Lwakatare ataichafua Tanzania

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,192
25,493
Makosa ya ugaidi aliyoshtakiwa Alfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph yanaweza kuichafua nchi kimataifa.

Kwa mawazo yangu,makosa ya ugaidi ni makosa 'sensitive' na hivyo kuvuta hisia za mataifa ya nje yakiwemo ya America na Ulaya. Nijuavyo mimi, hii ni mara ya kwanza tangu sheria ya kuzuia ugaidi ilipoundwa na Bunge mwaka 2002 kwa mtanzania kushtakiwa kwa ugaidi hapa nchini. Tanzania tuna magaidi na ugaidi!?

Nionavyo, hata utalii na uwekezaji utapungua kwakuwa watalii na wawekezaji wengi wataiona Tanzania nchi isiyo na usalama sana na hivyo kuwatisha wawekezaji na watalii hao. Mashtaka ya Lwakatare na mwenzake yanaweza kuleta taswira mpya toka ile ya Tanzania yenye amani na utulivu hasa kimataifa.

Tufanye mambo yetu tukiwa tayari kupokea madhara na matokeo ya masuala hayo.

Muhimu: Haya ni maoni na mawazo yangu binafsi kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977(kama inavyorekebishwa mara kwa mara)
 
Kwa akili fupi wanadhani mataifa ya ulaya yataangalia Lwakatare ni nani na anatoka chama gani! Ukweli ni kuwa watu watajadili je hayo makosa kweli ni ya ugaidi au ni upuuzi na kutuona sote ni wapuuzi!

DPP ndiyo ataiyeifanza Tanzania tuonekane ni wapuuzi.
 
Hii kesi yote ikidakwa na Reuters na wenzake itachafua Tanzania. Na mbaya zaidi, inakuja kipindi ambacho Tanzania imeomba msaada ya FBI.
 
Halafu unasikia mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa CCM anasema vijana msishabikie wanaoisema nchi vibaya.Hillarious indeed!
 
Unatumia makalio kufikiri! Hivi kuna kitu kimechafua Tanzania kuzidi maamuzi ya utawala uliopo madarakani?

Nafikiri ungemsoma vizuri mtoa mada ungemuelewa, manake hapa naona na wewe umemuunga mkono japo hujaelewa. Mimi nilivyomuelewa mtoa mada hapa anaishushia lawama serikali na vyombo vyake kwa kuipaka matope nchi. anasisitiza kwamba kumfungulia mtu mashtaka ya ugaidi kutaiweka nchi pabaya katika ramani ya dunia. kwahiyo hapa moja kwa moja anaulaumu utawala uliopo madarakani which is right pia according to your post.
 
Kilichoichafua Tanzania ni
  • Kuuawa kwa mwandishi,
  • Kuuawa kwa viongozi wa dini,
  • Kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi
  • Kutekwa na kuteswa kwa mwandishi mwingine
  • Kumwagiwa sumu watu mbalimbali au kuumizwa na vitu vyenye ncha kali
  • Uchochezi mbalimbali unaoendelea, na
  • Maovu mengine dhidi ya binadamu
 
Kwa kuwa kiongozi wa Chadema anahusika na ugaidi ndio unataka Mahakama isimhukumu kwa ugaidi aliopanga kuufanya? ili kujipendekeza kwa watalii? hivi ulisoma shule wewe? sheria ya ugaidi ilipitishwa na Bunge na kama kuna magaidi wacha sheria ichukue mkondo wake! mbona Waziri Nchimbi aliposema Zanzibar kuna ugaidi mlifurahia? Zanzibar mnakiri kuna magaidi lakini wa kutoka bara mnataka wafichwe au washtakiwe kama majambazi! uhasidi na chuki ni vitu hatari sana!
 
Cha msingi haki itendeke.

Hayo mambo ya kuichafua nchi hayapaswi kuwa kizingiti cha haki kutendeka.

Kwani nchi gani hakuna ugaidi mpaka itunyooshee kidole. Labda Vatican peke yake ndio hakuna ugaidi.
 
