Lusinde: Kiti cha spika kinapwaya

Lusinde: Kiti cha spika kinapwaya

CCM wanadhani jimbo la Mtera limekosa mwakilishi makini na hivyo juhudi zinafanyika ili wamng'oe, na mimi sina hakika kama wakati kama huu mwakani tutakuwa naye maana CCM wakimkosakosa nina hakika UKAWA hawatamwacha, lazima atamumwaga. Hatuwezi kuwa na wabunge ambao kkazi yao kubwa ni vijembe na halafu akafikiria atachaguliwa tena kwa vijembe vyake. Tundu Lissu alipodai apewe dakika zaidi ya dk tatu ambazo spika alizokuwa ameamua zitumike alikuwa amefuata kanuni na taratibu za bunge na ndiyo maana spika alikubaliana naye, sasa mbunge ambaye siku zote yuko bungeni lakini hajui hata hizi taratibu rahisi anakaaje bungeni. Wabunge wote wa aina yake lazima wawapishe wenye uwezo wakatufanyie kazi.
naunga mkono wabunge aina ya lusinde wanaliaibisha bunge, wanaliaibisha taifa! Poleni wana mtera.
 
Wana mtera mkirudisha hiki kiazi mwaka huu itabidi jimbo Zima mkapimwe akili tena uzuri hospitali ya magonjwa ya akili iko hapo hapo mkoani kwenu dodoma.
 
Mimi nitaamini kwamba sasa Watanzania wameelimika endapo watawapiga chini wabunge wote mizigo na vihiyo. Hatuwezi kuwa na wabunge aina ya joti wanaokwenda kufanya komedi na kuchekesha watu bungeni. Tunataka wabunge serious ndani ya bunge na siyo comedians.

Shida inakuja kuwa wapiga kule wengi vijiji hawana elimu hivyo wanamchagua mtu wa kufanana nao, wao kwao elimu sio tija ila vile vikofia na vitisheti
 
Kilichopwaya ni kiti cha Lusinde! Ndiyo maana na kujikomba kwake kote, hata JK ameona kwamba hamfai katika Baraza lake dhaifu la mawaziri.
haa haa lusinde awe waziri! Toba!! Hapo wizarani muda wote vitapigwa vichekesho na komedi za nguvu badala ya kuwatumikia watanzania!
 
Wana mtera mkirudisha hiki kiazi mwaka huu itabidi jimbo Zima mkapimwe akili tena uzuri hospitali ya magonjwa ya akili iko hapo hapo mkoani kwenu dodoma.
haa haaa...yaani jimbo zima wamekosa mtu wa kuwawakilisha bungeni wakampata lusinde! Kama taifa kwenye elimu tumekwama kama wabunge wenyewe ndo hawa"
 
Wenginajadili upuuzi, hii inanishawishi wengi mlifuata magamba vyuoni na mashuleni, mtu aliyeelimisha hujadili mambo muhimu na kutoa suluhisho ya nini kifanyike kwa maslahi ya nchi yetu. Mm c muumini wa siasa, ola kwa style hii upinzani tz itabidi wasubiri sana, other wise badilikeni, kwa kufanya siasa za kistarabu.
 
Sio kwamba kiti cha spika kinapwaya,ccm huwa wanamtegemea Mwigulu awashambulie wapinzani,lakini sasa hivi Mwigulu ameona anapoteza nguvu nyingi peke yake wakati wenzake wanatumia muda mwingi kusaka urais.Kuna wengine hawatumikii chama wanasubiri urais tu.
 
Lusinde amesema makinda anapwaya kwa kuwa sasa hivi halindi maslahi ya ccm, anafuata pressure ya UKAWA, na kwa kufanya hivo CCM inaumizwa kwa kuonekana hamna wanalolifanya.

Wamfundishe nidhamu kama mtiifu Samwel Sitta
 
CCM wanadhani jimbo la Mtera limekosa mwakilishi makini na hivyo juhudi zinafanyika ili wamng'oe, na mimi sina hakika kama wakati kama huu mwakani tutakuwa naye maana CCM wakimkosakosa nina hakika UKAWA hawatamwacha, lazima atamumwaga. Hatuwezi kuwa na wabunge ambao kkazi yao kubwa ni vijembe na halafu akafikiria atachaguliwa tena kwa vijembe vyake. Tundu Lissu alipodai apewe dakika zaidi ya dk tatu ambazo spika alizokuwa ameamua zitumike alikuwa amefuata kanuni na taratibu za bunge na ndiyo maana spika alikubaliana naye, sasa mbunge ambaye siku zote yuko bungeni lakini hajui hata hizi taratibu rahisi anakaaje bungeni. Wabunge wote wa aina yake lazima wawapishe wenye uwezo wakatufanyie kazi.

Ni wale wabunge wa nyama choma na DADA POA.
 
Huyujamaa sijuii walimpaje ubunge alitakiwa aawe anauza chaja za techno. Na. Huawei. Pale sinza vibandani
 
Utafiti wangu unaonesha.kuwa kibajaji akiongea wale waropokaji nassari na lema wanatulia tuliiii sijui kwa nini!
 
Pro-Chadema wengi uwa wanafiki sana hawajui wanachotaka wala wanachokipigania.

Juzi walikuwa wanaungana na Lusinde kuhusu ushahidi wake kuwa Zitto Kabwe aliongwa milioni 10 na PAP.

Tukaambiwa kuwa anafuatiliwa na TAKURU, leo tena pro-Chadema mnapingana na Lusinde.

Mkuu ndio maana utawala unawashinda,kwahiyo Lusinde hata akiongea points za msingi apingwe na Cdm?,na Zito akifanya utumbo asisemwe kwa kua ni upinzani?Acha fikra mgando mkuu,hiyo inadhihiridha jinsi ulivyo boya
 
Back
Top Bottom