Lulu atamani kushindana na wasomi

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
lulu.jpg

Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu amefunguka na kusema kama wasanii wa filamu nchini wana wakati mgumu kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo ya filamu nchini.

Kupitia Account yake ya Twitter Lulu Michael ameonyesha kukatishwa tamaa na mambo mbalimbali kwenye tasnia hiyo huku akionyesha wazi uelewa mdogo na kukosa maarifa kwa baadhi ya wasanii ndiyo chanzo kushindwa kusonga mbele kwani wengi wao wanashindana kwa mambo ambayo hayana tija kwenye tasnia hiyo.

Lulu Michael ametamani kuongeza elimu zaidi ili aweze kushindana na watu wenye elimu zao na watu ambao watampa changamoto za ushindani katika mambo ya maana kuliko kwenye tasnia hiyo ambapo watu wana kazi ya kushindana kuvaa, uzuri na umaarufu.

“Watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo outings na umaarufu, umaarufu wenyewe kama network ya mtandao mpya full kukatakata, hebu nikazane kusoma nianze ligi za kikubwa na dada zangu wenye madegree na ma masters kama Esilovey hizi ligi nyingine zinasikitisha” aliandika Lulu Michael
 
Kuongeza elimu sio vibaya.....
Sasa wasomi atashindana nao vipi.??? Kwamba kuwapita wenye masters au???

Afanye kazi kwa bidii...atoe filamu viwango...
Afanye kazi kiprofeshino....

Hatimaye atafanikiwa....
 
Umaarufu wa Instagram unagharimu sana wasanii wetu wa kibongo. Ni vizuri huyu mtoto amejitambua wakati bado umri haujamtupa Mkono. Afanye bidii tuu na ndoto Zake zitatimia
 
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael alimaarufu kama Lulu amefunguka na kusema kama wasanii wa filamu nchini wana wakati mgumu kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo ya filamu nchini.
Kupitia Account yake ya Twitter Lulu Michael ameonyesha kukatishwa tamaa na mambo mbalimbali kwenye tasnia hiyo huku akionyesha wazi uelewa mdogo na kukosa maarifa kwa baadhi ya wasanii ndiyo chanzo kushindwa kusonga mbele kwani wengi wao wanashindana kwa mambo ambayo hayana tija kwenye tasnia hiyo.
Lulu Michael ametamani kuongeza elimu zaidi ili aweze kushindana na watu wenye elimu zao na watu ambao watampa changamoto za ushindani katika mambo ya maana kuliko kwenye tasnia hiyo ambapo watu wana kazi ya kushindana kuvaa, uzuri na umaarufu.
“Watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo outings na umaarufu, umaarufu wenyewe kama network ya mtandao mpya full kukatakata, hebu nikazane kusoma nianze ligi za kikubwa na dada zangu Wenye ma degree na ma masters Kama Esilovey hizi ligi nyingine zinasikitisha, watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo Outings na umaarufu, umaarufu wenyewe Kama network ya mtandao unaokuwaga mpya, full kukatakata,” aliandika Lulu Michael

Huo Ndio ukweli mchungu about Bongo Movie , nguo , outings , makalio na kutafuta mabwana , ni vizuri ameliona Hilo mapema hajachelewa
 
Lulu pamoja na mambo mengine lakini anajua jinsi ya kufanya life calculations ambazo wengi zinawashinda, kingine ni kuwa haexpose maisha yake kivile.

Yani, hiyo ni quality na attributr nzuri sana ya mwanamke ambayo wengi hawana.
She is a wife material.
 
Kama kweli kamaanisha kuongeza elimu ni vizuri sana maana umri bado una mruhusu, ila asiende huko kwa kushindana maana hata weza kuwa mshindi, aende kwa kuongeza ujuzi na maarifa, kama anataka ma degree na ma . phd atazipata za chupi tu na atarudi yule yule. Ameamua kusoma asome.
 
Ameanza kujtambua ee.!
huyu lulu ni LE AKILI KUBWAZZ.. ana akili ya maisha, ana kipaji kikubwa sana kisanaa, anajitambua, pia ni msichana aliyebarikiwa toka mdogo japo kuna changamoto za hapa na pale, ni maarufu toka mtoto mchanga, amedumu kwenye tasnia mda mrefu toka mtoto mpaka sasa hajachuja.. kifupi huyo totoz ni balaaa.. toka mtoto alikua ana-host kipindi cha watoto show ITV.. hongera kwako endelea kukumbiza MABOYA na washamba wa jiji(wanaume kwa wanawake)
 
Mi bnafsi pia huwa namkubal anawashnda hata dada zake kwa skendo chafu(lyk wema)

Kwa kifupi...'Anafaa kuwa mke wa m2"!!
 
Back
Top Bottom