Lukuvi: Mbunge, Mkuu wa Mkoa, M/kiti bodi ya wakurugenzi wa taasisi ya Umma!

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Hivi kwa nini mtu mmoja agawiwe nyadhifa hizi mbili wakati kuna raia wema kibao wanaranda huku na huko kuyatafuta maisha bora kwa kila Mtanga na nyika (Mtanzania). Wana nini cha kipekee ambacho wengine hawana?. Haya mambo yangeishia kwenye CCeM lakini siyo kuletwa hadi serikalini.
 
Kuna mwanafunzi mmoja wa shule moja iliyopo kanda ya Ziwa aliwahi kumuuliza Waziri Mkuu EL kuhusu mtu kupewa Ukuu wa Mkoa akiwa mbunge. EL alijibu maswali ya wananchi wote wa hapo isipokuwa la huyo kijana ambapo aliahidi kulijibu atakaporudi tena. Bahati mbaya mambo ya Richmnd yakapitia hapo na EL akaachia ngazi kabla hajarudi tena !!! Labda Pinda atarudi kujibu kwa niaba ya aliyemtangulia !!!
 
Huu ni uendawazimu. Inawezakutokea kwa mtindo huu MBUNGE + RC + WAZIRI. It is possible ONLY in Tanzania.
 
Sioni sababu za msingi kwa mtu kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na wakati huo huo anashika nafasi ya Mbunge. Kwa maoni yangu, mtu huyo hataweza kuwa na ufanisi unaohitajika katika nafasi zote mbili. Na asipokuwa makini zaidi, anaweza asifanikiwe kabisa katika utekelezaji wa majukumu yake yote ya uongozi hasa akiwa ni Mkuu wa Mkoa ulio mbali na Jimbo lake (kama ni Mbunge wa kuchaguliwa). Ni sawa kabisa na ninavyoamini kuwa Waziri asingefaa kuwa Mbunge.

Ila kwa upande mwingine, Rais anayo mamlaka ya kumteua mtu yeyote kuwa Mkuu wa Mkoa wowote ndani ya Tanzania bara bila kujali wadhifa mwingine wowote wa kisiasa alionao. Nafasi ya Mkuu wa Mkoa ni nafasi ya kisiasa zaidi, hivyo Katiba ya Muungano haimnyimi mtu nafasi ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.

Kwa mtazamo wangu pia, ingekuwa busara kwa Rais kutoteua waBunge kuwa Wakuu wa Mikoa ili kuongeza ushiriki wa wananchi wengi zaidi katika nafasi za maamuzi.
 
Huu ni uendawazimu. Inawezakutokea kwa mtindo huu MBUNGE + RC + WAZIRI. It is possible ONLY in Tanzania.

Hii pia inawezekana kama Rais ataamua kufanya hivyo. Ila mtu huyo atakuwa anashika nyadhifa mbili ndani ya serikali moja inayoongozwa na Rais mmoja. Katiba haimzuii mtu kuwa na nafasi hizi mbili kama anayo sifa ya kuwa Mbunge.
 
Hilo ni swali ambazo wagombea wa uraisi msimu ujao waulizwe, na agenda iwe wafute huu wendawazimu.
 
Huu ni uendawazimu. Inawezakutokea kwa mtindo huu [B]MBUNGE + RC + WAZIRI[/B]. It is possible ONLY in Tanzania.

Naipenda sana JF ila wakati mwingine nikisoma madudu kama haya, hujikuta siku yangu ikiharibika! Inakera sana kwakweli!
 
Roho ya Fisi.

Greed! Pupa, ukiritimba,kufakamia. Uroho, Ujinga ujuvi.

Sasa afadhari madaraka hayo akipewa mtu mwenye uwezo,
Kumpa mtu kama Lukuvi aongoze mkoa, kisha arudi Isimani akasikilize matatizo na kukaa kujadili pamoja na wananchi wa Isimani ili kuyatatua, hiyo multi tasking ataiweza wapi?
 
