Usimfundishe mtoto kushindana

Usimfundishe mtoto kushindana

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,448
Reaction score
3,935
Kauli hii inatoka katika Wafilipi 2:3 inayosema: "Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."
Maana ya Andiko Hili

Epuka Mashindano: Usifanye mambo kwa nia ya kushindana, kuleta ugomvi, au kuonyesha kuwa wewe ni bora kuliko wengine

Ondoa Majivuno*: Usitende mambo kwa kiburi au kutafuta sifa za kibinafsi na sifa za kijinga.Kuwa Mnyenyekevu:
Mheshimu mwenzako na umhesabu kuwa wa thamani kubwa kuliko nafsi yako

Hata haya mambo ya shule za vipaji maalumu special school,haya mambo ya KUSHINDANA kushika nafasi ya kwanza darasani.
Kumjengea mtoto kumuaminisha kuwa yeye ni Bora sana kuliko wengine ama ana akili sana kuliko wengine KWA sababu amesoma shule Bora kuliko wengine ,amesoma chuo kikuu Bora kuliko wengine ,ana akili nyingi kuliko wengine na kwa sababu ana shika nafasi ya kwanza mpaka ya tatu au kumi Bora darasani.

NI KITU KIBAYA SANA .
Wengine tulipokuwa tuna soma tulikuwa tunashika hizi nafasi za kumi Bora top five darasani,ama wengine waliongoza kiwilaya ama kimkoa ,na wengine wamesoma vyuo vikuu Bora duniani ama hapa nchini ,ama shule za vipaji maalumu.SO WHAT??

SIO KWELI kwamba kushika nafasi ya kwanza darasani inakufanya WEWE kuwa Bora kuliko mwingine asiye shika nafasi ya kwanza darasani,sio KWELI MTU aliyesoma hizi formal education ni Bora kuliko MTU ambaye hajasoma hizi formal education/mwenye informal education.

KUMJENGEA MWANAO ajione kuwa yeye ni SPECIAL NI BORA kuliko wengine ni kitu KIBAYA SANA na sio REALISTIC NI MYTH.

Hata baadhi ya vyuo vikuu kuwaambia wanafunzi wao kuwa YOU ARE THE CREAM OF THE NATION ,nyie sio vyuo vya kata ,nyoe ni BORA SANA ni mbaya sana,
Haiwasaidii haiwajengi kitu na SIO KWELI NI UONGO.

Mungu anahitaji watu wote tuishi KWA UMOJA NA KUPENDANA na KUHESHIMIANA na kuthaminiana.

sisi wanadamu wote kila mmoja WETU Mungu amempa sehemu ya vipawa na karama yake tofauti tofauti lakini wote KWA UMOJA WETU tukishirikiana karama Mungu alizotupa tukiziunganisha ndio tunakamilishana na kukamilika.KILA MTU ni WA muhimu na kila MTU anahitaji watu.

Ukijiona kuwa Bora kuliko wengine hiyo inakutenganisha na watu ambao unawahitaji.

Wakorintho 12), yanayoeleza jinsi jamii au kanisa linavyopaswa kufanya kazi kwa umoja licha ya utofauti wa wanachama wake.
Maana yake kuu ni kwamba utofauti wa vipaji haupaswi kuleta mgawanyiko, bali unakamilisha ujenzi wa jumuia moja madhubuti.

Umuhimu wa Vipawa Tofauti katika Mwili Mmoja Kutegemeana:
Jicho haliwezi kusikia, na sikio haliwezi kuona.

Kila kiungo kinahitaji kingine ili mwili mzima uishi.
Kutofautiana kwa Majukumu: Kila mtu ana uwezo wa kipekee (uongozi, ualimu, huruma, au kusaidia) unaofaa kwa kazi maalum.Unyenyekevu:
Hakuna kipawa kilicho bora kuliko kingine. Vyote ni muhimu kwa ustawi wa pamoja.Lengo la Pamoja:

Vipaji vyote vinatakiwa kutumika kwa ajili ya kujenga na kuendeleza jumuia,
 
Luka 18:10-14

10 Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 yule Farisayo alisimama akasali kimoyomoyo. ‘Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine: wany ang’anyi, wadhalimu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma na kutoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali. Hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto akasema, ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.”
 
Mfano huu..

Mzungu mmoja alienda kutalii kisiwani,akakodi mtumbwi wa mvuvi mwenyeji wa kisiwa hicho,ili amtembeze KWA mtumbwi kumvusha kutalii

mzungu Akamuuliza unajua kucheza tennis 🎾 mvuvi akajibu hapana,

akamuuliza Tena unajua ,karata last card ♦️♠️ Mvuvi akajibu hapana sijui

Akamuuliza Tena unajua kuendesha baiskeli mvui akajibu Tena sijui.

Mzungu akamwambia hujui hata kuendesha baiskeli,kila kitu nakuuliza hujui sasa unaishije sasa???

