Lukuvi: Tunakuja na bei elekezi kwa viwanja

Lukuvi: Tunakuja na bei elekezi kwa viwanja

Bei elekezi ya sukari ni shilingi 1800 kwa kilo , mnanunua sukari kwa shilingi ngapi ?
 
safi sana kuna sehemu unaangalia hadi unauliza hichi kiwanja kwanini kinauzwa bei hii na wakati ni sehemu haipo karibu na mjini, haina good scenery, haina the most fertile soil hamna hata ugunduz wa gas wala madini katika hyo sehem na haipo karibu na huduma za jamii including schools, hospitals au hata vituo vya police.

Na hii ipo sana Arusha wale watu wa mawe wamesababisha sana mfumuko wa bei za ardhi bila sababu yoyote. Anapata vimilion vyake anaenda kuuziwa kiwanja kichwa kichwa matokeo yake anapandisha bei automatically viwanja vilivyo karibu yake.
 
Lukuvi kweli hapo umeongelea jambo la maana kabisa. Japokuwa nimesikia unasema eti almashauri zipate faida kwenye kupima viwanja! Hapa mimi nasema HAPANA, kazi ya kupima viwanja kwa Manispaa na Almashauri ni moja ya jukumu muhimu kwa niaba ya serikali kuu na kisiwe chanzo cha mapato.

Iweje sasa waanze kutaka kupata faida kwenye kupima viwanja? Tutiendekeza hizi faida hata kwenye Afya wataanza kulenga faida, Elimu itakuwa hivyo pia na mwishowe serikali itawahudumia matajiri tu.

Viwanja hasa mijini vinakuwa na bei isiyo na uhalisia. Ngoja tusubiri utekelezaji manake maneno matamu alikujanayo Prof. Anna Tibaijuka lakini hatukuona lolote!

Umemnukuu vibaya
 
Watu wanasahau kuwa ardhi ni mali ya umma...
Kwani lazima uwe speculator wa ardhi...si utafute biashara nyingine...????
Maana hii tabia ndio inafanya wazazi wawe na hofu na future za watoto wao na kufikiria kuwa na viwanja kadhaa...
Sheria ikiwa wazi hakuna atakaye kuwa na shaka...kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua kiwanja kwa muda wake...hakuna kulimbikiza...
 
Wazo ni zuri lakini limechelewa sana. Hakuna ardhi ya wananchi wa kawaida mijini bali wenyeji tayari wamenunuliwa. Moto utawaka pale Manispaa inapomfuata mwenye ardhi na kutakiwa kumlipa fidia stahiki. Ukute mwenye ardhi mwenyewe ana uwezo kidogo.

Kumbuka serikali ilivyopata shida kulipa wale wananchi wachache waliotakiwa kupisha ujenzi wa daraja la Kigamboni. Halmashauri itawaweza watu wa aina hiyo wakiamua kuweka misimamo ya hivyo?

Cha msingi ni serikali kuwapimia hivyo hivyo kwa gharama nafuu na kusimamia utaratibu wa mtu kutokuwa na viwanja vingi na visivyoendelezwa. Bei mbona itashuka yenyewe. Tukitaka kuua private sector serikali ifanye kila kitu tunaona slums nyingi kila kukicha. Watu watajenga holela tukisubiri siku manispaa itakuwa na uwezo wa kulipa fidia ili ipime viwanja na kuviuza kwa bei nafuu wakati watu hawana hata panadol vituo vya afya, vikao vingi vya kuchangia madawati, nyumba za walimu/Askari nk.

Hivi kwa nini kusiwe na sera zinazoongoza wizara ambazo kila waziri atatumia kwa miaka kadhaa? Juzi Tibaijuka, leo Lukuvi, Kesho??? kila mtu anakuja na mpango wake kama jeshi la mtu mmoja
 
Soko huria mana yake nini? Basi wapange kila kitu hadi bei za kona baa
 
Hii halmashauri iliyozuiliwa kuuza viwanja Ilitafuta ardhi, Ikapima, Ikaweka miundombinu kama barabara, umeme, maji nk. Huu ni mkopo wa bank. Tusubiri kusikia viwanja hivyo vinauzwa kwa bei elekezi ya bank.
 
