Lusinde (Kibajaji) ni mvivu kusoma

Lusinde (Kibajaji) ni mvivu kusoma

Kwa ufupi ni kwamba Kibajaji amechagua ujinga badala ya elimu, na kama tujuavyo elimu ya mjinga ni majungu (hata TOT waliimba hivyo).

Amesahau kuwa Banzastone alishawahi kuimba kuwa, "Kama Elimu ni ghali, basi jaribu ujinga". Kibajaji ameamua kujaribu ujinga. Ila bado muda upo wa kujaribu kuwa na Elimu pia. Akijaribu kuwa na Elimu atagundua jinsi wajinga wanavyotumika wanavyotumiwa na wanasiasa werevu na wanavyojidhalilisha wakiongea mambo wasiyoyajua
 
Mbunge wa Mtera ndugu Livingstone Lusinde au Kibajaji amekuwa akisema mara kwa mara kuwa hajasoma kwa sababu wazazi wake walifariki wakati yeye akiwa darasa la nne. Kwa ufupi shule ya Msingi ndiyo ikawa mwisho wa elimu ya Kibajaji.

Mawazo au malalamiko haya ya kibajaji hayana mashiko kwa sasa hivi kwani mtu anaweza kuendelea na elimu hata anapokuwa mtu mzima. Hata hapo bungeni ajaribu kuuliza wabunge wenzake kuhusu swala la elimu kwani kuna wengine wamepata diploma, first degree, Masters na Hata Phd wakiwa bungeni. na labda wametokea kwenye familia zenye matatizo kuliko yeye.

Kibajaji kama angetaka kujiendeleza angeanza kusoma QT (qualification Test) hapo ni mwaka mmoja, ikiwa ni elimu sawa kabisa na ya form one na form two. Baada ya hapo angesoma form 3 na 4 kwa mwaka mmoja. Yaani form one mpaka form 4 angesoma kwa miaka 2 tu. halafu form 5 na form six angesoma kwa mwaka mmoja tu. Labda kama ni kilaza wa kufa mtu. Nafasi anayo yakufanya hivyo. Tangua aingie bungeni mpaka sasa hivi yaani muda wa miaka 5 ungekuta anamalizia mwaka wa 3 chuo kikuu. Na hapa alikuwa na nafasi mbalimbali alizopita kabla ya kuwa mbunge angeweza kujiendeleza.

Hivyo kupitia kibajaji msitegemee kupata hoja za maana za kuendeleza nchi yetu na badala yake atakuwa akiongea majungu, matusi(kama alivyofanya Arumeru Mashariki) na upotoshaji kwa kutojua kama alivyofanya kwenye swala la ESCROW. Wananchi wa Mtera nawapa pole sana kwa kuchagua Mbumbu huyu, awamu hii ya uchaguzi mfikirie mara mbili kabla ya kufanya uwamuzi. Msikubali kuendelea kuchagua mbumbu la kujitakia. Ushauri wangu kwa kibajaji au Livingstone Lusinde kuwa aanze kujiendeleza kwani fursa ipo na aache kulalamika kuwa aliachwa yatima akiwa darasa la nne.

ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA MHESHIMIWA LIVINGSTONE LUSINDE

Ushuari mzuri pia mpe sugu na mbowe
 
Amesahau kuwa Banzastone alishawahi kuimba kuwa, "Kama Elimu ni ghali, basi jaribu ujinga". Kibajaji ameamua kujaribu ujinga. Ila bado muda upo wa kujaribu kuwa na Elimu pia. Akijaribu kuwa na Elimu atagundua jinsi wajinga wanavyotumika wanavyotumiwa na wanasiasa werevu na wanavyojidhalilisha wakiongea mambo wasiyoyajua
Umesema kweli mkuu
 
Elimu haipo shuleni pekee. Shule zingine zinafundisha ujinga, kama tuonavyo kwa wanajamii wengi.
 
Hivi na wewe unatetea ujinga?, ni shule gani zinazofundisha ujinga ili watu au watoto wetu wasizisome au serikali yako ya CCM iwashghulikie kama kweli inataka kumaliza tatizo la ujinga mashuleni
 
aanze kulitafuta darasa LA Saba, then form 1. kisha form 4, baadae form 6, then degree si atahitimu na miaka 80 huyo kibajaji
 
jamaa ni mjinga mtupu kichwani afu hana hekima
 
Mbunge wa Mtera ndugu Livingstone Lusinde au Kibajaji amekuwa akisema mara kwa mara kuwa hajasoma kwa sababu wazazi wake walifariki wakati yeye akiwa darasa la nne. Kwa ufupi shule ya Msingi ndiyo ikawa mwisho wa elimu ya Kibajaji.

Mawazo au malalamiko haya ya kibajaji hayana mashiko kwa sasa hivi kwani mtu anaweza kuendelea na elimu hata anapokuwa mtu mzima. Hata hapo bungeni ajaribu kuuliza wabunge wenzake kuhusu swala la elimu kwani kuna wengine wamepata diploma, first degree, Masters na Hata Phd wakiwa bungeni. na labda wametokea kwenye familia zenye matatizo kuliko yeye.

