti ni muhimu sana ili kufanya analysis!
 
Back
Top Bottom