Lukuvi usiwakandamize raia wa Tanzania

Lukuvi usiwakandamize raia wa Tanzania

Tatizo kubwa la ndugu yetu Lukuvi ni shule, inaweza na yy ni mmojawapo wa wahanga wa vyeti fake! Muhimu akasome kidogo aongeze elimu.. huu mchezo hauhitaji hasira.. ingekua hivyo waarabu wasingenunua majumba hapo London kwa sababu sio wazawa wa UK..na hawana uraia wa UK.
 
Hivi karibuni waziri Lukuvi amemfutia mfanya biashara mmoja Huko Mwanza mali zake kutokuwa mmiliki halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Lakini ameshindwa kutoa uthibitisho kuwa sio raia wa Tanzania, wakati mmiliki ana hati halali za kuzaliwa Tanzania na ana familia Tanzania.

Tatu ameshutumu watanzania kuomba uraia nje na kuja Tanzania kama watanzania na ku miliki mali kama nyumba, viwanja na biashara, hujui kuwa hawa ni watanzania halali walio enda nje kutafuta riziki halali na kujikomboa katika umasikini ambao uliopaliliwa toka tupate uhuru na serikali yako.

Viongozi hamuoni ufahari watanzania hao walivyopata mafanikio huko ughaibuni na kuja kuwekeza kwao, halafu kwa unafiki wenu, munaanzisha makongamano ya wana diaspora.

Viongozi na uraia pacha

Wako walikuwa maofisa wa ubalozi na mabalozi wenye uraia wa nje na familia zao ndani ya serikali yako, kama serikali na kama wewe waziri anza kwa watumishi wa mabalozi huko nje, na mabalozi na walio kuwa mabalozi.

Na wengine wako Zanzibar ndani ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kama mawaziri na wajumbe wa baraza la wakilishi, tena wanaishi kinyume na taratibu za uhamiaji.

Msiwakandamize wananchi wa kawaida tu kwa cheo chenu

Hata mimi nimeona na kusikia ile video kwenye Facebook. Kwa kweli imenitia hasira n kunihuzunisha, kwani Lukuvu amedhihirisha tena kwamba busara zake zipo chini. Kama kiongozi, hakustahili kabisa kuongea kwa chuki na kejeli vile dhidi ya Watanzania waishio nje...eti "kuna watu wamejilipua huko nje...na sasa wanajifanya kuishi hapa kama Watanzania, hawaruhusiwi kumiliki ardhi...[ ]..." Watu anaowazungumzia Lukuvi wanaweza kweli wakawa sio raia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria zao zilizopitwa na wakati na za kibaguzi, lakini pamoja na hilo watu hao bado ni Watanzania kwa maana ya utaifa wao, na si busara wala haki kuwatenga. Huu ubaguzi hautowaacha CCM salama hata kidogo!
 
Mleta mada unanichanganya unaposema kuna mabalozi na maafisa wa balozi zetu nje wamepewa uraia katika nchi wanazo tuwakilisha. Ni nchi gani inatoa uraia kwa afisa ubalozi wa nchi nyingine ikijuwa kwamba huyo mtu anatunza siri za nchi aliyo toka?
 
Jamani, kama uchangiaji wa jf utaendelea kuwa hivi basi tuna kazi ngumu sana mbele yetu. Tuwe tunasoma na kudodosa kidogo sheria na taratibu za nchi yetu kabla ya kuchangia. Kama hujui omba maelekezo au acha wanaojua wachangie.
Kisheria, ukishajilipua na ukachukua uraia wa nchi nyingine basi unakuwa sio raia tena wa Tanzania. Hata kama tunakujua kuwa ulizaliwa Kariakoo. Ndio maana watanzania walio nje wanalilia sana uraia wa nchi mbili.
Kwa suala hili vielelezo vyote alivyotumia vinaonyesha sio raia, sasa Lukuvi angefanyaje wakati yeye analinda sheria za nchi. Tusubiri siku watakapobadili sheria na kuruhusu uraia wa nchi mbili ndio ualalamishi huu ufanyike.
Niwape kisa kimoja. Kuna mama mmoja alienda Marekani, akapata mimba na kuzaa kule. Akarudi na mtoto akiwa mdogo lakini mtoto ana passport ya Marekani kwa kuwa alizaliwa kule. Ilibidi amlipie viza ya kuingia Tanzania kwa kuwa hakuwa raia wa Tz. Mtoto amebebwa anaambiwa sio raia wakati mama yake anaruhisiwa kuingia. Hiyo ndio sheria.
Wanaozungumzia maofisa ubalozi wanachekesha zaidi hapa.
 