Kibajaji kama angetaka kujiendeleza angeanza kusoma QT (qualification Test) hapo ni mwaka mmoja, ikiwa ni elimu sawa kabisa na ya form one na form two. Baada ya hapo angesoma form 3 na 4 kwa mwaka mmoja. Yaani form one mpaka form 4 angesoma kwa miaka 2 tu. halafu form 5 na form six angesoma kwa mwaka mmoja tu. Labda kama ni kilaza wa kufa mtu. Nafasi anayo yakufanya hivyo. Tangua aingie bungeni mpaka sasa hivi yaani muda wa miaka 5 ungekuta anamalizia mwaka wa 3 chuo kikuu. Na hapa alikuwa na nafasi mbalimbali alizopita kabla ya kuwa mbunge angeweza kujiendeleza.

Kwa ufupi ni kwamba Kibajaji amechagua ujinga badala ya elimu, na kama tujuavyo elimu ya mjinga ni majungu (hata TOT waliimba hivyo).

Hivyo kupitia kibajaji msitegemee kupata hoja za maana za kuendeleza nchi yetu na badala yake atakuwa akiongea majungu, matusi(kama alivyofanya Arumeru Mashariki) na upotoshaji kwa kutojua kama alivyofanya kwenye swala la ESCROW. Wananchi wa Mtera nawapa pole sana kwa kuchagua Mbumbu huyu, awamu hii ya uchaguzi mfikirie mara mbili kabla ya kufanya uwamuzi. Msikubali kuendelea kuchagua mbumbu la kujitakia. Ushauri wangu kwa kibajaji au Livingstone Lusinde kuwa aanze kujiendeleza kwani fursa ipo na aache kulalamika kuwa aliachwa yatima akiwa darasa la nne.

ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA MHESHIMIWA LIVINGSTONE LUSINDE

Nakubaliana na wewe 100% huyu jamaa mjinga sana uwa sielewi watu wa Mtera walimchagua kwa vigezo gani.
 
Ujinga na ukosefu wa elimu ni baadhi ya sifa za wagombea/viongozi wa CCM.Sasa hao waliowajinga zaidi ndo huwa wanatumika kutukana as toilet pepa.
Akumbuke..If you think education is expensive,try ignorance.
 
aanze kulitafuta darasa LA Saba, then form 1. kisha form 4, baadae form 6, then degree si atahitimu na miaka 80 huyo kibajaji
Mkuu hapo nilipobold pana walakini.Si mkuu wa Inji alisema elimu ya msingi sasa itakuwa miaka 10?
 
Ujinga na ukosefu wa elimu ni baadhi ya sifa za wagombea/viongozi wa CCM.Sasa hao waliowajinga zaidi ndo huwa wanatumika kutukana as toilet pepa.
Akumbuke..If you think education is expensive,try ignorance.
Hapana siyo kweli tutoe ushabiki mbona hata Chadema kuna wabunge wengi hawana elimu pale Bungeni.

Unaweza kunipa elimu ya Mbowe, Lema, Sugu.
 
Ujinga na ukosefu wa elimu ni baadhi ya sifa za wagombea/viongozi wa CCM.Sasa hao waliowajinga zaidi ndo huwa wanatumika kutukana as toilet pepa.
Akumbuke..If you think education is expensive,try ignorance.
Wapo kibao ambao wapo level moja na Lusinde lakini kutokana na elimu isiyorasmi ya mtaani (au elimu ya jadi) wamebadilika kutokana na mazingira na pamoja na kwamba ni STD 7 lakini wana michango mizuri tu kwenye jamii na makongomano mbalimbali ila huyu jamaa ni zigo maana ameshindwa ku-cope na mazingira aliyopo (kilichofanyika Mtera ni maamuzi ya hasira dhidi ya mbunge wao wa zamani na mwisho wa siku jamaa akaibuka kidedea nadhani kuna watu walimsaidia kusoma upepo)
 
aanze kulitafuta darasa LA Saba, then form 1. kisha form 4, baadae form 6, then degree si atahitimu na miaka 80 huyo kibajaji
Miaka 6 mpaka 7 atakuwa amemaliza degree kama siyo kilaza. Lakini kama ni kilaza anweza kuzeeka au kuwa na umri ulioutaja bila kuwa na degree. Lakini anapenda kusoma? hilo ndiyo swali la msingi ambalo anatakiwa aulizwe,

Wapo kibao ambao wapo level moja na Lusinde lakini kutokana na elimu isiyorasmi ya mtaani (au elimu ya jadi) wamebadilika kutokana na mazingira na pamoja na kwamba ni STD 7 lakini wana michango mizuri tu kwenye jamii na makongomano mbalimbali ila huyu jamaa ni zigo maana ameshindwa ku-cope na mazingira aliyopo (kilichofanyika Mtera ni maamuzi ya hasira dhidi ya mbunge wao wa zamani na mwisho wa siku jamaa akaibuka kidedea nadhani kuna watu walimsaidia kusoma upepo)
Yawezekana aliingia kwa upepo wa ushabiki, lakini jamaa kiukweli hakuna kitu pale...sijui kama anajijua kuwa hana kitu kichwani, kama hajui kama anajua anatakiwa asaidiwe, lakini kama hajui halafu anajifanya anajua huyo muacheni kwani ni sawa na mtu anatembea uchi halafu anasema hayuko uchi.

jamaa ni mjinga mtupu kichwani afu hana hekima
Yaani ingekuwa zamani wakati ambapo kulikuwa hakuna elimu asingepata uongozi wowote wa kimila...kwani walikuwa wanaangalia mtu mwenye busara na hekima. Sasa hekima na busara ni kitu kikubwa sana huyu Kibajaji amepungukiwa achilia mbali swala la elimu

Back
Top Bottom