Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,875
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema serikali itavunja nyumba zote ambazo zimejengwa katika maeneo hatarishi na mabondeni bila kujali kuwa wamiliki wake wana hati miliki za viwanja.
Lukuvi, alibainisha hayo jana jijini hapa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya sekta ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kwa waandishi wa habari katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.
Alisema kwa mujibu wa sheria wananchi hawaruhusiwi kujenga katika maeneo hatarishi pamoja na mabondeni na kwamba yeyote atayekaidi serikali itabomoa bila kujali kuwa anayo hati miliki ya kiwanja chake.
“Miaka ya nyuma fedha ilikuwa na nguvu kuliko sheria hali ambayo ilifanya hata watumishi wa wizara yetu kutoa hati katika maeneo hatarishi na mabondeni kama vile bonde la mto Msimbazi,” alisema Lukuvi.
Vilevile, alisema serikali ipo kwa ajili ya kulinda wananchi wake na hatokuwa tayari kuacha watu kujenga katika maeneo hatarishi na kwenye mabonde.
“Kama kuna mtu amejenga katika eneo hatarishi tukigundua tunakuvunjia bila kujali kuwa unayo hati maana yake kuna baadhi ya hati watu wamepatiwa kiujanjaujanja bila kufuata taratibu ndiyo maana unakuta watu wanajenga katika maeneo kama vile bonde la Msimbazi,” alisema Lukuvi.
Kutokana na hali hiyo aliwaagiza watumishi wa wizara hiyo kuacha kufuata hisia za watu kwenye utoaji wa hati katika maeneo hatarishi na mabondeni.
“Ukipewa hatimiliki ya eneo katika maeneo hatarishi na kwenye mabonde imekula kwako kwani tukibaini tu lazima tukuvunjie,” alisisitiza Lukuvi.
Akizungumzia kuhusu malalamiko yanayotolewa hivi sasa na wananchi kuhusu malipo ya fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na serikali kwa ajili ya kupisha miradi ya kimkakati kama wa SGR, alisema suala la fidia sio hisani ni lazima kwa mujibu wa sheria.
Alizitaka taasisi zote za serikali zilizochukua maeneo ya wananchi kwa ajili ya miradi mbalimbali kuhakikisha kuwa zinawalipa fidia kwa mujibu wa sheria.
“Suala la kulipa fidia siyo hisani ni lazima kwa mujibu wa sheria kwani sheria inasema kuwa ukimcheleweshea mtu malipo yake ya fidia ndani ya miezi sita unatakiwa kumlipa na riba na ukichelewa kwa miaka miwili tathmini inabidi ifutwe na ifanyike nyingine hivyo wahakikishie watu wote ambao wamepitiwa na miradi ya umma kuwa watalipwa,” alisema Lukuvi.
Kadhalika alisema hivi sasa serikali imetoa Sh. bilioni 50 kwa halmashauri nchini kwenda kufanya upimaji wa ardhi pamoja na upangaji wa miji ili kuwezesha wananchi kupata hatimiliki za maeneo yao.
GAZETI LA NIPASHE