Tatizo kubwa la ndugu yetu Lukuvi ni shule, inaweza na yy ni mmojawapo wa wahanga wa vyeti fake! Muhimu akasome kidogo aongeze elimu.. huu mchezo hauhitaji hasira.. ingekua hivyo waarabu wasingenunua majumba hapo London kwa sababu sio wazawa wa UK..na hawana uraia wa UK.
Kwanza hata kama hakusoma, bado ni waziei wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikidhi vigezo vyooote vya kuwa mbunge. Pili, unajua tofauti ya sheria ya Uingereza na aTanzania kuhusu umiliki wa ardhi? Acha serikali yetu itulinde vinginevyo watoto wetu watashindwa kununua ardhi siku moja.
 
Sheriaa ya ajabu sana hiyo ishapitwa na wakati.....hao wenyewe vigogo Wana uraia ea nchi mbili.....
Kuna watanzania Wana uraia nje na bado Wanawasaidia familia Zao huku.....

OVA
 
Mbona mheshimiwa kalieleza vizuri tu.ardhi ni ya wantanzania.wageni wanautaratibu wao.nenda India huone kama utanunua ardhi kinyemela.
 
Hivi karibuni waziri Lukuvi amemfutia mfanya biashara mmoja Huko Mwanza mali zake kutokuwa mmiliki halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Lakini ameshindwa kutoa uthibitisho kuwa sio raia wa Tanzania, wakati mmiliki ana hati halali za kuzaliwa Tanzania na ana familia Tanzania.

Tatu ameshutumu watanzania kuomba uraia nje na kuja Tanzania kama watanzania na ku miliki mali kama nyumba, viwanja na biashara, hujui kuwa hawa ni watanzania halali walio enda nje kutafuta riziki halali na kujikomboa katika umasikini ambao uliopaliliwa toka tupate uhuru na serikali yako.

Viongozi hamuoni ufahari watanzania hao walivyopata mafanikio huko ughaibuni na kuja kuwekeza kwao, halafu kwa unafiki wenu, munaanzisha makongamano ya wana diaspora.

Viongozi na uraia pacha

Wako walikuwa maofisa wa ubalozi na mabalozi wenye uraia wa nje na familia zao ndani ya serikali yako, kama serikali na kama wewe waziri anza kwa watumishi wa mabalozi huko nje, na mabalozi na walio kuwa mabalozi.

Na wengine wako Zanzibar ndani ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kama mawaziri na wajumbe wa baraza la wakilishi, tena wanaishi kinyume na taratibu za uhamiaji.

Msiwakandamize wananchi wa kawaida tu kwa cheo chenu
Lukuvi hakukosea hata kidogo. Sheria ya Tanzania hairuhusu dual citizenship. Ni juu ya Mwigulu kufuatilia aliyetoa uraia kwa asiye stahili. Kwa taarifa Tu kunà baadhi ya watu wana pasi hata tatu. Ya Tanzania inatumika tu kuingia na kutoka Tanzania. Hii ndiyo siyo haki. Wao wafuate sheria za nchi tu. Kuna muswada ulishapelekwa bungeni wa ku ruhusu uraia wa namna hii lakini haukupita. Kwa mada kama hizi na uchangiaji wa jinsi hii unawa expose ignorance yenu.

Kingine, nchi nyingi duniani zinajali wazawa nyinyi mnataka kuwainua wageni juu ya wazawa. Huu ni ujinga na Mimi sitakagi ujinga. Leteni mada zilizokuwa na mshiko.
 
Nimekumbuka issue ya Sumaye kulalamika kutaka kunyang'anywa ardhi...Nyumbu wana hasira na Lukuvi kuhusu issue ya Sumaye...kwa huyu mwingine ni kama kumalizia hasira zao tu..ila chuki zilianzia kule kwa Sumaye.

Nyumbu kasomeni sheria ya kumiliki ardhi kwanza, Lukuvi anasimamia sheria ya ardhi. Acheni kupiga kelele Nyumbu.
 
