SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,616
- 925
Mbunge wa Mtera ndugu Livingstone Lusinde au Kibajaji amekuwa akisema mara kwa mara kuwa hajasoma kwa sababu wazazi wake walifariki wakati yeye akiwa darasa la nne. Kwa ufupi shule ya Msingi ndiyo ikawa mwisho wa elimu ya Kibajaji.
Mawazo au malalamiko haya ya kibajaji hayana mashiko kwa sasa hivi kwani mtu anaweza kuendelea na elimu hata anapokuwa mtu mzima. Hata hapo bungeni ajaribu kuuliza wabunge wenzake kuhusu swala la elimu kwani kuna wengine wamepata diploma, first degree, Masters na Hata Phd wakiwa bungeni. na labda wametokea kwenye familia zenye matatizo kuliko yeye.
Kibajaji kama angetaka kujiendeleza angeanza kusoma QT (qualification Test) hapo ni mwaka mmoja, ikiwa ni elimu sawa kabisa na ya form one na form two. Baada ya hapo angesoma form 3 na 4 kwa mwaka mmoja. Yaani form one mpaka form 4 angesoma kwa miaka 2 tu. halafu form 5 na form six angesoma kwa mwaka mmoja tu. Labda kama ni kilaza wa kufa mtu. Nafasi anayo yakufanya hivyo. Tangua aingie bungeni mpaka sasa hivi yaani muda wa miaka 5 ungekuta anamalizia mwaka wa 3 chuo kikuu. Na hapa alikuwa na nafasi mbalimbali alizopita kabla ya kuwa mbunge angeweza kujiendeleza.
Kwa ufupi ni kwamba Kibajaji amechagua ujinga badala ya elimu, na kama tujuavyo elimu ya mjinga ni majungu (hata TOT waliimba hivyo).
Hivyo kupitia kibajaji msitegemee kupata hoja za maana za kuendeleza nchi yetu na badala yake atakuwa akiongea majungu, matusi(kama alivyofanya Arumeru Mashariki) na upotoshaji kwa kutojua kama alivyofanya kwenye swala la ESCROW. Wananchi wa Mtera nawapa pole sana kwa kuchagua Mbumbu huyu, awamu hii ya uchaguzi mfikirie mara mbili kabla ya kufanya uwamuzi. Msikubali kuendelea kuchagua mbumbu la kujitakia. Ushauri wangu kwa kibajaji au Livingstone Lusinde kuwa aanze kujiendeleza kwani fursa ipo na aache kulalamika kuwa aliachwa yatima akiwa darasa la nne.
ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA MHESHIMIWA LIVINGSTONE LUSINDE