Kwani mwenye kutoa vibali vya ujenzi ni nani? mwenye masterplan ya sehemu hiyo ni nani mpaka uropoke namna hiyo!?
Ficha ujinga wako kidogo. Mwenye shamba anaruhusiwa kuandaa mchoro wa mipangomiji. Hakuna sheria inayomlazimisha kukabidhi shamba lake halmashauri ili apimiwe na wao. Jielemishe kabla ya kubwabwaja hapa.
 
Hakuna kiwanja ambacho hakinunuliki labda kiwe hakiendani na bei hiyo! We uliyeshindwa kununua kiwanja una shilingi ngapi na unataka ununue wapi?! Nilionya kuwa taifa linarudi kwenye ujamaa kiaina.! Huu ni mfumo wa hovyo kabisa!

Huo UJAMAA ndio tunaupenda sana, urudi haraka
 
Personally nipo kwenye hii biashara ya viwanja mwaka wa pili sasa..alichokisema lukuvi ni either hakifahamu au amedanganywa au anatafuta sifa kwa mteule wake.
Hivi viwanja anavyovizungumzia vinapatikana kwa mbinde kuna njia mbali mbali zinafanyika ili kuvipata mpaka kuvipima
Njia ya kwanza..ni investor anakopa bank au anatoa pesa yake mfukoni ananunua ardhi anaiendeleza then anauza kutoka na na gharama alizotumia kuendeleza hiyo ardhi..
Njia ya pili ni kampuni ya upimaji inaingia ubia na wenye mashamba ya kupima mashamba yao then wanakubaliana malipo katika percentage kutoka kwenye eneo la shamba lake...
Baada ya kuendeleza uko kunabaadhi ya waendelezaji wanafanya uendelezaji wa maana wanavuta umeme na kusambaza Maji ktka kila kiwanja Barbara zinawekewa moram n.k wengine wanafanya partially tu..
Mh anavyosema hizi kampuni zinachokifanya sio sahivi Mimi binafsi simuelewi maana hizi Raman huwa zinapitiwa mpka kukubaliwa na baraza la madiwan,ofisi ya mipango miji,jiji mpaka kwa commissioner hawa wote wapo ofsini kwa mujibu wa sheria.
Nakumbuka kipindi cha nyuma mh wazir alishasema ili kuondoa migogoro ya ardhi wananchi wapime ardhi zao,
Upimaji wa ardhi ni wa ghari sio kila mwananchi anaweza kujipimia hizi kampuni zinauwezo zinasaidia kupika viwanja wazir yuleyule bado hataki anataka kampuni zifutwe..haya mambo sio siri serikali mnatuchanganya tumeinvest pesa zetu tumeajiri vijana na sisi wenyewe pia tumejiajiri lakini bado serikali inatu discourage.
 
Ninachojua mimi ni kuwa serikali ndiyo inamiliki ardhi ya Tanzania. Sasa hawa wanao uza wameipata wapi?[/QUOTE

Mkuu ni kweli serikali ndo inamiliki ardhi yote Tz; ila inaruhusu wananchi wake kuikodi hiyo ardhi (ndo maana kwenye hati halali za viwanja za serikali wanatumia neno "lease"). Sisi huwa tunaita kununua ardhi ila kimsingi ni kwamba ukinunua ardhi kutoka serikalini Tz ni kama umekodi ardhi kutoka serikalini - pia unaruhusiwa kuuza hiyo haki ya kukodi kwa Mtanzania mwingine. Mwisho wa siku mmiliki wa ardhi Tz ni serikali tu peke yake. Na ina haki ya kuichukua ardhi yake anytime ikitaka. Bado tupo kwenye ujamaa in many ways. Na tunaukumbatia kwa kasi sana chini ya utawala huu. Binafsi naona huu siyo mwelekeo mzuri.
 
Isiishie Kwa kiwanja adi bei ya kuuza nyumba n kupanga nyumba iwe elekezi
 
Kwako mheshimiwa lukuvi.
Kuna kampeni ya kurejesha nyumba za setikali sababu hazikuuzwa kihalali...nyumba za mabilioni zikauzwa kwa million 20.
Tukiacha hayo kama hapa tunaongea haki...hizi nyumba zote ziliuzwa kwa masharti. Moja ikiwa kutouzwa au kufanya any deal kwa miaka 25..
Inakulikana wazi karibu 80% ya wamiliki wamekiuka masharti haya kwa kuzitoa kwa long lease au kuuza kwa ujanja na kufanya JV.
Hayo waziri unayafahamu kama muko kweli kea ajili ya wana nchi zirejesheni hizi nyumba...au msinipendekeze kuwa mna fanya haki
 
Pigo lingine kwa walalahoi, na kicheko kwa walichonacho. Ardhi ndiyo rasilimali inayookoa watu huko vijijini, halafu eti upangie bei ili walichonacho wanunue kwa bei nafuu!
 