Hii ni vita ya serikali na matajiri.

Kwa uelewa wangu madeveloper wengi ni wageni, na kama mnavyojua real estate investing ni long term investing.

Je madeveloper watakuwa tayari kuwekeza kwenye mijengo kwa hayo masharti ambayo serikali wanayataka huku wakielewa kuna other investment destination kama south africa ambapo ardhi ni personal property na hakuna red tapes kama Tanzania na ROI ipo juu zaidi ya TZ.

Kwa mwenye uelewa naomba kufahamishwa kama hizo sheria za umiliki wa ardhi zinaapply kwa wageni kama individuals au hata kwa foreign owned companies?
 
Jee yeye Lukuvi ni msafi? Hana ufisadi wowote? Au anashabikia Watanzania wanaojituma kwa nguvu zao zote ughaibuni ili kuja kuwekeza nyumbani, kitu ambacho kinafaidisha Serekali ya Tanzania ma Watanzania wote kwa Ujumla
 
Jamani, kama uchangiaji wa jf utaendelea kuwa hivi basi tuna kazi ngumu sana mbele yetu. Tuwe tunasoma na kudodosa kidogo sheria na taratibu za nchi yetu kabla ya kuchangia. Kama hujui omba maelekezo au acha wanaojua wachangie.
Kisheria, ukishajilipua na ukachukua uraia wa nchi nyingine basi unakuwa sio raia tena wa Tanzania. Hata kama tunakujua kuwa ulizaliwa Kariakoo. Ndio maana watanzania walio nje wanalilia sana uraia wa nchi mbili.
Kwa suala hili vielelezo vyote alivyotumia vinaonyesha sio raia, sasa Lukuvi angefanyaje wakati yeye analinda sheria za nchi. Tusubiri siku watakapobadili sheria na kuruhusu uraia wa nchi mbili ndio ualalamishi huu ufanyike.
Niwape kisa kimoja. Kuna mama mmoja alienda Marekani, akapata mimba na kuzaa kule. Akarudi na mtoto akiwa mdogo lakini mtoto ana passport ya Marekani kwa kuwa alizaliwa kule. Ilibidi amlipie viza ya kuingia Tanzania kwa kuwa hakuwa raia wa Tz. Mtoto amebebwa anaambiwa sio raia wakati mama yake anaruhisiwa kuingia. Hiyo ndio sheria.
Wanaozungumzia maofisa ubalozi wanachekesha zaidi hapa.
Mkuu
Hao immigration wamemla pesa zake, mimi watoto wangu ni raia wa nje, nimekuja nao mwenyewe, nilipo fika airport nikagongewa kwa free kwa sababu watoto undermine, baadae nikaenda office za ndani immigration kuomba dual citizen kwa watoto wangu, wakagongewa kwenye passport zao, dual citizens hii mpaka watakapo fika 18 age, hapo watoto wana maaamuzi, kuwa na uraia upi.

Lakini kabla sijaja Tanzania niliwasiliana na ubalozi, wamenikatalia kunipa visa za watoto kwa free, kuna mtu kanipa maelekezo, nije nao mpaka airport Tanzania ndio watapata free visa ya 3 month halafu niwaombee dual citizens free pia
 
Lukuvi hakukosea hata kidogo. Sheria ya Tanzania hairuhusu dual citizenship. Ni juu ya Mwigulu kufuatilia aliyetoa uraia kwa asiye stahili. Kwa taarifa Tu kunà baadhi ya watu wana pasi hata tatu. Ya Tanzania inatumika tu kuingia na kutoka Tanzania. Hii ndiyo siyo haki. Wao wafuate sheria za nchi tu. Kuna muswada ulishapelekwa bungeni wa ku ruhusu uraia wa namna hii lakini haukupita. Kwa mada kama hizi na uchangiaji wa jinsi hii unawa expose ignorance yenu.

Kingine, nchi nyingi duniani zinajali wazawa nyinyi mnataka kuwainua wageni juu ya wazawa. Huu ni ujinga na Mimi sitakagi ujinga. Leteni mada zilizokuwa na mshiko.
Mgeni yupi, hapa tunaongea wazawa, iwe hata alijiripuwa nje, ni wazawa wa Tanzania
 
Back
Top Bottom