Lukuvi: Mbunge, Mkuu wa Mkoa, M/kiti bodi ya wakurugenzi wa taasisi ya Umma!

Hivi kwa nini mtu mmoja agawiwe nyadhifa hizi mbili wakati kuna raia wema kibao wanaranda huku na huko kuyatafuta maisha bora kwa kila Mtanga na nyika (Mtanzania). Wana nini cha kipekee ambacho wengine hawana?. Haya mambo yangeishia kwenye CCeM lakini siyo kuletwa hadi serikalini.

Huu ni uroho wa madaraka
 
Jamani nadhani wengi mmeshaona kitu kama hiki kikitokea katika serikali yetu!!. Hivi mantiki yake hasa ni nini??. Maana yake ni kwamba mtu huyo ni mchapa kazi sana au ni mroho wa madaraka, au ana agenda fulani na mtawala mkuu ambaye ndiye mteuzi wa nafasi za kuteuliwa?
Je ni kweli hakuna watanzania wngine wanaoweza kushika nafasi nyingine??
Je wana JF mnajungumziaje Ufanisi wa Utendaji wa mtu kama huyu!? Mfano ni Mh W.Lukuvi. Mbunge, na Mkuu wa Mkoa!. WHYYY? HATA HAYA HAWANA!! MTU ANAKALIA MADARAKA LUKUKI??
 
Lakini Ni kwa nini hili swala lisipigiwe kelele, ili hata wenye hizo nafasi waone aibu kwa jamii? Ifike wakati Mtu kama ana nafasi fulani halafu anateuliwa kushika wadhifa mwingine zaidi akatae kwa kuhofia aibu kwa umma.
 
Wana JF,

Hayo nimeyaona huku mikoanai na nadhani watu wanadhani kuwa na vyeo vingi ndio kiongozi bora.

Na wengine wanataka kugombea nafasi mbili kama Kimbisa Mayor wa JIJI Dar huku anataka udiwana na Ubunge Dodoma Mjini huku anamikashfa kibao nadhani CCM nao waangalie wale wanao tangaza nia kupitia CCM hiyo siyo Democracy kila anae taka kutangaza nia mwamkubali hamuangalii kama anamapungufu anachafua chama jamani CCM muwahangalie hawa watu kama wakina kimbisa ni kazi bure tuu ameshindwa huko Kondoa anang'ang'ania Dodoma Mjini apewe ubunge naninasikia anamwaga pesa kwa makatibu kwa kwenda mbele si kukichafua chama sasa hapo??
 
Madaraka mengi ya kuteua yasiyohojiwa wala kuthibitishwa na chombo kingine chochote aliyonayo Rais wetu KIKATIBA ndio chanzo cha yote haya. Rais wetu ni Mungumtu katika baadhi ya mambo.
 
Wana JF,

Hayo nimeyaona huku mikoanai na nadhani watu wanadhani kuwa na vyeo vingi ndio kiongozi bora.

Na wengine wanataka kugombea nafasi mbili kama Kimbisa Mayor wa JIJI Dar huku anataka udiwana na Ubunge Dodoma Mjini huku anamikashfa kibao nadhani CCM nao waangalie wale wanao tangaza nia kupitia CCM hiyo siyo Democracy kila anae taka kutangaza nia mwamkubali hamuangalii kama anamapungufu anachafua chama jamani CCM muwahangalie hawa watu kama wakina kimbisa ni kazi bure tuu ameshindwa huko Kondoa anang'ang'ania Dodoma Mjini apewe ubunge naninasikia anamwaga pesa kwa makatibu kwa kwenda mbele si kukichafua chama sasa hapo??
Kwakweli hii tabia inabidi ikomeshwe mara moja!! Hivi hata watu wanaowachagua hoo watu wao wanajisikiaje kumchagua mtu ambae anamavyeo mengine lukuki, inamaana miongoni mwao wapiga kura hakuna mtu anaeweza kuchukua hizo nafasi? Tusiwachague watu wenye majukumu mengine ya uongozi wa umma tafadhali. Tuwaulize, wewe si ni kiongozi tayari?. Swali hili lianzie kwenye uteuzi wa kugombea ndani ya chama kwanza.
 
