Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Zari Hassan maarufu kama Boss Lady amejikuta mwenye majonzi baada ya mumewe, Cham Lutaaya, kuchezea kichapo heavy na kupoteza kwa knockout mikononi mwa msanii Rickman Manrick katika pambano la The Kampala Rumble.
Pambano hilo lililofanyika jana Agosti 30, 2025 katika Ukumbi wa MTN Arena Lugogo*, jijini Kampala, Uganda. Baada ya wiki kadhaa za maneno makali kabla ya mpambano, mashabiki walijaa ukumbini kwa hamu ya kushuhudia kivumbi hicho cha nyota wawili.
Hata hivyo, kila kitu kiliisha ghafla katika raundi ya pili. Shakib, baada ya kuzidiwa mashambulizi, alipigwa ngumi kali na Rickman. Knockout hiyo ililipua shamrashamra ndani ya ukumbi na mara moja ikasambaa kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki walimsifu Rickman kwa ushindi wake huku wakimkejeli Shakib kwa kipigo alichopata, video za tukio hilo zikisambaa kwa kasi.