He spewed a lotta hot air na lugha za dharau kwa wananchi. Watu wametumia sheria za nchi kutafuta pesa we unasema "imekuwa kwao." .

Mambo ya ardhi hayaendi kwa amri za Waziri! There is a LAND ACT of 1999! Wewe Waziri huna mamlaka ya kuharamisha "kuanzia leo" utaratibu uliopo wa matumizi ya ardhi.

Unless kitu hicho kilikuwa tayari hakiruhusiwi. In which case na wewe unatakiwa utumbuliwe kwa sababu umekiri bungeni kwamba jana "wamempa" mtu hati 600. Wamemka, kina nani wamempa, UKAWA? Wewe na Kamishna wa Ardhi ndio mnatoa hati, nyinyi wawili mtumbuliwe!

Ukisikia mtu anasema "kuanzia leo marufuku" ujue somebody alikuwa hafanyi kazi yake! Yeye Lukuvi is responsible for Land Ministry malfeasance.

Anaongea bungeni utadhani anatoa lecture kwenye warsha elekezi ya wakurugenzi wa H/shauri. Kawaambie huko huko watu wako, sio kugombeza wananchi bungeni! Hebu heshimuni raia! Tunataka serikali inayofuata sheria za nchi, sio kuendeshwa na amri na marufuku!
 
Hakuna kiwanja ambacho hakinunuliki labda kiwe hakiendani na bei hiyo! We uliyeshindwa kununua kiwanja una shilingi ngapi na unataka ununue wapi?! Nilionya kuwa taifa linarudi kwenye ujamaa kiaina.! Huu ni mfumo wa hovyo kabisa!
We acha ubwanyenye serikali Ya gani ni makini ili kuwakumboa watanzania wa kawaida. Viwanja havinunuliki kwa mantiki Ya maisha ya kawaida ya mtanzania.ni kipindi kifupi tu hii issue Ya viwanja Na Nyumba vimepaa kupita maelezo na kwa uhalisia uwezo ulibaki kwa mafisadi na Watu wa kuja kama wahindi wakati wazawa wa kawaida wakikosa uwezo wa kumiliki ardhi yao. Serikali kwa kufanya hivyo itasaidia wengi ambao tulishakata tamaa Ya kumiliki ardhi.
 
Lukuvi kweli hapo umeongelea jambo la maana kabisa. Japokuwa nimesikia unasema eti almashauri zipate faida kwenye kupima viwanja! Hapa mimi nasema HAPANA, kazi ya kupima viwanja kwa Manispaa na Almashauri ni moja ya jukumu muhimu kwa niaba ya serikali kuu na kisiwe chanzo cha mapato.

Iweje sasa waanze kutaka kupata faida kwenye kupima viwanja? Tutiendekeza hizi faida hata kwenye Afya wataanza kulenga faida, Elimu itakuwa hivyo pia na mwishowe serikali itawahudumia matajiri tu.

Viwanja hasa mijini vinakuwa na bei isiyo na uhalisia. Ngoja tusubiri utekelezaji manake maneno matamu alikujanayo Prof. Anna Tibaijuka lakini hatukuona lolote!
Huwezi amini kuna makampuni yalikuwa yanakwea msafara wa Raisi kuja ulaya kunadi viwanja ardhi ambayo marehemu baba wa Taifa aliilinda kwa nguvu zake zote na ndo maana alikataa ardhi isiuzwe kama njugu na kuna mzungu mmoja nilibahatika kukaa nae meza moja akawa ananiambia anamiliki ekari kama Mia tano Arusha ( not sure exactly ) ila akitaja eneo moyo unakufa ganzi. Wakati huo huo mtanzania aliyepata uraia nje haruhusiwi kumiliki ardhi. Hatua za Mh lukuvi zimechelewa na Inabidi aje na gear Ya kutuomba radhi watanzania kwanza kwa Sababu ni serikali hiyo hiyo imetufanyia hayo madhambi na kufuru baada Ya baba wa taifa kukabidhi mikoba.
 
Back
Top Bottom