Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
MASTAA wawili wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ wamejikuta wakiingia kwenye mtifuano mkali baada ya kutoleana maneno machafu.
Ishu ilianzia kwa Gigy ambaye alisema mwanadada Lulu hajui kuvaa, huwa anavaa matangazo, hii ni baada ya kuulizwa na kituo kimoja cha runinga kwamba ataje mastaa kumi wanaojua kuvaa.
Lulu aliamua kumjibu kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram kuwa bora asijue kuvaa lakini hawezi kuvaa matambara kama yeye.
“Gigy alikasirishwa sana na kitendo cha Lulu kumwambia anavaa matambara alijikuta akipaniki na yeye akaendelea kushilikilia msimamo kwamba anavaa nguo za matangazo hivyo ni bora yeye anayevaa matambara anayonunua mwenyewe kuliko yeye,” kilisema chanzo.
Gigy alipoulizwa kulikoni, alisema amekasirishwa sana na kitendo cha Lulu kumwambia anavaa matambara wakati yeye alizungumza kama anavyoona kwani mavazi anayovaa hayaendani na mazingira.
“Matambara ni ya kwangu na haya ni maisha yangu siyo yeye anayevaa nguo za matangazo eti anajiona naye anavaa maana naona Lulu ameunda na kampeni na makundi kwa ajili ya kunishambulia, mimi ni jeshi la mtu mmoja hawaniwezi,” alisema Gigy Money.
Source: Tanzania Today