Huu u RC wanapewa wale ambao wamepata ubunge au wamekosa lakini ni watu wamuhimu kwa mhusika (mkuli) either ni watu wake wakaribu ama maadui ambao usipowapa chakufanya watakumaliza (that is how the state works) wale wa katikati waliokosa ubunge wanapewa u DC na makada wengine wanaojengwa for future positions... nashangaa watu wana lalamika nini wakati ndio system yetu yakijinga.. Utadhani rais ni Stalin.. Kwamfano Lukuvyi was in Malecela's camp with kina Chenge na Msekwa but it would not be smart for JK kumuacha Mbunge tuu because hapo jamaa atashine... lakini kwasababu Ukiwa RC wewe ndio unakukwa assimilated into what is known as 'watawala' huwezi jitofautishanao sana ata wakikosea.. Kumpa uwaziri inakua ngumu kwasababu kunakuwa na watu wengine wakaribu zaidi ambao inabidi fadhila iwarudie.. (its a political trick)...
 
Sijui hapa Marekani ni vipi mtu anaweza kuwa Gavana wa State na Senator kwa wakati mmoja??

Hapa kuongoza hata District tu ni lazima kichwa kikuume kila siku.

Watu wanarundikiwa madaraka kwa sababu hawawajibiki kwa wananchi ila kwa aliyewateua. Mtukufu Rais.
Sifa moja kubwa ya kuwa kiongozi Tanzania ni ujasiri wa kuharibu mambo bila kuogopa wananchi, kulinda maslahi ya aliyekuchagua hata kama itabidi watu ndani ya eneo lako la kujidai wafe kwa kula uyoga wenye sumu kwa njaa.

Pia kuna hili la ukinyonga wa Wabunge wafikapo Bungeni kugeuka Watumishi wa serikali na kuwasahau wananchi. Hili ni jambo moja linalowapa nguvu ya bandia ya kudhani kwamba wanweza kutumikia serikali kuu moja kwa moja bila kuleta migongano ya kimaslahi.

Mbunge ni mtu wa wananchi Mkuu wa mkoa ni mtu wa serikali kuu, vitu hivyo viwili ni Ardhi na mbingu.


Mtu mwenye hekima na upeo atatoa taarifa kwamba mkoa wa Dodoma una njaa mkuu wa mkoa atasimama na kusema hakuna njaa, watu wanaosema kuna njaa ni watu wanaopinga maendeleo ya mkoa wa Dodoma.
Wakuu wa Mikoa hawafiki vijijini labda rais awe anatembelea huku.
Wakiwa huko mikoani kama Iringa Mbeya na Rukwa macho na masikio yao huelekezwa Dar kwenye mlo.
Ifike siku wananchi tubadiri katiba ili tuchague wakuu wa mikoa wetu wenyewe, watu watakao kuwa na uchungu na mikoa yetu kuliko Mamruk wanao wekwa na Mtukufu Rais amabo hugeuka kuwa watukufu kama aliyewaweka.
 
Last edited:
Sijui hapa Marekani ni vipi mtu anaweza kuwa Gavana wa State na Senator kwa wakati mmoja??

Hapa kuongoza hata District tu ni lazima kichwa kikuume kila siku.

Watu wanarundikiwa madaraka kwa sababu hawawajibiki kwa wananchi ila kwa aliyewateua. Mtukufu Rais.
Sifa moja kubwa ya kuwa kiongozi Tanzania ni ujasiri wa kuharibu mambo bila kuogopa wananchi, kulinda maslahi ya aliyekuchagua hata kama itabidi watu ndani ya eneo lako la kujidai wafe kwa kula uyoga wenye sumu kwa njaa.
Mtu mwenye hekima na upeo atatoa taarifa kwamba mkoa wa Dodoma una njaa mkuu wa mkoa atasimama na kudema hakuna njaa, watu wanaosema kuna njaa ni watu wanaopinga maendeleo ya mkoa wa Dodoma.
Wakuu wa Mikoa hawafiki vijijini labda rais awe anatembelea huku.
Wakiwa huko Iringa Mbeya na Rukwa macho na masikio yao huelekezwa Dar kwenye mlo.
Ifike siku wananchi tubadiri katiba ili tuchague wakuu wa mikoa wetu wenyewe, watu watakao kuwa na uchungu na mikoa yetu kuliko Mamruk wanao wekwa na Mtkufu Rais amabo wangeuka kuwa watukufu.

tufanyaje viongozi wawajibike .. maana tatizo limekuwa sigu hili, hata soni viongozi hawana. Wala haoni mtu kosa kutotimiza wajibu.
 