Basi wakaendelea na safari,walipofika katikati ya ziwa yakatokea mawimbi na upepo ,mtumbwi ukayumba ukapinduka ziwani.
waliokuwa katikati ya maji mvuvi akamuuliza mzungu,
Boss je UNAJUA KUOGELEA...mzungu akamjibu hapana ,siwezi kabisa KUOGELEA..

Mvuvi akamjibu ,hujui hata KUOGELEA sasa BOSS utaishije ?
 
.
 
Attachments

  • usishindane.jpg
    usishindane.jpg
    32.3 KB · Views: 1
  • bad parent 2.webp
    bad parent 2.webp
    88.3 KB · Views: 2
  • bad parenting.jpg
    bad parenting.jpg
    41 KB · Views: 1
Kauli hii inatoka katika Wafilipi 2:3 inayosema: "Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."
Maana ya Andiko Hili

Epuka Mashindano: Usifanye mambo kwa nia ya kushindana, kuleta ugomvi, au kuonyesha kuwa wewe ni bora kuliko wengine

Ondoa Majivuno*: Usitende mambo kwa kiburi au kutafuta sifa za kibinafsi na sifa za kijinga.Kuwa Mnyenyekevu:
Mheshimu mwenzako na umhesabu kuwa wa thamani kubwa kuliko nafsi yako

Hata haya mambo ya shule za vipaji maalumu special school,haya mambo ya KUSHINDANA kushika nafasi ya kwanza darasani.
Kumjengea mtoto kumuaminisha kuwa yeye ni Bora sana kuliko wengine ama ana akili sana kuliko wengine KWA sababu amesoma shule Bora kuliko wengine ,amesoma chuo kikuu Bora kuliko wengine ,ana akili nyingi kuliko wengine na kwa sababu ana shika nafasi ya kwanza mpaka ya tatu au kumi Bora darasani.

NI KITU KIBAYA SANA .
Wengine tulipokuwa tuna soma tulikuwa tunashika hizi nafasi za kumi Bora top five darasani,ama wengine waliongoza kiwilaya ama kimkoa ,na wengine wamesoma vyuo vikuu Bora duniani ama hapa nchini ,ama shule za vipaji maalumu.SO WHAT??

SIO KWELI kwamba kushika nafasi ya kwanza darasani inakufanya WEWE kuwa Bora kuliko mwingine asiye shika nafasi ya kwanza darasani,sio KWELI MTU aliyesoma hizi formal education ni Bora kuliko MTU ambaye hajasoma hizi formal education/mwenye informal education.

KUMJENGEA MWANAO ajione kuwa yeye ni SPECIAL NI BORA kuliko wengine ni kitu KIBAYA SANA na sio REALISTIC NI MYTH.

Hata baadhi ya vyuo vikuu kuwaambia wanafunzi wao kuwa YOU ARE THE CREAM OF THE NATION ,nyie sio vyuo vya kata ,nyoe ni BORA SANA ni mbaya sana,
Haiwasaidii haiwajengi kitu na SIO KWELI NI UONGO.

Mungu anahitaji watu wote tuishi KWA UMOJA NA KUPENDANA na KUHESHIMIANA na kuthaminiana.

sisi wanadamu wote kila mmoja WETU Mungu amempa sehemu ya vipawa na karama yake tofauti tofauti lakini wote KWA UMOJA WETU tukishirikiana karama Mungu alizotupa tukiziunganisha ndio tunakamilishana na kukamilika.KILA MTU ni WA muhimu na kila MTU anahitaji watu.

Ukijiona kuwa Bora kuliko wengine hiyo inakutenganisha na watu ambao unawahitaji.

Wakorintho 12), yanayoeleza jinsi jamii au kanisa linavyopaswa kufanya kazi kwa umoja licha ya utofauti wa wanachama wake.
Maana yake kuu ni kwamba utofauti wa vipaji haupaswi kuleta mgawanyiko, bali unakamilisha ujenzi wa jumuia moja madhubuti.

Umuhimu wa Vipawa Tofauti katika Mwili Mmoja Kutegemeana:
Jicho haliwezi kusikia, na sikio haliwezi kuona.

Kila kiungo kinahitaji kingine ili mwili mzima uishi.
Kutofautiana kwa Majukumu: Kila mtu ana uwezo wa kipekee (uongozi, ualimu, huruma, au kusaidia) unaofaa kwa kazi maalum.Unyenyekevu:
Hakuna kipawa kilicho bora kuliko kingine. Vyote ni muhimu kwa ustawi wa pamoja.Lengo la Pamoja:

Vipaji vyote vinatakiwa kutumika kwa ajili ya kujenga na kuendeleza jumuia,
Fundisho la mudi boy linasema waislamu washindane kutenda mema ...mudi boy ni kiumbe kisicho na akili Al-mukheef Jagina Covax Malaria 2
 
Back
Top Bottom