Lugha za Mahaba za miili yetu. Tambua yako !!

Lugha za Mahaba za miili yetu. Tambua yako !!

UmkhontoweSizwe

Platinum Member
Joined
Dec 19, 2008
Posts
10,047
Reaction score
9,346
Wauu, kuna 'lugha' tano (5) ambazo mwili wa binadamu huji-express jinsi mtu huyo alivyo kimahaba.

1. Watu wanaopenda kusifiwa: Hawa ni watu wanaojisikia sana wanaposifiwa hata kwa jambo dogo tu. Kusifiwa huwafanya wajisikie kupendwa na kuthaminiwa.

2. Watu wanaopenda zawadi: Watu hawa hufurahia sana wakipewa zawadi hata kama ni ndogo kiasi gani. Kuna wimbi kubwa la wasichana siku hizi kupenda zawadi ingwa wengi utakuta zawadi siyo 'lugha' ya miili yao. Watu ambao zawadi siyo lugha ya miili yao hupenda kuchagua zawadi gani wapewe (very picky), lakini wale ambao hii ni lugha ya miili yao hufurahia chochote wanachopewa kama zawadi. hujisikia kupendwa wanapozawadiwa.

3. Watu wanaopenda kukaa pamoja na kuongea: Hawa ni watu wanaopenda sana kukaa pamoja na ku-spend time na wenzi wao. Watu wenye lugha hii wanaweza kukaa na wenzi wao kwa maongezi hata kwa siku nzima, maana hivyo ndivyo miili yao inavyoji-express kimahaba. Asipopata muda wa maongezi, hata kama angepata mizawadi kiasi gani, anajisikia kuwa neglected na kutopendwa.

4. Watu wapendao kufanya mambo pamoja: Hawa ni watu ambao hufurahia sana kufanya kitu wakiwa na wenzi wao. Hata kama ni kakitu kadogo tu bado atataka mwenzi wake awe naye na wafanye pamoja maana ndiyo miili yao inavojisikia kimahaba.

5. Watu wapendao kuguswa: Watu hawa hupenda sana physical touch. Wanafurahia romance, hugs, kushikana mikono, kiss, na hata kufanya tendo la ndoa.

NB:
1. Inawezekana mtu akajiexpress kwa lugha zaidi ya moja kati ya hizo, lakini mara nyingi mojawapo huchomoza na kuwa dorminant.
2. Ni vizuri ukatambua lugha yako ya kimahaba ili uweze kumsaidia mwenzi wako kuielewa na kukutimizia.
3. Ni muhimu sana kutambua lugha ya mwenzi wako ili uweze kumtimizia kile mwili wake upendacho.

Mwisho: Ebu tambua lugha ya/za mwili wako na tuambie ni ipi/zipi.
Weekend njema.

UMK.
 
Wanajanvi help! utafanyaje kama anaye stahili kukufuta machozi ndiye asababishae ulie?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom