Kwa mara ya kwanza sasa. Afadhali sasa nakuona umeanza kulegea. Maana ulikuwa unakomaa. Kila kitu unapinga tu. Mpaka ni kashangaa hivi huyu katokea sayari gani?
Mkuu, kupinga kila kitu ni vibaya kama vinvyowekwa mezani havina maana?
mfano hoja hizi hapa tano:-
1. Hakuna kubadili katiba kwa sababu iliyopo inatulinda sana sisi watawala dhidi ya makosa ya kibinadamu.
2. Wakulima watatoa kodi za mazao yakiwa shambani na ruzuku ya mbolea tunaondoa ili kujenga dhana ya kujitegemea.
3. Wanafunzi watalipa kodi ya kupata elimu kabla hawjafanya mitihani ya mwisho ili kuongeza pato la taifa.
4. Watumishi wa umma wanaoitwa wataalam kuanzia sasa wataajiriwa kwa kura za wananchi kwa sababu tunahitaji wafanyakazi wanaokubalika na wananchi ili kurejesha heshima ya serikali.
5. Makosa yote isipokuwa yanayohusika na uhaini, yataamuliwa na kamati ya usalama ya halmshauri za vijiji ili kupunguza msongamano wa kesi mahakamani na kupunguza rushwa mahakamani.
MKUU, ILI MTU AWE SAFI KWAKO, ANATAKIWA ASIPINGE MANGAPI HAPA NA YAPI HASA?