Heshima kwako Analysti,

Ukweli hata mimi nimekuwa nikishangaa sana jinsi mambo yanavyopelekwa.Nadhani mtu wa kwanza kuanzisha utaratibu huu ni marehemu Mwl J K Nyerere sijui wakati huo kulikuwa na uhaba wa watu wenye sifa au vipi.Utaratibu huu umeendela si kwasababu ya kukosa watu wenye sifa bali to accomodate watu kwa faida za kisiasa zaidi.Mfano mzuri ni Lukuvi na mkuu wa mkoa wa Mwanza na Mbeya majina nimeyasahau hawa walikuwa ni wanamtandao ambao pamoja na Muungwana kuunda baraza kubwa la mawaziri walishindwa kuwemo wakatafutiwa nafasi za ukuu wa mikoa ambayo tunazidi kuongeza kwa minajili ya kuwatafutia wateule nafasi.
 
Ni kweli, hiyo ndo ilikuwa mantiki enzi zile za nyerere, tena Mwanzoni!. Lakini Hivi sasa wasomi ni Lukuki, tena wamebobea kwelikweli. Inakuwaje hawa wakuu waendeleze huu mchezo. Tena baadhi ya hao wateule elimu zao zinatiliwa mashaka e.g. Lukuvi. Nafikiri imefika wakati sasa suala hili livaliwe njuga!. Kuna kijana alimuuliza swali hili mh Kikwete kule Mwanza wakati wa kampeni 2005, yule kijana akasumbuliwa sana na usalama wa taifa. Turekebishe mambo
 
Naomba kusahihisha kidogo,Aliyeulizwa swali alikuwa E Ngoyai Lowassa wakati huo alikuwa waziri mkuu kabla ya kashfaa ya RICHARDMonduli
 
Dear Brothers & Sisters,

Tz is ours, we are responsible to shape it the way we wish, no body else will do.
Keep shouting on these vices, God is with us and ours is victory at the end of the day!
This is another form of graft!
 
Hivi kwa nini mtu mmoja agawiwe nyadhifa hizi mbili wakati kuna raia wema kibao wanaranda huku na huko kuyatafuta maisha bora kwa kila Mtanga na nyika (Mtanzania). Wana nini cha kipekee ambacho wengine hawana?. Haya mambo yangeishia kwenye CCeM lakini siyo kuletwa hadi serikalini.

acheni wivu... khaa!! kama vipi na nyie gombeeni nyazifa zinazogombewa..... uchaguzi ndio huu...!!!
 
Cha kubadilika hapa ni katiba hii fake tuliyonayo inayompa madaraka rais kumiliki hata mkeo bila kuulizwa na chombo chochote.

Mnataka mabadiliko, tuungane kudai katiba mpya. Nashauri iwe ni mkakati mpya kwa ajili ya mwaka 2011/2015
 
Hata kama katiba inaruhusu ila hata Rais mwenyewe(anayeteua) atleast awe na aibu kwa hili. inamaana nchi nzima ni yeye tu Lukuvi ndo kiongozi! hakuna mwingine anayeweza kuwa Mkuu wa Mkoa!!
 
Cha kubadilika hapa ni katiba hii fake tuliyonayo inayompa madaraka rais kumiliki hata mkeo bila kuulizwa na chombo chochote.

Mnataka mabadiliko, tuungane kudai katiba mpya. Nashauri iwe ni mkakati mpya kwa ajili ya mwaka 2011/2015

Wenzetu Kenya wamepiga hatua sana kwenye hili la KATIBA. Kuna wakati UKABILA unasaidia kusukuma baadhi ya mambo.
 
Haya mambo ya mwenzetu ndo yanayopunguza ufanisi..
Haijalishi uwezo..
Tukomae na Katiba mpya basi..!!1
 
Huu ni uendawazimu. Inawezakutokea kwa mtindo huu MBUNGE + RC + WAZIRI. It is possible ONLY in Tanzania.
Bob... hiyo haiwezi kutokea... its either RC or Waziri but sio vyeo vyote viwili kwa wakati mmoja
 
Hivi kwa nini mtu mmoja agawiwe nyadhifa hizi mbili wakati kuna raia wema kibao wanaranda huku na huko kuyatafuta maisha bora kwa kila Mtanga na nyika (Mtanzania). Wana nini cha kipekee ambacho wengine hawana?. Haya mambo yangeishia kwenye CCeM lakini siyo kuletwa hadi serikalini.

Kichankuli... unashangaa hilo?? mbona cha mtoto

Hebu oanisha hivyo vyeo na elimu yake ndio upate kushangaa vizuri zaidi
 
Back
Top Bottom