Atachafuliwa Lwakatare na cdm pekeyao!

kwa akili zako fupi na fikra zilizoja utando wa utumwa unaweza kuona mwisho wa pua yako. Jaribu kutumia darubini uone mbali ndipo utakapojua kuwa jeshi lenu la policcm pamoja na DPP wao ndo wamejichafua kwa kujipaka kinyesi chao wenyewe. Ndio maana mpaka sasa wanacheza mchezo wa kuigiza (enzi zetu tulikuwa na vituko RTD vya pwagu na pwaguzi). Wanafanya mambo ya kitoto kwenye jambo ambalo ni kubwa na linalotazamwa sio tu na watanzania bali pia jamii ya kimataifa. Kwahiyo aibu hii itaiangukia serikali na tutazidi kuchekwa.
 
Kwa kuwa kiongozi wa Chadema anahusika na ugaidi ndio unataka Mahakama isimhukumu kwa ugaidi aliopanga kuufanya? ili kujipendekeza kwa watalii? hivi ulisoma shule wewe? sheria ya ugaidi ilipitishwa na Bunge na kama kuna magaidi wacha sheria ichukue mkondo wake! mbona Waziri Nchimbi aliposema Zanzibar kuna ugaidi mlifurahia? Zanzibar mnakiri kuna magaidi lakini wa kutoka bara mnataka wafichwe au washtakiwe kama majambazi! uhasidi na chuki ni vitu hatari sana!
Kuna haja ya kuelewa vizuri maana ya ugaidi maana naona kila mtu anaimba ugaidi bila kuelewa tafsiri yake halisi.
 
The term "terrorism" comes from French terrorisme , from Latin :
'terror' , "great fear", "dread", related to the Latin verb terrere , "to frighten".

The terror cimbricus was a panic and state of emergency in Rome in response to the approach of warriors of the Cimbri tribe in
105BC. The French National Convention declared in September 1793 that "terror is the order of the day". The period 1793–94 is referred to as La Terreur (Reign of Terror).

Maximilien Robespierre, a leader in the French revolution proclaimed in 1794 that "Terror is nothing other than justice, prompt, severe,
inflexible." [11] The Committee of Public Safety agents that enforced the policies of "The Terror" were referred to as "Terrorists". [12] The word "terrorism" was first recorded in English-language dictionaries in 1798 as meaning "systematic use of terror as a policy". [13]
Although the Reign of Terror was imposed by the French government, in modern times "terrorism" usually refers to the killing of people
by non-government political activists for political reasons, often as a public statement.

This meaning originated with Russian radicals in the 1870s. Sergey Nechayev, who founded People's Retribution (Народная расправа) in 1869, described himself as a "terrorist". [14] German anarchist writer Johann Most helped popularize the modern sense of the word by dispensing "advice for terrorists" in the 1880s. [15]

According to Dr Myra Williamson: "The meaning of "terrorism" has undergone a transformation. During the reign of terror a regime or system of terrorism was used as an instrument of governance, wielded by a recently established revolutionary state against the enemies of the people.

Now the term "terrorism" is commonly used to describe terrorist acts committed by non-state or subnational entities against a state.
 
Kikokotozi - is this how it is defined in the applicable law being quoted in the charge sheet?
 
Ahmed Khalfani Ghailani ndiye mtanzania aliyekuwa na kesi ya ugaidi achana na hii tamthiliya,jana si uliona scene zilivyorudiwa,mawazo ya mwanadamu/mtanzania yanayolindwa na kataba yenye uhalisia na Mara nyingi yanatokeaga kicks anti,siamini Kama haya yanatokea Huko.....
 
Kilichoichafua Tanzania ni
  • Kuuawa kwa mwandishi,
  • Kuuawa kwa viongozi wa dini,
  • Kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi
  • Kutekwa na kuteswa kwa mwandishi mwingine
  • Kumwagiwa sumu watu mbalimbali au kuumizwa na vitu vyenye ncha kali
  • Uchochezi mbalimbali unaoendelea, na
  • Maovu mengine dhidi ya binadamu


Na kitakachoipa sifa Tanzania ni kuanza kuwashughulikia kikamilifu Wahusika wakuu wa uvunjifu wa Amani kina Lwakatare na chama chake cha Demekrasia Feki!
 
Back
Top Bottom