Lukuvi aruhusu malori kubeba wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi aruhusu malori kubeba wanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 10, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  10th February 2010

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, ametoa ruksa kwa malori, kenta, magari ya wazi kuwasafirisha wanafunzi wanaosoma nje ya Jiji.
  Alitoa agizo hilo jana akiwa katika ziara ya kukagua shule za sekondari wilayani Ilala.
  Lukuvi alisema vitatolewa vibali kwa magari yatakayoomba kutoa huduma hiyo kupitia kwa mkuu wa wilaya ili Polisi wa Usalama Barabarani wasiyakamate.
  Aidha, alitoa wito kwa watu binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga mabweni kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule zao.
  Lukuvi alitembelea shule ya Msongola, Kivule Abuu, Jumaa, Vingunguti pamoja na Gerezani ambapo wanafunzi walimueleza kuwa wanakabiliwa na matatizo ya usafiri, uhaba wa walimu na ukosefu wa mabweni.
  Akiwa katika Shule ya Sekondari Abuu Jumaa, Lukuvi aliwakuta baadhi ya wanafunzi wamekaa chini na Sekondari ya Kivule wakiwa wamekaa kiti kimoja wanafunzi wawili lakini kila mmoja na dawati lake.
  Alimuagiza Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bernard Mkali, kuorodhesha majina ya wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa shule za mbali kuwapa uhamisho kuanzia leo ili waepukane na adha hiyo.
   
 2. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hivi sisi ni watu wa aina gani?

  Kama daladala ambalo limeundwa kwa ajili ya kubeba watu, matumizi ya mafuta ni kidogo, yanakataa kubeba wanafunzi. Leo hii unaruhusu malori, ambayo hayana hata safety measure yoyote kubeba abiria, yanatumia mafuta mengi zaidi, eti wabebe wanafunzi.

  Swali:"Haya malori yatabeba wanafunzi bure au kwa gharama?"

  Kwanini kusiwe na mpango madhubuti wa kusajili magari (daladala) ambazo kazi yake ni kubeba wanafunzi @ a given time range with incentive kutoka serikalini kusuluhisha hii ishu?

  Ukiangalia kwa wenzetu ni rahisi ku-control internal affairs kwa sababu watu wao wanatambulika. Sisi karibu tunatimiza miaka 50 ya uhuru lakini hatujui hata nani ni raia na nani ni mgeni. Budget zetu si halisi. Yaani tunakurupuka tu na mambo.

  AAAGH! BONGO INANIKERA SANA!
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,468
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hii habari imenitia kichefuchefu kabisa! Kuna mahala fulani humu JF nimesoma kwamba Lukuvi aliishia darasa la saba, nikaona watu sasa wanaongeza chumvi. Ila sasa nimeamini. Hatimaye nimeanza kupata mwanga wa tatizo letu Watanzania kutokuwa na maendeleo ni nini. TATIZO ni kuwa na viongozi VILAZA!!!
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,227
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Pole ndugu yangu usikereke, si unajua tena kila kitu hapa kwetu solution ni zimamoto. Kesho atakuja mwingine atasema basi wenye punda wanaweza kutumia kubebea watoto wao kenda shule.

  Mradi ametamka na amesikika.
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 23,167
  Likes Received: 6,874
  Trophy Points: 280
  na hakuendelea kwa sababu ya kupanda malori kule kwao isimani
   
 6. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 747
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  We still have many miles ahead of us.Hivi haya maneno/solution kurupushi wanatoa wapi?.Kweli ukiwa mkimya unahesabiwa hekima.
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,098
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  MNAOCHONGA BILA KUKUTANA NA HALI HALISI HII NI SALAMU YENU.....!
  HEBU PATA WASAA WA KUTEMBELEA HIZO SHULE.......ANGALIA MAZINGIRA KUANZIA ASUBUHI MPAKA JIONI.....!
  HALAFU NJOO HAPA JF HUKU VIDOLE VYAKO VIKIWA NA HAMU YA KUBOFYA NA UKICHUKUA NAFASI YA MTOA MAAMUZI UONE NI USAFIRI GANI UTARUHUSU KWA VIJANA WALE.....!
  Hali ya usafiri kuelekea njia ile ni ngumu mno, hayo malori yanayozungumziwa ni kwa sababu yanaenda shamba ama kufata mchanga......!
  na wakato yanaenda yanaenda tupu...ni vigumu kuwapita wanafunzi huku nawe unaelekea huko huko......!
  AU WAPINGA MADA MPO ALASKA NINI?
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,931
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  kwa swala la malori kubeba wanafunzi hapa swala la usalama wa wanafunzi ndio tatizo.kwanini serikali isitoe mabasi yao kufanya uduma hio kwa wanafunzi?
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Lukuvi amefikiria mbali!
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Masa hii ni tooo much jamaniwewe lol!!
   