Nakumbuka mara moja Mh Ali Ameir kule Zanzibar alikuwa Mbunge wa jimbo la Donge, Mjumbe Baraza la Wawakilishi kuteuliwa na Rais, Waziri wa mambo ya ndani Tz, Waziri asiekuwa na Wizara maalum ZNZ (MBM), Naibu katibu mkuu CCM Zanzibar.
Kwenye CCM tena mjumbe wa vikao vyoote vya juu ZNZ na TZ kwa nafasi yake wakati huo.
Kila kitu possible Bongo
 
Wanabodi,
samahani mnapenda kupata darasa kidogo.. Hivi kuna ubaya gani ikiwa Mbunge ndiye awe DC na chini yake ktk utekelezaji kuwepo na Meya - Halmashauri za mji, kuondoa ile nafasi ya DC wa kuteuliwa..
Ni maoni tu napenda kufahamu utata utatokea wapi maanake sifahamu vizuri ngazi za uongozi na kazi zao.
Tuache kwanza swala la Mbunge+RC+madaraka mengineyo pembeni..
 
Wanabodi,
samahani mnapenda kupata darasa kidogo.. Hivi kuna ubaya gani ikiwa Mbunge ndiye awe DC na chini yake ktk utekelezaji kuwepo na Meya - Halmashauri za mji, kuondoa ile nafasi ya DC wa kuteuliwa..
Ni maoni tu napenda kufahamu utata utatokea wapi maanake sifahamu vizuri ngazi za uongozi na kazi zao.
Tuache kwanza swala la Mbunge+RC+madaraka mengineyo pembeni..

fafanua kidogo swali lako. unaaminisha nafasi ya RC isiwepo halafu ile ya DC ndio iwe ya mbunge na maye ndio afanye kazi ya DC? Kwa hiyo ungaongelea mfumo wa majimbo kwamba kutakuwa na mwakilishi wa jimbo, halafu wabunge wa mikoa na watendaji wa wilaya?
 
Hivi kwa nini mtu mmoja agawiwe nyadhifa hizi mbili wakati kuna raia wema kibao wanaranda huku na huko kuyatafuta maisha bora kwa kila Mtanga na nyika (Mtanzania). Wana nini cha kipekee ambacho wengine hawana?. Haya mambo yangeishia kwenye CCeM lakini siyo kuletwa hadi serikalini.

....Umeshawahi kuona mtu anapiga kona kisha anakimbilia kuuwahi mpira afunge golini?? soma hii...

Baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge (mwanaCCM) anaingia moja kwa moja ktk baraza la madiwani, pili anaweza kuteuliwa kuwa waziri, RC (RPC?), DC, halafu huyoooo kuwa mjummbe au mwenyekiti wa bodi fulani nyeti. hajakaa sawa anasikia kaharufu kataaaam kanamwita chamani (uchaguzi wa ndani) ambapo anakwenda kugombea kuwa mjumbe wa mkutano mkuu, kamati kuu au mwenyekiti wa mkoa au takataka nyingine.
Sasa kona ndo hii hapa...
Wakishaboronga serikalini, haoooo wanakimbilia chimwaga kukaa na kutathmini kazi na utekelezaji wa ilani (waliyotumwa kuitekeleza). Kwa hiyo wanakuwa CUM MAKADA. wanatunga ilani, wanaitekeleza, kutathmini utekelezani na kujipongeza (kujiwajibisha).

Na ukiwakuta wakati wanapigana vikumbo mikoani kugombea nyadhifa za chama utawahurumia. Hapo ndipo utagundua kuwa wanamtaja Mungu ila ktk akili zao huyo Mungu ha-exsist kamwe. Kutwa kuchwa kutafuta njia za kutoana roho ili muradi wapate nafasi.

Hii ndiyo biashara na soko la KURA.

hakika NAWAAMBIENI hata aje malaika kututawala, kwa mfumo huu hakutakuwa na muujiza. na tusitafute mchawi wa umasikini wetu. mchawi ni mfumo wetu halafu ni mimi na wewe kwa kujifanya shingo ngumu tusiotaka kubadilika.

Naomba kutuma salam.....
 
Back
Top Bottom