 11. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,614
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  tukiona inafaa tuiruhusu sio mbaya, mbona wengi wetu huwa tunatumia usafiri wa malori tukiwa vijijini,, sioni kama kuna ubaya.........
   
 12. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,158
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  Mkuu mahesabu naona wewe ni mwenzangu na mimi wa ''MANEROMANGO''......! watu wanazungumza tuuuuuu hawajui hata what is going on here!

  Kuna maeneo mengi sana ya pembezoni mwa jiji la Dar, huko hata dala dala moja haliendi ni malori ya mchanga, macanter ya mihogo basi.....huko, zimejengwa shule za kata.....na mpk sasa (b4 hilo tamko la Lukuvi) tayari wanafunzi usafiri wao mkuu ni hayo malori......kilichotokea hao wenye malori wamelalamika kwa RC kwamba wanakamatwa na Traffic kwa kupakia wanafunzi tena bureeeee......so RC anakuja na temporaly vibali, ili hawa wenye malori wasikamatwe wakati wanatoa msaada huo.....sasa mnataka hao watoto waende vipi shule for now?

  Kama serikali imeshindwa kupeleka huko walimu, vitabu, maadara, madawati etc, do you expect inaweza nunua mabasi ya kupeleka huko wanafunzi? Mnaona mtokeo ya FIV ....65,000 ni zeros??????? can't you figure out what is happening huko kny hayo mashule mazee?
   
 13. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 414
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Basi kama vp ile project ya mabsai yaendayo kasi sana wanayoihubiriga hawa watukufu waiahirishe, watoe tu mabasi yaendayo slow kama uda vile yakafanye hizo kazi za kubeba wanafunzi! Mbona uda zilivyokuwepo zilikuwa zinasaidia sana wanafunzi!
  Mi naona tuachane na mabasi yaendayo kasi kwani ni jambo la kufikirika hilo, tu deal tu na mabasi slow yawasaidie wanafunzi!!!!
   
 14. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,316
  Likes Received: 29,041
  Trophy Points: 280
   
 15. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 4,278
  Likes Received: 4,440
  Trophy Points: 280
  He must be joking. Hii nchi mbona ina mazingaombwe kupita mazingaombwe yenyewe kwa kweli hii ni kali ya mwaka 2010. Kuwapakiza watoto kwenye malori wakati wao wanaendesha magari ya kifahari kwa nini waziuze hayo magari yao wananunue usafiri kwa shule hizo period. Kuna waziri yeyote au mkuu wa mkoa yeyote wa Tz. atakubali mtoto wake apandishwe kwenye lorry? Lukuvi waonee imani na huruma watoto hawa sema jingine kwa hili umechemsha kidogo ndugu mheshimiwa
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,158
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ..umeyaona matokeo ya FIV ya mwaka huu mjomba?
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  kwa watu wa pugu, kibiti, minaki, mringa nk. hili si jipya... lakini tunaomba iwe short term solution; mimi nilifaidi pia zile basi za wanafunzi

  kuna haja ya kuandaa mkakati (hata ikibidi kwa pesa ya rada) wakuu wa dr kuandaa mkakati wa mwanafunzi salama ambao uta-address mahitaji ya wanafunzi wa dar kuanzia chakula, elimu, ulinzi hadi mahitaji mengine

  sina hesabu zozote lakini siamini kama utakua pesa nyingi kama zile zinazoibiwa kila siku
   
 18. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Bado haijaniingia akilini yani mwenye Gari aende kuomba kibali cha kupakia waafunzi bure...au?
   
 19. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Lakini Tanzania hii watu hawataki kufikiri kabisa. Na pia hawataki maoni ya wengine eti kwa kuwa wao ni viongozi. Hili ni tatizo kuu linalotumaliza. Pia unafiki, unafiki na unafiki.

  Nilipopata bahati ya kujifunza maswala ya usafirishaji niliona kweli huku kwetu tunakwenda kinyume. Inabidi unapofikiri kuanzisha makazi upange na usafiri. Sasa huku kwetu sijui hata hizi shule zinaanzishwa mahali fulani kwa kuzingatia kitu gani? Mfano kuna shule kama FEZA mikocheni, Al-Muntazir nursery Upanga, Upanga nursery Azikiwe/Bi Titi, East African International School, na nyingine nyingi wamekubali zianzishwe bila kuangalia au kuzingatia town plan.

  Kwa kusema eti malori yabebe watu(wanafunzi) ni kinyume na sheria za usalama wa usafirishaji. Ina maana katika kipindi hiki tunachotaka kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani yeye Muhishimiwa anataka tuongeze.Hata kama tuna matatizo, jibu sio kuongeza matattizo dawa ni kutatua hilo tatizo.

  Kuna haja ya kuangalia distribution ya shule in relation to residence. Watoe study watu tuingie front tuwape solutions.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...